Martha Mwaipaja atoboa siri sakata la Rose Muhando

Mkuu mimi sifahamu kitu chochote bali niliyoyaandika hapa ni maelezo ya Martha Mwaipaja ndiyo maana kwenye andiko hili jina Martha Mwaipaja limetokea kama lote, yote hii ni kwa kuwa sijafanikiwa kupandisha clip ya Martha Mwaipaja akiongea. Hivyo kama kuna sehemu pamepotoka wewe jazia tu usipate taabu.
 
Leteni na habari za mmoja ya wale wacheza show wake, sio nathan tu.
 
Better late than never! Ni heri taarifa hii imechelewa kufichuliwa kuliko isingefichuliwa kabisa.
 
mpaka ninajihisi vibaya,huo ni utumwa

tofauti na saida karoli ni ndogo sana
 
mkuu tunaomba na wewe utupe ukweli unaoujua ili sote tuone namna ya kumbeba Rose........


unaposema baada ya Nathan aliangukia kwenye mikono ya watu wabaya, ni kina nani hao?.............


hao vijana wake ma dancer ana uhusiano gani nao zaidi ya kutumbuiza? nao alikua anazini nao?.....
 
Sasa MTU amejihusisha na utaje mnaanza msingizia roho sijui
 
Hadithi hii umeegemea upande mmoja wa shilingi na hivyo huyo Nathan anabebeshwa lawama zote.. ..!kana kwamba Rose kalikuwa ni katoto kadogo under 18 hakajui madawa ya kulevya ni mabaya,kuzini tena na mume wa mtu ni dhambi,n.k..!embu acheni unafiki.Mtu huvuna anachokipanda hata kama ulipanda gizani.
 
SIO kweli.

Ni kweli kabisa Nathan alikuwa Menaja wake.

Kama ni hivyo amewezaje kuwa magari mengi na majumba? Kama sio mafanikio kutoka kwa meneja wake?
.
Rose alishiba kiburi.

Tunaomjua Rose hakuwa ameokoka.

Unajua wakati yupo kwaya ya Chimuli Rose Mhando alikuwa anafanya kazi za house girl?

Alipoinuka Kimusiki hakukumbuka alipo toka.

Hata kanisa alilokuwa anasali alikuja kuhama.

Huyu Nathan watu wanamchukulia poa tu. Ni matajiri wa kutisha hapa dodoma. Hapa dodoma ukisema unapesa unajiita mimi ni maluganji. Mwaluganji ni baba yake Nathan ambaye wakati huo alikuwa ni mtu tajiri sana. sasa Nathan si mtu wa kumdhurumu Rose Mhando.

Mwaipaja msiteteane kwa ujinga ujinga. Bila Msama na hawa akina Nathani wahindi wangewafanya vibaya sana. Wakina Nathani na kina Msama wamejitolea kuwatoa katika makucha ya wahindi wa kariakoo leo mnasema walikuwa wanawaibia.

Tutawasikia sana mkiweweseka. Rose maisha haya kwenda kombo na kutumia dawa au pombe au kufirisika yalianza muda mrefu sana Je wewe Mwaipaja ulimsaidia nini?

Wengi wenu mlikuwa mkimkwepa ili msije mkafananishwa naye leo mnajifanya mtetezi wake shame!

Rose Mhando yaliyomkuta yamemkuta atarejea tena kwa nguvu mpya na ujasiri wa Bwana.

Mwaipaja umefanya kosa kubwa kutaja hadhalani mambo ya mtu binafsi (Personal) wewe ni nani?. Wewe ya kwako ni yapi? Tunajua waimbaji wa Injili maarufu wengi wenu mmeachika na waliobaki ndoa zao ziko hoi kabisa.
 
You know nothing about Music Industry, ushajiuliza kwanini wasanii wengi hujiingiza katika madawa ya kulevya? na ilihali wanaona kabisa wenzao walioathirika na madawa wapo vipi.

This shit is real, usiombe mpendwa wako ajikwae huko.
 
kwahyo kumbe kuna time alikuwa anapiga vyombo then ana perform....

Ila hizi menejiment za kibonGo ni laana tupu..nilijua ni kwa wadada wa bongo fleva tu wanafanyiwa hivi kumbe hata Gosple
 
Yes, baada ya kumuingiza kwenye madawa unahisi angekua tena yule Rose wa zamani? hayo yote uliyoyasema ni matokeo ya madawa ya kulevya aliyokua anapewa na huyo Nathan.

Hapo hawezi kuchomoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…