Mariamu Sagini awaasa vijana wa kike kutengeneza nafasi za Uongozi

Mariamu Sagini awaasa vijana wa kike kutengeneza nafasi za Uongozi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mjumbe wa Baraza Kuu UWT Taifa, Mariam Sagini amewataka vijana hasa wa kike kutengeneza historia nzuri maishani kwa kujaza nafasi za mbalimbali za uongozi hasa kadri zinavyojitokeza.

Akizungumza na vijana kwenye Hafla ya Ufungaji wa Kambi la Umoja wa Vijana mkoani Katavi iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wanawake ya Mpanda, Mariam amesema kuwa Jumuiya ya UWT ipo kazini chini ha Mwenyekiti Merry Chatanda kuhakikisha inamsaidia mtoto wa kike katika nafasi mbalimbali za uongozi.

"Wanawake mkajaze nafasi kama sisi mama zenu tupo kazini vijana mnashindwaje?, usiende kusomwa kijana ambaye siku ukifa unaenda kusumbua padri, mchungaji au Sheikh yaani wanasoma historia ya marehemu kwamba Marehemu alizaliwa Akafa. Tengeneza historia ambayo ulikuwa nani? labda Katibu, Hamasa au Mwenyekiti hata wasikilizaji wanalia na kukuombea.

Ndivyo tulivyo andaliwa sisi na sisi tunawaandaa hivyo na tunategemea na nyie mtaandaa wadogo zeu kwa ajili ya Chama Cha Mapinduzi," amesema Mbaraza Mariam.
 
Mke wa Naibu Waziri?.

Kama ni Yes, mama ana Roho mbaya huyo ,Watoto alomkuta nao Naibu Waziri wa Mama wengine, Wanaishi Maisha ya kichokoraaa.
 
Ndio wanajiuza Sasa halafu wanakamatwa! Askari anaulizwa maana ya ukahaba au umalaya anasema hajui! Nchi ya vilaza hii!
 
Back
Top Bottom