Maria Sarungi aishtaki Serikali ya Tanzania kwa Beyonce kuhusu suala la Ngorongoro

Maria Sarungi aishtaki Serikali ya Tanzania kwa Beyonce kuhusu suala la Ngorongoro

Anahangaika sana huyu mwanaharakati uchwara.

Wamasai sio Jamii ya kwanza kuhamishwa TZ. Watu Kila siku wanahanishwa kwa sababu mbali mbali za maendeleo from ujenzi wa miundombinu, maeneo ya jeshi, hifadhi nk.

Hawa wamasai wanalipwa fidia, kupewa maeneo mapya na kusafirishwa wenzao kule Mbezi Kimara walibomolewa bila fidia yeyote including nyumba ya Prof Jay.

Ardhi ni Mali ya serikali na Rais ndo custodian mkuu wake, hawa mayeroo watahama tu kwa hiari au shurti kama wanajiona special sana watakipata wanachokitafuta.
 
Wamasai
Naunga mkono hoja, Raise your voice to help the voiceless.

Wamasai wanalazimishwa kuondoka Ngorongoro kwa vipigo huku serikali ikitudanganya na maandamano feki ya "wamasai wa mjini"

Kumfurahisha mjomba kusiwaumize wamasai.
Wamasai waliojitokeza dar ubalozini sio wamasai ni wahuni wsliokulia mjini hata masikio yao ni ya kawaida. Pia kuna watu wanaitwa waarusha wanazurura mijiji wakijiita wamasai .
 
Ni katika muemdelezo wa sakata la wamasai wa Ngorongoro.

Bi Maria Sarungi ambaye ndiye mtu namba moja aliesimama kwa hali na mali kuwapigania Wamasai wa Ngorongoro ameamua kuishtaki serikali ya Tanzania kwa Mwanadada Beyonce na mumewe Jay Z.

Vita ya uchumi ni mbaya sana.

View attachment 2265420
Kwa nini Beyonce Sasa?
 
Nicheke kwa sauti,
Kwa hiyo Beyonce aje aichape serikali yetu,
Kumbe waeza kua kigagula lakini ukabaki na akili za kitoto.
Mbona nikama wewe ndo umeandika utoto.Jielimishe kwanza alichokua amekikusudia kukiwakilisha kwa jamii .sio mambo yakuchapana kama alivyowaza wewe kitoto.
 
Sisemi nasapoti yanayoendela NgoroNgoro, ila Maria ni mweupe sana kichwani sijui kwanini huwa anapata airtime!
 
Maria harakati anazofanya ni nzuri sana. Tujiulize kwa Tanzania kwasasa ni nani ana mzidi Maria kwa kuwa na influence kubwa kwenye mtandao wa Twitter?
 
Hoja yako Mbona hatuioni ?Unaongea kuwa Maria Hana hoja.Sawa yako ni ipi?

Hoja ziko wazi. Serikali ikitaka kutwaa eneo kwa masilahi ya Taifa ni suala la kisheria. Hakuna anayepaswa kupinga huo mchakato. Maana kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

Sasa huyu binti sarungi anachojua ni eviction, brutality na masai.

Wakati ile ni relocation ambayo inafuata kwa umakini kabisa a well prepared resettlement action plan na sheria zilizopo. Naomba niishie hapa.
 
Wamasai Ni moja ya vivutio hapo Ngorongoro

Yuko sahihi

Kama movie ya Royal Tour , hakuleta matekeo yoyote Basi Samia hajui lolote kuhusu Utalii.
Na hii kitu ita chafua sekta ya utalii

Kule wameongezeka sana. Hivi kwamba kama hatua yoyote haita chukukiwa kwa sasa miaka kumi ijayo Ngorongoro itakuwa historia. Uamuzi wa serikali kufanya hivyo uungwe mkono. Maana ni kwa faida ya Taifa kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Tatizo wenye dhamana ya kuelimisha hawafanyi mengi zaidi kuliko wapotoshaji. Wazushi wana tumia nguvu nyingi kuliko serikali inavyofanya.
 
Back
Top Bottom