G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,795
- 36,704
Hatimaye mwandishi wa habari na mwanaharakati huru wa Tanzania Maria Sarungi amethibitisha rasmi leo kupeleka ndani ya ICC nyaraka muhimu za ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi mkuu.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter amesema kuwa "Namshukuru Mungu kuwa hatimaye nimefanikiwa kupeleka nyaraka muhimu ICC zinazohusu ukiukwaji wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi mkuu, nawashukuru pia wote tulioshirikiana"
Miongoni mwa nyaraka hizo zipo video, picha za mauaji, kauli za vitisho kutoka kwa watawala dhidi ya upinzani na video zinazoonesha polisi wakipiga raia.
Mtuhumiwa namba moja kwenye nyaraka hizo ni Rais John Pombe Magufuli. Aidha wapo pia IGP, DC Lengai Ole Sabaya, RC wa Mbeya Albert Chalamila na baadhi ya watendaji wakuu wengine wa serikali ya Tanzania na jeshi la polisi.
Kwenye Mtandao wa Twitter, Maria kaandika hivi:
Thank God! Alhamdulillah! I have used my skills, training and ability as a journalist to fulfill my duty and submitted to @IntlCrimCourt evidence and facts on Crimes against Humanity in #Tanzania - many thanks to everyone Nawashukuru nyote -
Leo nimekamilisha kazi Mungu atulinde!