Martin Maranja Masese amchambua Hayati Magufuli (JPM) mwanzo mwisho

Martin Maranja Masese amchambua Hayati Magufuli (JPM) mwanzo mwisho

kipindi cha jiwe nchi yetu ilikua donor country, tuliwapa msumbiji msaada na malawi, kipindi cha jiwe tuliwatikisa wazungu jiwe alinipa ujasiri wa kukataa chanjo za mchongo, jiwe ni jiwe.
Yaani wewe huna akili mpaka ukapewe ujasiri wa kukataa chanjo na mwanaume mwingine tena Jiwe
 
Watu uchwara wanaojidai kujua kuliko Mungu... Kila kinachotokea sehemu kubwa ni mipango ya Mungu hivyo hakuna kuwahi wala kuchelewa.
USISIFIE mtu hovyo mpaka ukamkosea Muumba hiyo ni kufru kubwa sana na nikuvuka mipaka...
 
jiwe alijenga masoko nchi nzima jiwe alijenga hospitali za mikoa nchi nzima jiwe alifukuza watu waliochongesha vyeti jiwe amejenga sgr jiwe kajenga bwawa la umeme la kihistoria, jiwe kajenga stendi nzuri za mabasi nchi nzima mimi kama mtanzania mawazo yangu binafsi jiwe angekuepo ningemruhusu ajilimbikizie mali anazotaka kama gadafi, wakati wa jiwe nilienda hospitali nilihudumiwa kama niko uk, jiwe amelala nimeenda tena hospitali nimehudumiwa kama niko somalia, jiwe ni jiwe. jiwe namfananisha na putin mwanaume lazima uwe na misimamo.
So unakili kuwa wewe unauwezo mdogo kuliko Jiwe?
 
Demokrasia na maridhiano vimefanya sukari iwe shilingi ngapi? Namudu maisha yangu sijisifii unyonge ila ninafahamu kuna wanyonge wana haki pia ya kupata nafuu ya maisha, kuwa daraja la kati kimaisha kusikufanye usahau walio chini yako
Mimi ninachomaanisha ni kuwa usijisifie unyonge hata kama uko daraja la chini. Pambana utoke huko. Ukishindwa kutoka huko ila umepambana basi hayo ni matokeo tu. Swala la kujiita mnyonge siyo zuri utabaki kuchukia matajiri tu
 
Siku nikiwa rais wa nchi hii nitamfuta kwenye kumbukumbu za serikali asitambulike tena kama mtu aliyewahi kuhudumu kama rais wa nchi hii
Utakuwa rais wa magasho wenzio
 
Machadema bado yanabutuliwa na JPM hata baada ya kufa
 
So unakili kuwa wewe unauwezo mdogo kuliko Jiwe?
jiwe alikua kidume na nusu, wewe kwanini nijifananishe naye mimi ni mimi niko nyuma ya keyboard yeye aliwanyosha vibaraka wa magasho mchana kweupe mafisadi walisota rumande, ila jiwe aliwafundisha wapinzani kupambana sio kulia lia kutafuta huruma ya wananchi bila kupambania wanachotaka.
 
Yaani wewe huna akili mpaka ukapewe ujasiri wa kukataa chanjo na mwanaume mwingine tena Jiwe
jiwe alikua anatembea kwenye maono yangu mimi niligoma chanjo ya mabusha nikiwa high school miaka hiyo, kabla ya jiwe kua presidenti na sina busha hadi leo lakini jpm aliokoa wengi kwanza alitutoa woga na makorona watu wachache walipotea tz na wengi sababu ya magonjwa mengine hasa ugonjwa mkubwa ulikua ni woga sio kingine.
 
Ni vyema kujifunza kupitia historia
 
Kusemwa lazima asemwe milele ili isijetokea tukapa kiongozi kama yule tena. Vizazi vyote lazima vijue hilo
Kumsema ni sawa na kumfufua, hii ni kuthibitisha wazi kuwa hajafa na ndio maana mmechagua kumsema. Atakuwa amekufa pale tu mtakapo sitisha kumsema.

Hivi hujui kuwa kumsema JPM unazalisha mbegu nyingine ya JPM mpya?

Siku akiibuka JPM mpya ndio utaelewa ninachokwambia.
 
😅😅 Linalalamika lilitekwa likauliwa 😅
Wapi nimelalamika kuwa nilitekwa? Dah aisee kuna wazazi wana hasara. Nilikuwa najiuliza wafuasi wa Jiwe wanatoka wapi, kumbe ni watu kama wewe
Kumsema ni sawa na kumfufua, hii ni kuthibitisha wazi kuwa hajafa na ndio maana mmechagua kumsema. Atakuwa amekufa pale tu mtakapo sitisha kumsema.

Hivi hujui kuwa kumsema JPM unazalisha mbegu nyingine ya JPM mpya?

Siku akiibuka JPM mpya ndio utaelewa ninachokwambia.
Yaani kwa uovu ule aliotenda unataka aachwe kusemwa? Nduli Amin mpaka leo anasemwa na ndiyo itakavyokuwa kwa Jiwe
 
Back
Top Bottom