Nime NOTE mambo mawili makubwa kutokana na speech aliotoa CDF Mabeyo jana.
Kwanza, kitendo cha kutamka kwamba Jeshi kuweka nadharia na tamko la kumtii Rais Samia kama jinsi katiba inavyotaka. Imeashiria kuna watu nyuma ya pazia walianza kushawishi na kusambaza propaganda chini kwa chini kwa jeshi na vyombo vingine kukataa kumtii na kumtambua Rais Samia. Kifupi, kuna struggle of power ilitaka kutokea mara baada ya Rais Magufuli kuugua sana na baada ya kufariki, kupelekea CDF Mabeyo kuingilia kati na kugoma kwenda kinyume na katiba kwa vishawawishi wa waliotaka kufanya mapinduzi.
REF Pia: Tarehe ambazo Rais Magufuli alivyougua sana na ndio usiku wake akafariki, Makamo Wa Rais Samia alipangiwa ziara ya kwenda Tanga ya Siku 7, na alisisitiza sana kwa msisitizo wa juu kabisa kutuomba raia tumuombee dua kwa mungu yeye na msafara wake uende salama na urudi salama alipokua Tanga akihutubia, alionekana ni mtu mwenye hofu na mashaka juu ya usalama wa msafara wake (Rudia kuangalia video zile).
Ziara za viongozi huwa zinapangwa kutoka kwa "Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi Ya Rais - Ambaye Ni Dk Bashiru Ally Kakurwa". Kwa scenario hii, hakuna shaka Dk. Bashiru Ally ndio aliompangia ziara Makamo Wa Rais Samia Suluhu kumpeleka tanga kwa siku 7.
Swali,
1) Unampangia vipi Makamo Wa Rais ziara ya kazi ya kusafiri kwa muda wa Siku 7, wakati ukijua kwamba Rais ana hali isioridhisha na muda wowote lolote linaweza kumtokea?
2) Kwamba muda wowote huyo Makamo Wa Rais unaempeleka ziara ya Siku 7, anaweza kutakiwa kutangaza kifo cha Rais na kushika dola ya uongozi wa nchi?
3) Kwanini Makamo Wa Rais asingefutiwa ziara hizo, kuwekwa sehemu salama na kuongezewa ulinzi wa hali ya juu kwa lolote likitokea kwa Rais anaeumwa?
4) Makamo Wa Rais kupelekwa Tanga kufanya ziara ya Siku 7, mkoa wa tanga ambao ni mdogo na angeweza kuumaliza ziara zake kwa siku moja au mbili tu tena kwa kutumia hata boda boda. Siku 7 zote hizo za nini? Kipi au miradi gani ambayo ipo tanga ingemchukua siku 7 kumaliza kuzifanyia ziara hizo???. Haiingii akilini kabisa.
Jambo la pili,
Lack Of Proffessionalism, hakukua na haja yoyote ya yeye CDF kutangaza mbele ya umma na dunia kwamba kuna siri amepewa yeye na Rais Magufuli, angekaa kimya na kufanya appointment ya kwenda kuonana nae Rais Samia private katika Ofisi Ya Rais Ikulu.
Kitendo cha yeye kutangaza mbele ya umma kwamba amepewa siri na Rais Magufuli ni hatari hata kwake yeye CDF dhidi ya maadui wa nje na ndani ya Tanzania. Pia ni kuzua taharuki na sintofahamu isiokua na ulazima wowote kwa raia na wageni waliohudhuria mazishi na hata kwa wale walioshuhudia mazishi katika vyombo vya habari.
"LABDA PENGINE" CDF Mabeyo nimepokea speech yake ndivyo-sivyo kwenye swala la lack of proffessionalism, na pengine ujumbe aliotaka kuufikisha kwa viongozi wa umma (Makatibu na Mawaziri) ni kuonesha hasira zake kwao waliotaka kuforce na kueneza propaganda ili Mama Samia asiapishwe kuwa Rais na kuchelewesha kutangaza msiba wa Rais Magufuli. Hasira alizielekeza kwa wale waliotaka Katiba ivunjwe na mapinduzi yafanyike sambamba na kujichotea mabillioni ya pesa hazina kabla ya kutangazwa kifo cha Rais.
Ila kitendo cha yeye CDF kutamka kwamba JESHI LINAMUUNGA MKONO NA LIPO NYUMA YAKE RAIS ni jambo la msingi sana kwa taifa, tetesi za kwamba jeshi lilitaka kufanya mapinduzi au jeshi lipo njia panda juu ya uongozi wa Rais Samia umetokomezwa na kufutwa kabisa. Na amethibitisha jeshi letu lipo imara na "HALIJA YUMBISHWA NA WASAKA MADARAKA KWA NGUVU (WAZEE WA PROPAGANDA)", pia ni ONYO KWA YOYOTE ATAKAETAKA KUFANYA UJINGA UJINGA ili kumkwamisha Rais aliepo kikatiba.
UJUMBE KWA RAIS SAMIA SUKUHU HASSAN - CDF Mabeyo ni tunu kwa taifa, na ni zawadi kwa utawala wako mama, shirikiana nae mguu kwa mguu kuisafisha serikali na viongozi wa umma wote waliotaka kucheza michezo michafu tokea kipindi Rais Magufuli, anaumwa na mpaka alipofariki.
Hata kama kuna wana CCM wenye vyeo vya juu wamehusika kumwaga sumu ilikufanya mapinduzi washughulikie mapema (Nina Amini kuna Mawaziri/Naibu Waziri/Makatibu Wakuu wamefurahishwa sana na kifo cha Rais Magufuli kufariki, wakiamini aliekuwa anawabana sasa hayupo - VUNJA BARAZA LOTE LA MAWAZIRI).
Wangesababisha machafuko makubwa sana kama wangefanikiwa ushenzi waliotaka kuufanya - Tumesikia, wapo waliojichotea Mabillioni kule hazina kwa kigezo cha kununua vifaa vya kumtibu Rais Magufuli. Wengine hela zile baada ya kuchukua wamegawa kwa wajumbe kumpitisha mtu wao kuwa Makamo Wa Rais. Pita nao woteeeeee!!! Raia na Jeshi lipo nyuma yako Mama!!!