Mark Zuckerberg: Apple hawajabuni kitu chochote kwa miaka zaidi ya 20 toka Steve Jobs avumbue Iphone, wamebaki kukamua wateja

Mark Zuckerberg: Apple hawajabuni kitu chochote kwa miaka zaidi ya 20 toka Steve Jobs avumbue Iphone, wamebaki kukamua wateja

Boss wa Meta na mmiliki wa Facebook, Instagram, Thread na WhatsApp bwana Mark Zuckerberg amesema kampuni ya Apple haina ubunifu wowote kwa zaidi ya miaka 20 baada ya Steve Jobs kuvumbua Iphone.

Anasema sasa hata mauzo ya Iphone yanashuka sana na kufidia hasara ya kushuka mauzo ya Iphone, Apple wamejikita kwenye kukamua wateja wanaotumia huduma zao kwa mfano kukata kodi ya 30% kwa developers.

Mark anasema Apple walivumbua iPod, kitu kizuri sana ila wakakosea kuinyima Ipod uhuru wa kuunganishwa kwenye vitu vingine nje ya apple ecosystems.

Msikilize mwenyewe hapa.

View: https://x.com/tsarnick/status/1877856200349331521?s=19

Niliwahi kusema kitu kama hiki hapa.

Ila labda sasa kasema Zuck mtasikia.
 
Ni mawazo yake, kuwa bilionea haimaanishi kama ushauri wake una maana sana au ana akili nyingi, Mark alibahatika tu kutengeneza website flani nzuri kwa lugha ya html na php ndipo ikawa facebook ... lakini tayari social media kama myspace zilikuwepo...

Meta ni mtoto mdogo kwa Apple...
tusisahau yupo kwenye PR campaign kubwa sana hivi sasa

ndo maana anaongea ongea kwenye mapodcast
 
Ni katika kukumbushana tu, kipindi apple inafanya ubunifu huo(20yrs ago) ndicho kipindi mbowe alikua anaanza uenyekiti
Ila watu😂.

Miaka 20 ni mingi sana. Kama miaka yote 20 hujafanya kitu hakuna kitu kingine utaweza kufanya.

Apple a.k.a Mbowe waachie wengine kina Sumsung a.k.a Lisu na wengine
 
tusisahau yupo kwenye PR campaign kubwa sana hivi sasa

ndo maana anaongea ongea kwenye mapodcast
Kujaribu ku clear jina lake na kampuni zake baada ya kutuhumiwa kuzuia mijadala mbalimbali kwenye platforms zake.

Trump aliwahi kumuita public enemy number 1 mwaka jana.

Sasa hivi Mark anamuangushia ziko la lawama Biden.
 
yeye kafanya innovation gani?

metaverse?😆 zile VR headsets?😆

labda zile open source AI models zake kidogo

tech imekuwa matured sana hakuna mabadiliko makubwa yanayoshtukiza
 
Hio haifikii hata Apple Vision Pro..
Trust ya Western campany itaendelea kushuka maana wameioneka ni watu wa kufanya lolote kwa ajili ya israel eastern asia wameshaanza kuachana na product za usa baada ya ile issue walk talk za lebanon na pager kulipuka ... amna mtu kiongozi wa maana atakayetumia tech za western .. maana kampuni ipo tiari kutoa taarifa kwa majasusi ili kuilindi israel bila kiujua madhara yake
 
Kwani Facebook wamebuni / walibuni nini ?
Facebook ilikuwa ni website ya kienyeji ametengeneza dogo wa college, baadae akapata wawezeshaji ambao wakaajiri computer scientists na professional programmers ili kuboresha facebook.

Baada ya kufungua soko la hisa na wawekezaji kuingia, ndipo dogo kama founder akawa billionare...
 
Na Iphone wanakuja na camera za Samsung, patamu hapo
Siku hizi ni macamera tu hakuna jambo jipya ambalo ni exciting.
Ila wamefanikiwa kwa upande hasa wa computer kwa kuitupilia mbali intel wakaja na inhouse processors ambazo ni arm based ambazo zinafanya computer ziwe more powerful na kukaa na charge kqa muda mrefu pasipo kupata joto.
Kwa upande mwingine japo kasema ukweli, ana hasira nao maana wanapiga app zake za instagram na facebook spana zisiweze kumfuatilia mtumiaji anapohama kwenye hizo apps ili zisiweze kumletea ads ambazo zinaendana naye hivyo kuifanya meta kupoteza revenue.
 
Ni mawazo yake, kuwa bilionea haimaanishi kama ushauri wake una maana sana au ana akili nyingi, Mark alibahatika tu kutengeneza website flani nzuri kwa lugha ya html na php ndipo ikawa facebook ... lakini tayari social media kama myspace zilikuwepo...

Meta ni mtoto mdogo kwa Apple...
Na meta wamefanya vitu kibao sana.
Anachoasema kuhusu apple ni kweli na watu walidhani labda vision pro itabadili upepo ila nayo imefail sokoni.
Lakini kitu kingine ambacho apple wamefanya miaka ya hivi karibuni ni kuitupa intel na kuanza kutumia inhouse processors ambazo ni arm based. Hii move imekuwa game changer kwa sababu imefanya comps kuwa more powerful huku hazichemki na zinatumia umeme kidogo.
Pia mark ana hasira na apple kwa kuzilima apps zake kufuli zisiwezi kumfuatilia user anapotoka kwenye apps zake.
Lakini bado alichosema ni kweli siku hizi upgrades za iphone ni ndogo sana kiasi kwamba hakuna anything exciting.
 
Facebook ilikuwa ni website ya kienyeji ametengeneza dogo wa college, baadae akapata wawezeshaji ambao wakaajiri computer scientists na professional programmers ili kuboresha facebook.

Baada ya kufungua soko la hisa na wawekezaji kuingia, ndipo dogo kama founder akawa billionare...
Kabla ya Facebook kulikuwa na Myspace; Friendster; Second Life na nyingine nying tu; Whats App, Insta zote wamenunua....

Narudia tena Facebook wamebuni nini ? Ingawa this is neither here nor there..., Anyone can have ideas, Implementation is Key...
 
Back
Top Bottom