Mariamu Ditopile anatumwa na nani?

Mariamu Ditopile anatumwa na nani?

Sote tunajua kuwa Mhe.Mariamu Ditopile ni Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Dodoma.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu ni nguvu kubwa anayotumia kusaka ubunge Jimbo la Kondoa Mjini,kwa kweli anacheza rafu mbaya sana

Kuna maswali mengi ya kujiuliza kwani anatumia pesa nyingi Sana kutoa misaada kwenye makundi mbalimbali Huku akitumia sehemu ya pesa hizo kuwakamata vilivyo viongozi wa CCM wa Kata nane za Kondoa mjini na wale wa wilayani.

kila anapotoa misaada hiyo ni lazime amtaje Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania as if ndiye anayemtuma.

Hili Jambo limefanya watu makini wajiulize maswali mengi bila majibu kwani vyombo vinavyopambana na rushwa na utawala Bora kama vile Takukuru havijawahi hata siku moja kumkamata au hata kumwita kwa mahojiano.

kwa kifupi ndani ya CCM kwa nchi nzima huyu ndiye kinara wa wasaka ubunge hasa ukitathmini nguvu ya pesa anayotumia.

Hii imemfanya Mbunge dhaifu wa Jimbo Hilo Ndugu Ally Makoa aonekane bwege.
Tutaendelea kutoa taarifa za Mhe huyu kila mara kwani mambo anayofanya ni ya ajabu yanayopaswa kukemewa na wanamaendeleo na watu waadilifu wa Taifa hili.

Hatupaswi kuendelea kuwaacha watu wachafu wa sampuli hii waendelee kunajisi taifa.huko ni kukosa uzalendo
Hakuna kosa hapo as long wote ni wana CCM, na anachofanya ni takrima kwa wanachama wenzake.
 
Kwenye itifaki as umesema ni mbunge, lazma amtaje boss wake.
Mbili aweze kumwaga steve nyerere hela sikukuu ya xmas. Ashindwe huyo anayetaka ubunge. Vitu gani hivo unauliza yakheee. Lazma hilo jimbo alipambanie maana umesema analitaka. Why asilipe upendeleo wakati huu ana nguvu.
 
Bongo hakuna tofauti kati ya msomi na ambaye Hana elimu kabisa. Majukumu ya mbunge unaweza kuuliza kalifanyia Nini Jimbo lake? Mbunge ni mkurugenzi wa maendeleo?
Maendeleo yanaletwa na nani??
 
Mkiletewa zawadi na mbunge ama mwanasiasa yeyote wewe kula, suala la kupiga kura, utakuwa mwenyewe kwenye kichumba cha kupigia kura, kwa uhuru wako huku ukilindwa hakuna wa kukulazimisha umpigie. Utamchagua umpendaye kwa kadri uoendavyo bila kujali chama au asili yake. Umchekea nje, ndani unamlima. Utu wa mtu haununuliwi.
👍👏🙏
 
Huenda ametumwa na chama! Ally Makoa aanze kujiuliza tangu awe mbunge ameleta maendeleo gani jimboni?
 
Back
Top Bottom