Marks ya chini kabisa ambayo ulishawai pata kwenye mtihani ni ngapi

Marks ya chini kabisa ambayo ulishawai pata kwenye mtihani ni ngapi

Sijawahi kufeli mtihani/test/quic toka naanza kusoma. Hata nikisema safari hii sisomi nione itakuwaje. Nikipiga napata above average kama sio zote.

Nikaja kugundua kuwa nakuwaga sana makini kwenye vipindi na sikosagi kipindi kabisa ndio maana. Nakusoma soma vitabu vitabu hovyo hovyo bila mpangilio pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
test yang ya kwanza physics advance nligonga saba dadeki hio ndio siku ambayo nlianza kuishi kama bundi

I can imagine ulivokuwa unaucheki baada ya kurudishiwa, kama huamini amini vile

IMG_20180824_035924.jpg
 
Primary niliwahi pata zero somo lilikua kiingereza nakumbuka siku ya paper nilikua naumwa afu ndio ilikua paper ya mwisho mwalim alinikomalia nifanye ivyo ivyo nilichojaza humo nadhani ni jina langu tu.
Kiufupi class nilikua kichwa sasa mitihani ikasahishwa watu wakaanza kupokea. Nikiwa nyumbani najiuguza akaja rafiki yangu tokea nje akiniita kwa sauti Heavy Weight nimekuletea mtihani wako.
Haikua kawaida yangu kumiss shule na sikuwai pokelewa mtihani sababu mda wote nilikuepo. Mda huo naitwa tulikua na maza tumekaa barazani ananiuguza hakwenda kazini.

Jamaa akaleta paper imechorwa zero na masikio na macho bi mkubwa alinicheka sana na mimi badala ya kusikitika nikaishia kucheka. Nadhani hata yeye alielewa kwakua sikuwahi pata maksi kama zile shuleni.
Ajabu ule mtihani nikaingia top 5 sababu masomo mengine nilinyoosha

Ila secondary zero ya civics hii ilitoka topic moja tu mwalim alikua anapima kama watu tumepitia pre form one kumbe wengine tulisugua mtaani nikapata zero takatifu

Mtu Mzito HEAVY WEIGHT
 
Ndio, mi mwenyewe nilikuwa sijui. Nashangaa juzi kananiambia kumbe wewe ndo unajiita Thad? Uzi wako nimeuona na msimamo wako nimeuona pia nimekubali....nitakuita shemeji! [emoji16][emoji16][emoji16]
aseeh pole aseeeh
 
Back
Top Bottom