Marubani wanalazimishwa Kutua Bukoba Airport?

Marubani wanalazimishwa Kutua Bukoba Airport?

Binafsi nilikuwa najua hiyo Airport ni kubwa kumbe ndio hivyo!!

Kwahiyo ni kama viwanja vya huko kwenye mbuga zo wanyama zinakotua ndege ndogo ndogo.
Ndiyo maana umewekwa ziwani kama likitokea la kutokea(kama la precision Air) ngoma iishie ziwani kupunguza madhara.
 
Kwa nini sasa walazimishe? ningekuwa rubani nasubiri maofisa kama wote wa Serikali ndani ya ndege afu naitokomeza ndani ya maji ...vile vile.
alafu anatokea super hero mwengine kama majaliwa anavunja mlango kwa mwiko wa ngalawa kisha wanatoka wote hahahaha
 
Airdomes , Air strips haziwi na tower

Hapo unatumia VFR kutua na kupaa, maana hakuna IFR kama ILS ambazo zinakuwezesha tua hata hali ikiwa mbaya (isiwe upepo tu)
Lakini huwezi tumia VFR kama hali ya hewa ni mbaya(poor visibility, FOG, n.k)
 
Kila kitu majaliwa. Huyo Waziri wa Zanzibar, wa uchukuzi humuoni? Waziri Mkuu na Viwanja vya ndege ana husikaje? Ww binafsi ume panda ndege mara ngapi? Je ndege ndio kipaumbele sana akilini mwako?
Ndivyo unavyo jitetea bwana kassim majaliwa? Kama umechoka na majukumu achia kiti waje wenye uwezo wa ku handle issues. Zanzibar na viwanja vya huku bara vinahusiana vipi? Usipanic shughulikia jambo hilo. Au kama wewe ni chawa fikisha ujumbe
 
Kiujumla usafiri wa anga hapa Tz umekaa kimagumashi mnoo, ukiondoa KIA (Pale Kilimanjaro), JNIA (Dar) na Zanzibar ambapo ndege nyingi za kimataifa hutua, sehemu zingine bado kuna walakini sana, kuna ubabaishaji mwingi ajabu.
 
Nimeshangaa sana hata mimi. Yaani uwanja unaotua ndege za abiria hauna control tower?
Uwanja wa ndege wa Bukoba ni upgraded Airstrip, siyo uwanja wa ndege halisi.
Airstrip hazina Control Tower wala Aircraft Controller.

1668846021537.png

Uwanja wa ndege wa Bukoba(Airstrip) mimi nimeshatua pale na ulikuwa unakuw serviced na vindege vidogo sana size ya Twin Otter- The de Havilland Canada DHC-6 Twin Otter ia Canadian STOL (Short Takeoff and Landing) utility aircraft .
Hivi vindege ni vya watu 18 hadi 20.

Sasa yameingia madege makubwa na mazito ya 45-55, uwanja huu hautoshi.
 
Hata tukifa watanzania kwani wao inawahusu nini haswa, wanapata hasara gani wakati biashara zao na familia zao ziko salama salimin
 
Hata hapo Mwanza pamoja na AIr Control Tower kuna kipindi kunatibuka inabidi Kutua Rubondo Island kupisha Mwanza kutulie
 
Airdomes , Air strips haziwi na tower

Hapo unatumia VFR kutua na kupaa, maana hakuna IFR kama ILS ambazo zinakuwezesha tua hata hali ikiwa mbaya (isiwe upepo tu)
Terminogy za traab and traats mpaka hapa ushaniingiza kichochoroni huu mzigo mpaka nikuele ni copy nika pest google[emoji16][emoji16]
 
Sasa hivi pakiharibika Mwanza airport waende Chato badala ya Rubondo
 
Back
Top Bottom