Primary niliwahi pata zero somo lilikua kiingereza nakumbuka siku ya paper nilikua naumwa afu ndio ilikua paper ya mwisho mwalim alinikomalia nifanye ivyo ivyo nilichojaza humo nadhani ni jina langu tu.
Kiufupi class nilikua kichwa sasa mitihani ikasahishwa watu wakaanza kupokea. Nikiwa nyumbani najiuguza akaja rafiki yangu tokea nje akiniita kwa sauti Heavy Weight nimekuletea mtihani wako.
Haikua kawaida yangu kumiss shule na sikuwai pokelewa mtihani sababu mda wote nilikuepo. Mda huo naitwa tulikua na maza tumekaa barazani ananiuguza hakwenda kazini.
Jamaa akaleta paper imechorwa zero na masikio na macho bi mkubwa alinicheka sana na mimi badala ya kusikitika nikaishia kucheka. Nadhani hata yeye alielewa kwakua sikuwahi pata maksi kama zile shuleni.
Ajabu ule mtihani nikaingia top 5 sababu masomo mengine nilinyoosha
Ila secondary zero ya civics hii ilitoka topic moja tu mwalim alikua anapima kama watu tumepitia pre form one kumbe wengine tulisugua mtaani nikapata zero takatifu
Mtu Mzito HEAVY WEIGHT