Marriage is an outdated concept

Marriage is an outdated concept

Naungana na hoja katika aya zako tatu za mwanzo ndio maana nikasema sheria ilitungwa kwa kumchora mwanamke wa zamani hakupewa haki nyingi sana ikiwemo elimu na ajira sasa kama mwanamke hana ajira ataishi vipi sasa hapa ndipo inakuja hoja ya kwamba atatakiwa kuhudumiwa na mwanaume hata mgao wa mali anastahili kama jamii inambana sasa akiachwa hana ajira hana makazi ataoshi vipi? Lazima apate gawio lake. Kwa sasa mwanamke kapewa access zote za kutoboa ikiwemo ajira, elimu, kumiliki mali n.k ivyo akiamua kuishi bila kujishughulisha na chochote hayo ni maamuzi yake sio sawa kuchota mali za mwanaume kumpa mwanamke ambae alipewa access zote za kujitafutia ila akufanya ivyo. Ndio maana nikasema sheria imepitwa na wakati sababu mwanamke sio inferior tena kama kipindi ambacho sheria hii ilitungwa.

Kuhusu aya yako ya mwisho, mimi sikatai mahusiano ya mwanamke na mwanamke kimapenzi. Mahusiano yana kupanda na kushuka, nyakati nzuri ja nyakati chungu ni vyema mkakaa chini kumaliza tofauti zenu..kinachonitatiza ni vipengere vya ule mkataba wa ndoa mnaotakiwa kusaini.
hapa ndo pagumu sasa

hatutaki kuwahudumia kwasababu sikuhizi wanajiweza

lakini,

hatutaki watuzidi kiuchumi tunaogopa

pia wenyewe wanajua wanajiweza ila wanataka kuhudumiwa

sio poa
 
Naungana na hoja katika aya zako tatu za mwanzo ndio maana nikasema sheria ilitungwa kwa kumchora mwanamke wa zamani hakupewa haki nyingi sana ikiwemo elimu na ajira sasa kama mwanamke hana ajira ataishi vipi sasa hapa ndipo inakuja hoja ya kwamba atatakiwa kuhudumiwa na mwanaume hata mgao wa mali anastahili kama jamii inambana sasa akiachwa hana ajira hana makazi ataoshi vipi? Lazima apate gawio lake. Kwa sasa mwanamke kapewa access zote za kutoboa ikiwemo ajira, elimu, kumiliki mali n.k ivyo akiamua kuishi bila kujishughulisha na chochote hayo ni maamuzi yake sio sawa kuchota mali za mwanaume kumpa mwanamke ambae alipewa access zote za kujitafutia ila akufanya ivyo. Ndio maana nikasema sheria imepitwa na wakati sababu mwanamke sio inferior tena kama kipindi ambacho sheria hii ilitungwa.

Kuhusu aya yako ya mwisho, mimi sikatai mahusiano ya mwanamke na mwanamke kimapenzi. Mahusiano yana kupanda na kushuka, nyakati nzuri ja nyakati chungu ni vyema mkakaa chini kumaliza tofauti zenu..kinachonitatiza ni vipengere vya ule mkataba wa ndoa mnaotakiwa kusaini.
Binafsi nakuelewa, considered ni mwanamke na siku za usoni naweza kuwa na mtoto wa kiume.

Lakini Je unafahamu ndoa ni makubaliano? Hakuna anayelazimishwa ndoa, amini nakwambia labda ukiwa maiti ndio unaweza kufungishwa ndoa bila kupenda, Sasa kama ni makubaliano iweje wewe ukubali mdada ambaye hana kazi, hajawahi kuwa nayo au hana biashara?

Ngoja nikwambie, Kuna muda tukiolewa tunaambiwa labda acha kazi fanya hii biashara, au acha hii biashara fanya kazi hii au mali hizi tunazalisha lakini zote ziko kwa majina ya mume sababu hata mke ni wa mume vilevile. Hayo makubaliano yanayofanyika Pre-marriage or during marriage ndio yanaamua mwanamke awe compensated wakati wa divorce, Elewa kwanza ndoa ni makubalino ambayo wawili hao kunavitu wamevi-giveup kuaccomodate mahitaji ya ndoa yao. Tuache kuoverlook vitu.

Again, labda huku kwetu tu…. Nchi zilizoendelea hujawahi sikia wanaume wakidai mgao wa divorce? Tunatakiwa tuelekee huko.
 
binti kiziwi na Jadda nahitaji input zenu hapa
Mdogo wangu hiki kitu kinakuzwa kuliko uhalisia, hizi ndoa tunazoziona mtaani ziko na diversity kwa kiasi kikubwa, Hivi mfano mwanaume kutoa hela kwaajili ya chakula cha familia ni kumuhudumia mwanamke??

Hivi we unaamini kuwa kuna wanawake wanafanya kazi wana familia na watoto na wana waume zao na hela zao hazihusiki kwenye kutunza familia? Ingekuwa hivyo wanawake tungetajirika basi.

Mimi ntakuwa mtu wa mwisho kuamini hili.
 
Binafsi nakuelewa, considered ni mwanamke na siku za usoni naweza kuwa na mtoto wa kiume.

Lakini Je unafahamu ndoa ni makubaliano? Hakuna anayelazimishwa ndoa, amini nakwambia labda ukiwa maiti ndio unaweza kufungishwa ndoa bila kupenda, Sasa kama ni makubaliano iweje wewe ukubali mdada ambaye hana kazi, hajawahi kuwa nayo au hana biashara?

Ngoja nikwambie, Kuna muda tukiolewa tunaambiwa labda acha kazi fanya hii biashara, au acha hii biashara fanya kazi hii au mali hizi tunazalisha lakini zote ziko kwa majina ya mume sababu hata mke ni wa mume vilevile. Hayo makubaliano yanayofanyika Pre-marriage or during marriage ndio yanaamua mwanamke awe compensated wakati wa divorce, Elewa kwanza ndoa ni makubalino ambayo wawili hao kunavitu wamevi-giveup kuaccomodate mahitaji ya ndoa yao. Tuache kuoverlook vitu.

Again, labda huku kwetu tu…. Nchi zilizoendelea hujawahi sikia wanaume wakidai mgao wa divorce? Tunatakiwa tuelekee huko.
Hata kama ni makubaliano kama hayupo fair basi yanatakiwa kupitiwa na yawekewe utaratibu ambao haumkandamizi yoyote kumbuka kuna wengine wagumu kuelewa au ni mpaka wapigwe na kitu kizito ndio wanashtuka. moyo wa mtu ni kichaka anaweza kuwa mwema kwako kumbe lengo lake ni mali baada ya kupata cheti cha ndoa hapo ndio heka heka zitaanza kwaiyo suala sio makubaliano tu suala ni kwamba hayo makubaliano yapo fair? hayo makubaliano yakivunjika kila upande utakua satified?

Kama mwanaume alikushinikiza kuacha kazi/ biashara au una msaada wa kiuchumi katika mali zilizozalishwa kwenye ndoa (mfano umechangia mtaji au ujuzi wako wankitaaluma) hapo una haki ya kupata percent yako lakini kama mwanamke alikukuta tayari ushajipata na hana mchango wa moja moja kwenye mishe za mwanaume basi uyo hana haki ya kupata mgao.
 
Una uhakika kuwa hajawaambia??

Hili ni suala la kijamii,halihusu baba,mama wala dada,linawahusu wanajamii wote,hao dada zake na shangazi zake yeye hawezi kuwaoa.

Hivyo ana haki ya kuwasilisha jambo hili kwenye jamii ili jamii ijifunze.
 
Nadhani unayo hoja ya msingi kabisa. Ila kukufumbua macho zaidi ni vema ukafahamu kuwa ndoa haijawai wala haitawahi kuja kuwa outdated concept bali shida ni wahusika wanaoingia ndani ya ndoa kutokuwa na vigezo au uwezo wa kusimama ndani ya ndoa.

Kuna sababu ambazo kimsingi zinasababisha ndoa katika kizazi cha sasa kuwa kazi kubwa kuitumikia, na sababu zenyewe ni kama ifuatavyo:

1. Ndoa ni taasisi, na kila taasisi ndani yake ina watendaji wenye vigezo na uwezo wa kuitumikia. Huwezi kuajiri askari jeshi bila mafunzo ya jeshi. Huwezi ajiri muhasibu bila kufuzu mafunzo ya chuo na CPA, huwezi ajiri mkemia bila kuwa na cheti cha mkemia, je kwenye ndoa, hawa mabinti wa kisasa na vijana ni wapi hukaa kambi hata ya mwaka m'moja kupitia mafunzo makali ya ndoa?

2. Wanaume wameshusha sana standards zao kwa wanawake na wanawake wamepandisha sana standards zao kwa wanaume. Mwanamke zamani aliqualify kuwa mke kwa kuwa bikra kama sifa ya lazima, halafu tabia nzuri ikawekwa kama sifa inayofuata ya lazima.

Leo hii wanaume hii sifa hamuhangaiki nayo tena wanaume wengine wanatetea kabisa kwa kusema kwan kuna ubaya gani akiwa hana bikra, hawa ni wanaume wanaotetea si wanawake, sasa kwann wanawake wasikubaliane na huo uhalisia kuwa wanaume hawana shida na bikra watatuoa hata wakikuta tulishazaa na wanaume kwahiyo wacha tukachezewe kuna mabwege yatatulipia mahari na kutuoa.

3. Wanaume miaka hii wamekuwa wakwepa majukumu au wabeba majukumu yasiyowahusu. Mwanaume anazaa na binti ila hajui wajibu wake kama Mume na baba, hajui majukumu yake kwa kitu alichokianzisha mwenyewe anatoa toa macho kama ng'ombe na kusubiria wakwe, mashemeji, na familia yake wafanye jambo kumsaidia. Au anakutana na mwanamke ambaye sio wake ana watoto yeye huyo kabebelea, ni wa kwako? Kwann usitafute wa kwako? Hiyo roho nzuri si ungelea watoto wa dungu zako wenye hali ngumu, kwenda kulea mabao ya watu halafu ndio uitwe mwanaume wa shoka ni ujinga kutoka sayari gani huo? [emoji848] Kwa sampuli hii ya wanaume ndoa haiwezi kuwa imara.

4. Kudharau mafunzo ya kimaadili na Maagizo ya mwenyezi MUNGU ambayo kaagiza watu kuyafuata ili kuwa imara kiimani na kimwili ila viburi sasa vya wanadamu leo ndio matokeo yake tupo hapa ndoa zinaendeshwa kwa idea za movies za Hollywood, tamthiria za Telemundo, na hawa relationship coaches wa mitandaoni.

5. Wanawake wa sasa ni wavivu eneo la ndoa ila wanabidii kujihangaikia. Mwanamke unaweza mkuta alikuwa amepanga analipa Kodi kwa biashara ndogo ndogo au ameajiriwa lakini siku ukianza kaa nae ndani hatochangia hata 1000 endapo kutakuwa na dharula na mwanaume haupo karibu au haupo na vema kiuchumi kwa kukwambia wewe ni mwanaume as if yeye ndie huwa analipa 100% ya bills. Kwa kifupi ubinafsi.

So kimsingi Ndoa haijawai na haitakuja kuwa outdated concept shida ni wahusika kutokutambua na kusimamia vigezo vya ndoa na kuisimamia vilivyo kwa kila mojawapo kukaa eneo lake na si kuingiliana.
 
Back
Top Bottom