Nimesoma haya maelezo kuna nusu ya ukweli na Nusu ya chumvi.!
Binafsi ni muandaaji wa Matamasha haya ya muziki wa injili. Nimeanza kufanya kazi na Rose mwaka 2007.
Akiwa chini ya Nathan, na bila shaka Nathan ndio meneja pekee Rose aliyewahi kuwa naye.!
Nathan alimuwezesha Rose kuwa na maendeleo kadhaa, Nathan aliweza kumsaidia Rose kumiliki magari kadhaa ikiwemo Rav 4 ya blue gari yake ya kwanza kisha baadae prado .alimuwezesha kuwa na makazi yake pale ipagala.!
Rose alipoamua kuachana na Nathan kwa sabbu anazozijua yeye aliangukia kwenye mikono ya watu kadhaa, mbona haujaeleza habari za yule meneje mchungaji Fake aliye mnyang'anya passport na gari zake?
Wakati akienda marekani?
Rose kaanza kupotea hewani baada ya kuondoka kwenye mikono ya Nathan hakujua tena upepo wa umaarufu wake unampeleka wapi. Hakuwa na Nguzo imara tena kwa kazi zake.!
Baada ya kuachwa huru na Nathani kila mtu alikuwa anajipigia je amekueleza kuhusu wale vijana aliokuwa anaambatana nao pale Dodoma?
Mimi binafsi Rose Muhando keshakula pesa yangu nyingi tu, na wala sio Nathan, kuna watu amewaumiza zaidi ya unavyoweza kuleta hayo maelezo ya Martna. Isingekuwa muziki wa Injili natumai angekuwa amefanyiwa kitu kibaya sana!
Mara ya mwisho nimemtafuta Rose mwezi huu tarehe 13 . Kupitia kwa Producer wangu na akatoa maelezo kuwa kazi yoyote atakayopaswa kuifanya ipitie kwa Meneja wake Nathan.
Hii ikiwa kabla ya video ya Nairobi haijaanza kusambaa mitandaoni.
Mwisho. Rose Mhando bado ana nafasi ya kufanya vizuri zaidi kama atampata mtu sahihi wa kumsimamia Kiafya, na kazi zake kwa ujumla.
Usione vinaelea vimeundwa bila Nathani usingemfahamu Rose mhando.