Mark Zuckerberg: Apple hawajabuni kitu chochote kwa miaka zaidi ya 20 toka Steve Jobs avumbue Iphone, wamebaki kukamua wateja

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Boss wa Meta na mmiliki wa Facebook, Instagram, Thread na WhatsApp bwana Mark Zuckerberg amesema kampuni ya Apple haina ubunifu wowote kwa zaidi ya miaka 20 baada ya Steve Jobs kuvumbua Iphone.

Anasema sasa hata mauzo ya Iphone yanashuka sana na kufidia hasara ya kushuka mauzo ya Iphone, Apple wamejikita kwenye kukamua wateja wanaotumia huduma zao kwa mfano kukata kodi ya 30% kwa developers.

Mark anasema Apple walivumbua iPod, kitu kizuri sana ila wakakosea kuinyima Ipod uhuru wa kuunganishwa kwenye vitu vingine nje ya apple ecosystems.

Msikilize mwenyewe hapa.

View: https://x.com/tsarnick/status/1877856200349331521?s=19
 
Ni katika kukumbushana tu, kipindi apple inafanya ubunifu huo(20yrs ago) ndicho kipindi mbowe alikua anaanza uenyekiti
 
Ni mawazo yake, kuwa bilionea haimaanishi kama ushauri wake una maana sana au ana akili nyingi, Mark alibahatika tu kutengeneza website flani nzuri kwa lugha ya html na php ndipo ikawa facebook ... lakini tayari social media kama myspace zilikuwepo...

Meta ni mtoto mdogo kwa Apple...
 
Kama umefuatilia vizuri utagundua hujajibu hoja za mauzo ya iphone kushuka na kuwakata asilimia 30 developers ila umeishia kumshambulia yeye binafsi na bidhaa zake bila kujibu hoja.
 
Mkuu katika biashara kuna kupanda na kushuka.. Suala la mauzo kushuka kila kampuni inapitia...
Huwezi washambulia Apple kisa kushuka kimauzo.. Bidhaa za Apple always zitaendelea kuwa bora.

Yeye anazungumziaje kuwaiga tiktok kwa kuleta instagram reels ambayo ilikuwa ni feature ya tiktok? walishindwa kuvumbua kipya hadi kuwaiga tiktok?
 
Back
Top Bottom