Kiasi watanzania tusiende mbele kimaendeleo,bila hata watu kumjua huyu dogo tayari wameshaijua kazi anayofanya,tayari wameshampa jina la muuza unga,...kesho kutwa polisi watakwenda nyumbani kwake kumpekua kama hawajamuona na kitu watamuwekea kidhibiti,ndio maisha ya Dogo yatakuwa yamemalizia hapo,,,,juhudi zake zote za kupambana ndio zitakuwa zimemalizika na kusahaulika..!!
Kwanini Watanzania tuko hivi,kuanzia Raisi wetu mpaka mtanzania wa maisha ya chini kabisa mawazo yetu yanafanana,tuko na chuki,wivu,choyo,uhasidi..!!
kwanini hatumuombei tu huyu Dogo azidi kufanikiwa,tujiombee na sisi vile vile tufanikiwe ili tusonge mbele katika masiha yetu ya kawaida pamoja na tunaowapenda zikiwemo na familia zetu