Ngoja na mie niseme yangu
lara 1.
Kidogo na mie Biblia nimeisomapo. Tukianzia hapoo, yaani Biblia iko full kuelezea pande zote za shilingi.
Ukisema Ibrahim na Sara, upande mwingine wako Isaka na Rebeka.
Ukisema Hosea na Gomeri, wako Musa na Zipora.
Ukisema Daudi, yuko Esta.
Wako kina Ruthi na Boazi, Mariam na Yusufu, Elizabeti na mumewe. Kina Nuhu, Yusufu, Ayubu na wengine wengi ambao upande wa pili haujasemwa unaweza kuhisi hadi waitwe wema lazima walikuwa wako vizuri kwenye ndoa zao.
Ukiongelea kupenda, Samson na Yakobo, na Sulemani wanaonyesha chaguzi zilivyo ngumu.
Ukisema mwanaume hawezi kuwa mwaminifu ukijitetea kwa Suleiman, Daudi na Ibrahim wapo waseja Danieli, Eliya,Paulo watakuhukumu.
Mwanamke ukisema sitaweza vishawishi kwa reference ya Bethsheba au mke wa Potifa, wapo kina nabii Anna na Tamari watakushuhudia.
Kwa ufupi, dunia yako chaguo lako. Wote, waliochagua kuishi wenyewe au kuwa na ndoa mitikasi ni constant. Ukibahatisha hewala hewala, mkiamua kuwa kama Rebeka na Isaka sawa, pia kama Ahabu na Yezebeli ushirikiano utakuwa juu. Ole wao wapatao aina za Gomeri, Bethsheba, mke wa Potifa, Nabali, Daudi na Sulemani. Ukichagua unafiki, unafiki utaishi ndani yako ya moyo, ukichagua kusimamia show kama Abigaili na kwenyewe ni heri.
Ndoa ni entity isiyo na umbo kama maji. Kwa hiyo wewe kifaa ukiwa ovyo, itakuwa ovyo ukiwa poa itakuwa poa.
Upande wa pili, kwa kina sie tusiofaa ambao hatujakamilika na tungependa kukamilika ndoa ni mtihani mzuri wa kufikia ule utu kamili. Kwa kirefu, hakuna sehemu duniani ukalala na betrayer asiye ndugu yako na kesho ukamsaidia kupata mahitaji yake kwa roho moja eti mke wangu au mume wangu, what a love!