Marufuku Mtanzania kujiunga Jeshi la nchi nyingine

Hiyo marufuku yake nani ataisikiliza? Yaani watu waache fursa kwa sababu ipi yaani?
 
Mbona wengi walienda kujiunga Congo, Iraq, Sudan kusini, Marekani hamkutoa angalizo
 
Huyo hakujiunga kwa hiyari yake bali kwa kulazimishwa, Serikali ilitakiwa kutoa tamko kuilaani Urusi kwa inachokifanya hasa kwa wageni maana ni kinyume na haki za binadamu.
 
Kwani wale Wagner ni jeshi la nchi nyingine au ni “mercenaries”?!
 

Kwa wale tulosoma uganda mwanzoni mwa miaka ya 2000 mtakumbuka kule kulivyo na wanajeshi wengi watanzania tena wengi naona wapare!
Mi nilikua najiuliza wanapataje hizo nafasi tena za jeshi?
Nikaishiwa kuambiwa tu kuwa ni wanajeshi wastaafu wa tz!
Na kuna wale wajeshi wawil nawaonaga kwenye instagram wa marekan wale nao vepe?

Mwenye uelewa!
 

Unaowaona insta wameukana uraia wa tz kabla ya kujiunga kwao. Maana jeshi la marekani lenyewe linalazimu uchukue uraia wa nchi hiyo kwanza
 
Kuna watanzania wengi nawafahamu ni wanajeshi wa marekani lakini badala ya kutoa kauli kali atueleze balozi zetu zinafanya Nini pale watanzania wanapopata matatizo wakiwa nje ya nchi.
Wanahakikisha wanapata mawakili pia wanapata muda wa kuwatembelea ni wazi Kuna uzembe kwenye wizara yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…