Mariamu Ditopile anatumwa na nani?

Mariamu Ditopile anatumwa na nani?

Sio vibaya ukisema toka achaguliwe, ameifanyia nini Kondoa?.
P
Mkuu unajua wewe ni wakili na legend tunaye kutegemea kwenye nondo za hoja humu ndani. Nashangaa unaendeleza upotoshaji wa majukumu ya mbunge? Common on Paskal unamuonea mbunge wa watu!
 
Unajaribu kuomba huruma mitandaoni?

Unajaribu kuonyesha woga wako uchaguzi ujao 2025?

Unajaribu kuficha uwezo wako mdogo wa kutatua kero za wananchi wa Jimbo lako kwa kumchafua ambaye anajiimarisha kugombea uchaguzi ujao?

Hoja dhaifu sana umeianzisha kabla ya uchaguzi. Ushauri kwako Katibu wa mbunge wa huko kwenu; ikiwa mnao ushahidi wa hayo matumizi binafsi ya mtu kua anahonga/takirima, fikeni TAKUKURU mshitaki na kwa Mwenyekiti wa chama chenu wilaya na mkoa.
Pia wakati mmeshitaki nanyi anzisheni mbinu za kujiwinda na uchaguzi ujao kwa kuwasaidia wahitaji hapo jimboni kwenu.
Akashitaki Takukuru ipi, hii hii ya Wala rushwa? Utashangaa akienda kushitaki Takukuru wanahitaji rushwa ili wachunguze, kisha wanaenda kuvuta rushwa kwa anayetuhumiwa. Hakuna taasisi ya kipuuzi kama hiyo takukuru.
 
Sote tunajua kuwa Mhe.Mariamu Ditopile ni Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Dodoma.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni nguvu kubwa anayotumia kusaka ubunge Jimbo la Kondoa Mjini,kwa kweli anacheza rafu mbaya sana

Kuna maswali mengi ya kujiuliza kwani anatumia pesa nyingi Sana kutoa misaada kwenye makundi mbalimbali Huku akitumia sehemu ya pesa hizo kuwakamata vilivyo viongozi wa CCM wa Kata nane za Kondoa mjini na wale wa wilayani.

kila anapotoa misaada hiyo ni lazime amtaje Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania as if ndiye anayemtuma.

Hili Jambo limefanya watu makini wajiulize maswali mengi bila majibu kwani vyombo vinavyopambana na rushwa na utawala Bora kama vile Takukuru havijawahi hata siku moja kumkamata au hata kumwita kwa mahojiano.

kwa kifupi ndani ya CCM kwa nchi nzima huyu ndiye kinara wa wasaka ubunge hasa ukitathmini nguvu ya pesa anayotumia.

Hii imemfanya Mbunge dhaifu wa Jimbo Hilo Ndugu Ally Makoa aonekane bwege.
Tutaendelea kutoa taarifa za Mhe huyu kila mara kwani mambo anayofanya ni ya ajabu yanayopaswa kukemewa na wanamaendeleo na watu waadilifu wa Taifa hili.

Hatupaswi kuendelea kuwaacha watu wachafu wa sampuli hii waendelee kunajisi taifa.huko ni kukosa uzalendo
Kutoa Msaada hadharani inakuaje Rushwa? Wewe kama umekalia.kuti kavu pisha watu usituchoshe.

Kama yeye anamtaja Samia na wewe mtaje Lisu au Kassim 😁😁
 
Akashitaki Takukuru ipi, hii hii ya Wala rushwa? Utashangaa akienda kushitaki Takukuru wanahitaji rushwa ili wachunguze, kisha wanaenda kuvuta rushwa kwa anayetuhumiwa. Hakuna taasisi ya kipuuzi kama hiyo takukuru.
🙄🤔
 
Namuonea kivipi?, ila kiukweli wabunge wa Dodoma ni majanga, angalia huyu Kwa wale mliowahi kufika Kongwa, ni jimbo choka mbaya kiasi kwamba Mbunge wake hafai kwa lolote!

P
NO nooo Paskal usipotoshe majukumu ya mbunge, hivi ungechaguliwa ubunge Kawe ungeleta maendeleo kwa fedha yako? Tuambie tujue leo, au ulidhamiria kuwaongopea wana kawe!

Mkuu tumia elimu, uzoefu na nafasi yako kuelimisha jamii. Usiendeleze upotoshaji!

Unafahamu vizuri kuwa sio jukumu la mbunge kutatua kero za jimbo lake au kuleta maendeleo kwa sababu hana fungu la bajeti la kufanya hayo!

Ila unafanya makusudi!
 
View: https://youtu.be/Qr6j25jFGyI?feature=shared
P
 
Akashitaki Takukuru ipi, hii hii ya Wala rushwa? Utashangaa akienda kushitaki Takukuru wanahitaji rushwa ili wachunguze, kisha wanaenda kuvuta rushwa kwa anayetuhumiwa. Hakuna taasisi ya kipuuzi kama hiyo takukuru.
Yalinikuta.sina hamu na hao mashetani
 
Pole sana mkuu!
Mkuu unaenda kupeleka mashitaka unapeleka na ushahidi.unaambiwa kwahiyo tunafanyaje?
Hii ndio Tz unaenda kushitaki kuombwa rushwa na mamlaka inakuomba rushwa.
 
Watajuana wenyewe huko

Ova
Ally lazima apigwe chini. Wakondoa hawajaona alichokifanya walakumsikia akiongea chochote.
Kumbe Tao yaani mbunge wa Sasa hata jf ulikua hujajiunga, mpaka ukipoona kitumbua kinaingia mchanga.
Pole Sana mbunge wa Sasa.
Ukiona vipi kamhonge mkuu wa mkoa Kama unaona mwenzio anahonga madiwani.
Kifupi. UMEUMIA
 
Mkiletewa zawadi na mbunge ama mwanasiasa yeyote wewe kula, suala la kupiga kura, utakuwa mwenyewe kwenye kichumba cha kupigia kura, kwa uhuru wako huku ukilindwa hakuna wa kukulazimisha umpigie. Utamchagua umpendaye kwa kadri uoendavyo bila kujali chama au asili yake. Umchekea nje, ndani unamlima. Utu wa mtu haununuliwi.
 
Sote tunajua kuwa Mhe.Mariamu Ditopile ni Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Dodoma.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni nguvu kubwa anayotumia kusaka ubunge Jimbo la Kondoa Mjini,kwa kweli anacheza rafu mbaya sana

Kuna maswali mengi ya kujiuliza kwani anatumia pesa nyingi Sana kutoa misaada kwenye makundi mbalimbali Huku akitumia sehemu ya pesa hizo kuwakamata vilivyo viongozi wa CCM wa Kata nane za Kondoa mjini na wale wa wilayani.

kila anapotoa misaada hiyo ni lazime amtaje Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania as if ndiye anayemtuma.

Hili Jambo limefanya watu makini wajiulize maswali mengi bila majibu kwani vyombo vinavyopambana na rushwa na utawala Bora kama vile Takukuru havijawahi hata siku moja kumkamata au hata kumwita kwa mahojiano.

kwa kifupi ndani ya CCM kwa nchi nzima huyu ndiye kinara wa wasaka ubunge hasa ukitathmini nguvu ya pesa anayotumia.

Hii imemfanya Mbunge dhaifu wa Jimbo Hilo Ndugu Ally Makoa aonekane bwege.
Tutaendelea kutoa taarifa za Mhe huyu kila mara kwani mambo anayofanya ni ya ajabu yanayopaswa kukemewa na wanamaendeleo na watu waadilifu wa Taifa hili.

Hatupaswi kuendelea kuwaacha watu wachafu wa sampuli hii waendelee kunajisi taifa.huko ni kukosa uzalendo
Yeye kama anaweza hata kuzunguka Tanzania nzima azunguke tu kutoa hiyo misaada.
 
Back
Top Bottom