Mariam Ditopile amlipua Lema, amtaka ajitokeze kuomba radhi

Mariam Ditopile amlipua Lema, amtaka ajitokeze kuomba radhi

VICOBA = Village Community Bank.

Ndivyo ilivyo??
Ndiyo maana yake hiyo.Hebu mueleze huyo m-viti maalumu jinsi akina mama masikini wa huko Kitanzini,Ipogolo,Kitwiru,Malolo,Mlandege,Mtwivila,Nduli(Iringa)Hadi Kibaigwa,Nkuhungu,Msalato,Aghondi na Manyoni yote wanavyoteswa na mikopo ya hovyohovyo.Halafu,wengi wameolewa na waendesha bodaboda.Yeye hajui chochote.Amekuzwa kwa mapesa "mwolofu" ya serikali kupitia baba yake Ukiwaona Ditopile Mzuzuri.Amekaa anadanganya akina mama masikini na vijana.
 
Vicoba ni Ponzi scheme inayotumiwa na CCM.
Watu wamekataa uongo wa CCM.Sasa,wamebaki wanalia na kauli za Lema.Siku hizi wanazichambua kauli za Lema kuliko kufuatilia malezi ya familia wakijidai wanazitolea majibu.Njoo kwenye majibu yao ndiyo utajua ni watu au wanasesere!
 
DITOPILE AMLIPUA LEMA
AMTAKA AJITOKEZE KUOMBA RADHI

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile amemtaka aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ajitokeze aombe radhi kutokana na kauli yake aliyoitoa kuhusu Vicoba ambayo ni yakuwadhihaki wanawake.

Katiba hotuba yake Lema alikaririwa akisema Vicoba ni umasiki na ndio maana alimwondoa mkewe kwenye benki hizo.

Ditopile ametoa wito huo alipo kuwa mgeni rasmi katika kongamoano la Vicoba na kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani liloandaliwa na Shirika la Msaada wa Kisheria (JUST).

“Kama kweli tunataka kurekebisha pale ambapo serikali imekosea basi tuwe na lugha nzuri,kama kuna mtu anaona vikoba havifai basi aje na hoja zake sio kudharau kwasababu wapo wanawake wengi wanaendesha shughuli zao kupitia fedha hizo kidogo"

Amesema “Ndugu yangu huyu Godbless Lema kiukweli ametumia lugha ambayo imetudhihaki sisi wanawake na inawezekana hata mama yake alikuwa ni miongoni na kama anahoja aishauri serikali"

"Mimi namuomba ashuke chini akafuatilie vikoba hivi ni kwa namna gani vimeinua maisha ya watanzania ajifunze na kama anaona kuna sehemu ya kujirekebisha aseme, ikiwezekana atoke na afute kauli yake kwasababu ametukosea sana, asitumie uhuru vibaya aliopewa na Rais Dkt. Samia"

Ditopile amesisitiza kuwa uanzishwaji wa huduma ndogo za fedha upo kwa mujibu wa sheria ambayo ilitungwa wakati Godbless Lema akiwa Mbunge.

Alisema wizara ya fedha ilitunga sheria ya huduma ndogo za fedha mwaka 2017 lengo ni kuhakikisha huduma hiyo inaleta tija kwa wananchi.

View attachment 2550130View attachment 2550131View attachment 2550132View attachment 2550133View attachment 2550134View attachment 2550135
View attachment 2550136
Mbungee wangu ditopile. Nakupongeza saana Kwa kuliona hilii
 
Waanze wao familia nzima kuomba Msamaha kwa baba yake kumpiga risasi dereva bajaji amabaye hakuwa na hatia pale Kawe. Hata kama alikuwa nayo haikuwa sahihi kumpiga risasi hadi kufa wakati sheria iko wazi.
Hivi Alikua Dereva Bajaj au Daladala?
 
Huyu ni mtoto wa JK kisiasa. No JK No Miss Ditopile na JK hataishi milele. Anza kujijenga now kuliko kudhani kama JK atakuwepo milele na issue ya Lema haitakusaidia kuibuka mshindi Dodoma 2025
Jk na marehemu ditopile ni Kama juma nature na kr,Wana kitambo
 
Waanze wao familia nzima kuomba Msamaha kwa baba yake kumpiga risasi dereva bajaji amabaye hakuwa na hatia pale Kawe. Hata kama alikuwa nayo haikuwa sahihi kumpiga risasi hadi kufa wakati sheria iko wazi.
Kwa hiyo point zenu wavuta bangi wa Chadema ni kumhusisha yeye na makosa ya baba yake?

Je!
Ni nani aujuaye usafi wa wazazi wenu enyi manyumbu wa ufipa?

Mkipewa maswali yanayohitaji weledi mnakimbilia kujitoa akili !
 
Kwa wasiomjua huyu maria ditopile, ni mtoto wa kada mkubwa wa CCM, aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Dar, Ukiwaona Ditopile Mzuzuri, kwa sasa ni marehemu, akiwa mkuu wa mkoa mstaafu, daradara lilimchomekea akashuka akampiga dereva risasi ya kichwa akafa hapo hapo na yeye alikuja kufia gest akiwa na mchepuko,
Huyu maria, hajuhi shida, hajasomeshwa na vicoba, vicoba ni katika hari ya kutapatapa tu maisha.
Village Community Banks imekuwepo mda mrefu, hamssisemea eti sasa hivi lema anatafuta kiki za kisiasa ndo mnanyanyua midomo! Lema alishachuja.
 
Kwa hiyo point zenu wavuta bangi wa Chadema ni kumhusisha yeye na makosa ya baba yake?

Je!
Ni nani aujuaye usafi wa wazazi wenu enyi manyumbu wa ufipa?

Mkipewa maswali yanayohitaji weledi mnakimbilia kujitoa akili !
woote wawe na weledi hata wewe pia? una swali gani la weledi ulijualo wewe zaidi ya kuimba mapambio ya kusifu na kuabudu wafu? unaabudu watu badala ya mfumo? chama chako chenyewe hukipendi ila unapenda watu.
mungu aliamua ugonvi na wema huwa hawafi. jadili
 
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dodoma Mhe Mariam Ditopile amemtaka aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema ajitokeze aombe radhi kutokana na kauli yake aliyoitoa kuhusu Vicoba ambayo ni yakuwadhihaki wanawake.

Katiba hotuba yake Lema alikaririwa akisema Vicoba ni umasiki na ndio maana alimwondoa mkewe kwenye benki hizo.

Ditopile ametoa wito huo alipo kuwa mgeni rasmi katika kongamoano la Vicoba na kumpongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili madarakani liloandaliwa na Shirika la Msaada wa Kisheria (JUST).

“Kama kweli tunataka kurekebisha pale ambapo serikali imekosea basi tuwe na lugha nzuri,kama kuna mtu anaona vikoba havifai basi aje na hoja zake sio kudharau kwasababu wapo wanawake wengi wanaendesha shughuli zao kupitia fedha hizo kidogo."

Amesema “Ndugu yangu huyu Godbless Lema kiukweli ametumia lugha ambayo imetudhihaki sisi wanawake na inawezekana hata mama yake alikuwa ni miongoni na kama anahoja aishauri serikali."

"Mimi namuomba ashuke chini akafuatilie vikoba hivi ni kwa namna gani vimeinua maisha ya watanzania ajifunze na kama anaona kuna sehemu ya kujirekebisha aseme, ikiwezekana atoke na afute kauli yake kwasababu ametukosea sana, asitumie uhuru vibaya aliopewa na Rais Dkt. Samia."

Ditopile amesisitiza kuwa uanzishwaji wa huduma ndogo za fedha upo kwa mujibu wa sheria ambayo ilitungwa wakati Godbless Lema akiwa Mbunge.

Alisema wizara ya fedha ilitunga sheria ya huduma ndogo za fedha mwaka 2017 lengo ni kuhakikisha huduma hiyo inaleta tija kwa wananchi.

View attachment 2550130View attachment 2550131View attachment 2550132View attachment 2550133View attachment 2550134View attachment 2550135
View attachment 2550136

Yeye ndio aanze kuomba msamaha kwa familia ya Marehemu. Mjinga kweli.
 
Anaye jua mchango wake wa maana bungeni ani tag.
Sasa anasubiri kikao kirefu cha bajeti na tshs 350000- kila siku🙄
 
Ulipomuita Mh. Ditopile moto wa muuaji positivity energy ilikuwa inakuimarisha Ili nikupe hongera! Pumbavu!!!
Niliyemuita mtoto wa muuaji ni mimi, hate inakusababishia kuchanganyikiwa na ni ukweli kwamba huyo demu ni mtoto wa muuaji tena aliyeua hadharani kwa kiburi alichonacho.
 
Kwa hiyo point zenu wavuta bangi wa Chadema ni kumhusisha yeye na makosa ya baba yake?

Je!
Ni nani aujuaye usafi wa wazazi wenu enyi manyumbu wa ufipa?

Mkipewa maswali yanayohitaji weledi mnakimbilia kujitoa akili !
Mtoto wa nyoka ni nyoka.
-Nimenukuu msemo wa wahenga.
 
Back
Top Bottom