Maria Sarungi: Watanzania msiwe wanafiki, mteteeni Tundu Lissu anayewapigania

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Mwanaharakati Maria Sarungi Tsehai amewalipua Watanzania kwa kile alichokiita ni kushindwa kumtetea Tundu Lissu, kiongozi ambaye amejitoa mhanga kwa miongo kadhaa kusema ukweli bila woga. Maria Sarungi amesisitiza kuwa Tundu Lissu ana rekodi ya kipekee ya utendaji isiyoyumba, na ndiyo sababu viongozi wa kimataifa wanamfuatilia kwa ukaribu.

Amesema ni aibu kwa taifa kuwa na kiongozi mwenye akili na ujasiri kama Lissu, lakini wananchi wanashindwa kusimama kidete kudai uhuru wake.

Maria Sarungi amebainisha kuwa Tundu Lissu amepimwa na majaribu mengi, ikiwemo shambulio la risasi, lakini hajawahi kubadilisha msimamo wake wa kuipigania haki. Alisimulia kwa masikitiko namna rafiki yake mmoja raia wa Kenya alivyomhoji kwanini Watanzania wanashindwa kumlinda kiongozi wao imara, swali ambalo amesema linapaswa kumfanya kila mwananchi atafakari. Kwa mujibu wa Maria Sarungi, kumpenda Lissu kwa maneno hakusaidii, bali ni lazima wananchi wasimame na kudai haki yake sasa.

Mwanaharakati huyo amehitimisha kwa kusema kuwa CHADEMA ina Mwenyekiti halali ambaye kwa sasa anasota gerezani, jambo ambalo linazuia taifa kupata uongozi imara unaohitajika. Maria Sarungi amesisitiza kuwa suala la Tundu Lissu si la CHADEMA peke yake, bali ni mtihani kwa kila Mtanzania.

Amesema kuwa taifa haliwezi kutoka lilipo ikiwa watu wenye uwezo wa kuongoza kama Lissu wataendelea kufungwa kwa sababu tu ya msimamo wao wa kusema ukweli.

Lissu Akitoka afanye mambo yake,asipoteze muda kuwatetea mazuzu wa Simba na yanga....acha CCM iwaenyeshe hadi maji waite mma.
 
Mwambie aje na yeye, Tumpambanie TAL woote, Matrako yake.

Ukombozi hauji kwa siku moja, Ndo maana hata Nelson Mandela alikaa miaka 27 gerezani kabla ya kuja kua Rais, Fuatilia Historia ya Hechilema jinsi alivopambana mpaka kupata ukombozi wa Zambia..

Watanzania Wengi wako na CHADEMA na TAL, Ngoja vidonda vya mo29 Vipungue utaona joto litakavo panda.
 
Anawaoigania nyie ambao mnatafuta madaraka.

Sijawahi msikia akimpigania mkulima.
 
Mwambie aje na yeye, Tumpambanie TAL woote, Matrako yake.

Ukombozi hauji kwa siku moja, Ndo maana hata Nelson Mandela alikaa miaka 27 gerezani kabla ya kuja kua Rais, Fuatilia Historia ya Hechilema jinsi alivopambana mpaka kupata ukombozi wa Zambia..

Watanzania Wengi wako na CHADEMA na TAL, Ngoja vidonda vya mo29 Vipungue utaona joto litakavo panda.
Naona kwanza tutangulie mimi na wewe kisha yeye aje baadae, tusikae kumsubiri mtu aliye mbali mpaka afike wakati mimi na wewe tunaweza kuanza.
 
Chadema ndio iliyofanya kuwa suala la Lissu ni lao peke yao. Hauwezi kuwaita wote unaotofautiana nao vibraka, wasaliti, walamba asali n.k. halafu ukategemea watasimama na wewe ukipata matatizo. Badala ya kuwaita watanzania wanafik wawakaribishe kwa dhati kuungana nao katika vita wanayopigana. Ukweli ni kuwa Chadema haiwezi kushinda mpambano huu bila kushirikiana na wasio wanachama wa Chadema. Na hawatashinda kwa kutegemea mitandao peke yake.

Amandla...
 
Mwanaharakati Maria Sarungi Tsehai amewalipua Watanzania kwa kile alichokiita ni kushindwa kumtetea Tundu Lissu, kiongozi ambaye amejitoa mhanga kwa miongo kadhaa kusema ukweli bila woga. Maria Sarungi amesisitiza kuwa Tundu Lissu ana rekodi ya kipekee ya utendaji isiyoyumba, na ndiyo sababu viongozi wa kimataifa wanamfuatilia kwa ukaribu.

Amesema ni aibu kwa taifa kuwa na kiongozi mwenye akili na ujasiri kama Lissu, lakini wananchi wanashindwa kusimama kidete kudai uhuru wake.

Maria Sarungi amebainisha kuwa Tundu Lissu amepimwa na majaribu mengi, ikiwemo shambulio la risasi, lakini hajawahi kubadilisha msimamo wake wa kuipigania haki. Alisimulia kwa masikitiko namna rafiki yake mmoja raia wa Kenya alivyomhoji kwanini Watanzania wanashindwa kumlinda kiongozi wao imara, swali ambalo amesema linapaswa kumfanya kila mwananchi atafakari. Kwa mujibu wa Maria Sarungi, kumpenda Lissu kwa maneno hakusaidii, bali ni lazima wananchi wasimame na kudai haki yake sasa.

Mwanaharakati huyo amehitimisha kwa kusema kuwa CHADEMA ina Mwenyekiti halali ambaye kwa sasa anasota gerezani, jambo ambalo linazuia taifa kupata uongozi imara unaohitajika. Maria Sarungi amesisitiza kuwa suala la Tundu Lissu si la CHADEMA peke yake, bali ni mtihani kwa kila Mtanzania.

Amesema kuwa taifa haliwezi kutoka lilipo ikiwa watu wenye uwezo wa kuongoza kama Lissu wataendelea kufungwa kwa sababu tu ya msimamo wao wa kusema ukweli.

Lissu ana rekodi ya kamdomo sio utendaji!! Lissu ni mfitini na mzandiki aliyejawa na chuki na upumbavu uliopitiliza kiasi cha kushindwa kuudhibiti mdomo wake.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mgawanyo wa kisiasa baina ya watanzania ndio chanzo cha nguvu za ccm
 
Huyu mala*** akikosa kufikishwa kunako tu na mumewe basi lazima hasira zake azielekeze kwa Samia.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Back
Top Bottom