Maria Sarungi alipewa na nani siri ya Ziara ya Rais Samia Nchini Marekani wiki moja kabla ya kutolewa Taarifa rasmi?

Maria Sarungi alipewa na nani siri ya Ziara ya Rais Samia Nchini Marekani wiki moja kabla ya kutolewa Taarifa rasmi?

SaSa wewe Lucas si umuulize Maria nani kampa taarifa za safari ya Rais ? Kuja hapa kutuuliza sisi ndo nini ?/
Huyu mshamba anamuonea wivu Maria, yaani kumlinganisha Maria na Lucas katika tasnia ya habari ni sawa kulinganisha Treni ya SGR na bajaji Lucas akiwa ndiye bajaji.
 
Asante sana mkuu Pascal kwa ufafanuzi mzuri, wewe ni mwanaccm unayejielewa hatuna shaka na uwezo wako, ila huyu Lucas Mwashamba ni mzigo kwenye chama chenu msaidieni.
Asante sana kwa compliments zako kuhusu mimi, ila huyu dogo sio mzigo, ana kipaji kikubwa na uwezo mkubwa hivyo ni asset muhimu kwa CCM, haswa kwenye kujibu hoja za mitandaoni, sisi wazee hatuwezani na speed ya social media, madogo hawa wanaweza.

P
 
Mwanamke mwenye hasira na wanawake wenzake inamaanisha hapati bakora kabisa au za kumtosha.

Nawashangaa gen Z wapenda mishangazi hamzijuwi hizo dalili.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Unaweza ukaona kama ni jambo dogo lakini kwa jicho la tatu hili ni jambo kubwa sana linalopaswa kudhibitiwa kwa uharaka juu ya Mtu au watu au kikundi cha watu kinachoweza kuwa kinavujisha siri na taarifa za siri ambazo hazijawa rasmi na kutolewa kwa Umma.

Nasema hivi kwa kuwa wiki moja iliyopita Maria Sarungi niliona katika mtandao wake wa Twitter maarufu kama X akitoa taarifa kuwa Jumatano hii yaani kesho Rais wetu atatua Nchini Marekani.

Ambapo Maria Sarungi alieleza mambo mengine ambayo mimi binafsi nayachukulia kama uzushi na muendelezo wa tabia yake ya kuendelea kuchafua wale wote alio na hasira nao na chuki binafsi. Kwa kuwa amekuwa akiongea na kuandika vitu pasipo ushahidi wa aina yoyote ile na hata yeye amekuwa akikiri kuwa hana ushahidi.

Sasa Leo taarifa rasmi imetolewa ambapo imeonyesha kuwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi atakuwa Marekani siku ya kesho baada ya kuondoka hii leo.hii ikimaanisha kuwa taarifa iliyotolewa na Maria Sarungi wiki moja iliyopita juu ya safari ya Mheshimiwa Rais kwenda Marekani ilikuwa sahihi japo naamini maneno mengine ni ya uongo,uzushi na uchonganishi pamoja na kutaka kuwapaka watu matope hasa wale ambao ana chuki nao binafsi na kutumika na kutumiwa na watu walio nyuma ya pazia.

Swali langu ni je nani anayevujisha siri na kumpatia Maria Sarungi? Kwa Malengo gani? Kwa maslahi gani kwa Taifa letu?

Huyo mtu anataka nini? Anataka kujenga taswira ipi? Anamtumikia nani na kupokea maelekezo kutoka kwa nani?

Hata hivyo naipongeza sana awamu ya sita kwa namna ilivyodhibiti kwa kiasi kikubwa kudhibiti uvujaji wa siri za ikulu ukilinganisha na awamu iliyopita. Najuwa suala hili litafanyiwa kazi na wahusika na hatimaye kukibaini kirusi na kukiweka pembeni.

Hongereni sana wahusika kwa kazi hiyo ya kudhibiti uvujaji wa taarifa za siri.naamini hata hili mmeshaanza kulifanyia kazi na muhusika au kirusi hicho kitabainika na kunaswa na hatimaye kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria ,miongozo,taratibu na miiko ya kazi yake.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.

PIA SOMA
- Rais Samia kuondoka leo Oktoba 29 kuelekea Marekani kuhudhuria mjadala wa Norman E. Borlaug
Dogo watu wanajua mpaka aina ya ktanda acholalia sembuse ratiba

Biblia inasema hivi " Mungu asipoulinda mji waulindao wafanyabkazi bure"

Acheni viburi tenda haki hamna ulinzi wowote

Mrudisheni uraian Soka afurahie maisha yake vinginevyo yatawakuta ya mwendazake
 
Dogo watu wanajua mpaka aina ya ktanda acholalia sembuse ratiba

Biblia inasema hivi " Mungu asipoulinda mji waulindao wafanyabkazi bure"

Acheni viburi tenda haki hamna ulinzi wowote

Mrudisheni uraian Soka afurahie maisha yake vinginevyo yatawakuta ya mwendazake
Kwani soka yupo wapi huko unaposema arudishwe ? Maana inaonyesha unafahamu aliko.
 
Back
Top Bottom