Tetesi: Marufuku ya kuzidisha abiria ili kupambana na Corona, Daladala zimeanza kugoma Dar es Salaam

Hii ni emergence kipind hiki ni cha muda, wavumilie.
 
hapo kwenye kupunguziwa bei ya mafuta ni ngumu sana kwasababu serikali haifanyi biashara ya mafuta na hata kama ingekuwa inauza mafuta hakuna namna ambayo ingeweza kupunguza bei ya hayo mafuta.
Tatizo letu Watanzania ni kutofuata sheria au maelekezo ya serikali hata kwa mambo muhimu kam kujikinga na maradhi ya COVID 19. Kenya waliweza kuzuia matatu kubeba abiria zaidi lakini sisi hapa umekuwa kama wimbo! Juzi nilisafiri kwenda Msho kutoka Arusah, coaster ilijaza abiria wakiwa wamekaa watano watano na wengine walisimama licha ya serikali kutoa maelekezo ya kutobeba abiria wengi zaidi
 
Pa;e moshi kulikuwa na katazo la kutupa takataka ovyo, kwa jinsi watu walivyokuwa wanatozwa faini, ilibidi wajiongeze na Mji ukawa msafi. Kwa hiyo, hata daladal ziwekewe utaratibu huo, abiria akikutwa amesimama katika daladal apigwe faini na dereva pia apigwe faini. Hapo tutatii sheria bila shuruti
 
Level seat kwa daladala za Dar mmh haiwezekani, kuna kipindi walileta hii sheria ila iligonga mwamba.
Hayo mataifa mengine ambayo usafiri ni level seat wao wamefanikiwaje??
 
Haya ndo mawazo ya "kipumbavu" naomba mnisamehe kwa kutumia neno hili, kuna mtu ashawahi kuniambia sikumuelewa kwamba " utajiri huondoa utu,matajiri ni wachache Sana wenye roho za kujali binadamu,wao huwaza pesa tu"

Nilibishana nae sana lakini naanza kumuelewa, yaani nyie mnawaza kupiga PESA tu, what a shame!

Jumatatu nilipanda dala dala kondakta na dereva wake wakaleta mawazo ya kipumbavu kama haya na baadhi ya abiria nadhani siku hiyo hawatasahau hawa kondakta na dereva wake, walijaza gari then nikauliza kondakta hujapata taarifa ya serikali kuhusu Corona? Akanijibu toa umaskini wako ! Dah nilikasirika nikamuacha akawa amepandisha abiria nikamwambia sasa utajuta kwanini unatamani pesa kupitia majanga, nikawambia maabiria wote msiokaa kwenye siti jiandaeni kutoa faini koz mmekiuka utaratibu uliotolewa na serikali mmeshiriki na kondakta,hapo kwa mbele kulikuwa na trafiki walipiga kelele wanataka kushuka nilipata sapoti then nikawambia muache kujitia uchizi, waliomba kushuka wote then dereva nikamwambia lazima mtoe elimu na si vinginevyo wote kimya , nikamalizia hasira zangu kuwafoka with logical reasons na abiria nikawaambia tuacheni kujitoa ufahamu kama wewe umekata tamaa na maisha kakae huko ila siyo kuhatarisha maisha,

Ujinga kabisa!

Acheni kuwaza hela nyie watu, na serikali naishauri isichukue hata punje la ushauri huu ulioutoa, ndorobo wakubwa nyie, nchi inaingia kwenye hatari nyie mnawaza hela tu, stupid!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
...Mbona unafanya ya Muwamba Ngoma Huvutia kwake??
Sema tu kweli utaeleweka.
Daladala za kawaida zote tunazojua za route ya Mbezi - Mbagala zote ni seat 30. Na sio wote wanaoanzia mbezi wanakwenda Mbagala.
Humu njiani kuna kushuku na kupanda kibao.
Seat moja inapofika Mbagala inakuwa imekaliwa hata na watu watatu!

WKati mwingine Serikali inapaswa kuwa kichwa maji tu na Kusema amri ni hii, anayetaka aendelee kufanya kazi kwa amri hii na asiyetaka akaweke gari lake Uwani afugie kuku!
Hawa hawa wanaotingisha kiberiti wataingia wenyewe barabarani!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea bila kushirikiana na akili yako.hivi unajua madhara ya watu kutokwenda kazini kwa wiki moja.yaani umeandika upuuzi tupu huku jazba ya waziwazi imekujaaa.nyinyi ndio huwa mnakuwaga na maneno machafu kwenye daladala
 
hapo kwenye kupunguziwa bei ya mafuta ni ngumu sana kwasababu serikali haifanyi biashara ya mafuta na hata kama ingekuwa inauza mafuta hakuna namna ambayo ingeweza kupunguza bei ya hayo mafuta.
Namna ipo, kwa kuvipunguzia kodi vituo vya mafuta na kodi nyingi za vyombo vya usafiri kwa msimu huu na kupanga bei ya dharura,kama baadhi ya chi nyingi zilivyofanya kwa vitu vyote.Sisi tuzingatie kwanza usafiti kisha mengineyo.Wanashindwa mini,mbo8na misaada wanapata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…