Tetesi: Marufuku ya kuzidisha abiria ili kupambana na Corona, Daladala zimeanza kugoma Dar es Salaam

Tetesi: Marufuku ya kuzidisha abiria ili kupambana na Corona, Daladala zimeanza kugoma Dar es Salaam

Kwahiyo unaona serikali hawajui ni kiasi gani unapata au hasara? Watu wanaingia na kushuka mpaka gari linafika kituo cha mwisho sit ilishakaliwa Mara nne.hutaki acha wanaoweza watafanya.
 
Kwahiyo unaona serikali hawajui ni kiasi gani unapata au hasara? Watu wanaingia na kushuka mpaka gari linafika kituo cha mwisho sit ilishakaliwa Mara nne.hutaki acha wanaoweza watafanya.
Watu msiopanda daladala mnaonaga rahisi sana, gari ya kutoka tegeta to kkoo abiria wa kwanza kushuka ni moroco utapakia abiria gani tena kuanzia hapo?

Yaani hata kwa akili ya kawaida haiwezekani hata kidogo, mwendokasi ya serikali wenyewe wameshindwa pakia level seat

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa utaratibu huu itakuwa vigumu sana. Biashara ya dalal dala ni ngumu sana. Mfano hapo Mwanza dalala kwa kawaida inatoza Tshs.400 kwa tripu na nyingi zina viti vya abiria 15 kwahiyo kama ni level seat itachukua abiria 15 @ 400 = 6000 na kwa siku inaenda safari 20 yaani kwenda safari 10 na kurudi safari 10 na hivyo Tshs.6000x20 Tshs.120,000. Mafuta kwa siku ni kama lita 30x2260 = Tshs.67,800, Hela ya Tajiri kila siku Tshs.50,000. Hela ya wale wajamaa Tshs.5,000, Hela ya dereva na tingo Tshs.20,000, Mafuta kwa siku inayofuata Tshs.67,800. Hvyo gharama yote kwa siku ni Tshs.210,000. Mapato kwa siku ni Tshs.120,000 - 210,000 (-90,600) ambayo ni hasara. Kwa utaratibu huu itabidi Serikali ikae chini na Wadau wote wanaohusika na usafiri ili muafaka upatikane.

Mzee umechambua vema sana hizo gharama za uendeshaji daladala ‘Mwanza’ kwa siku, ila sielewi kitu kimoja hebu nifumbue macho:

Ninavyojua mimi [ninavyosikia], dereva anakabidhiwa gari ikiwa na mafuta ‘full tank’ anaanza kazi.... anachotakiwa ni kuhakikisha akirudi kupark gari iwe full mafuta kama alivyokabidhiwa.

Sasa hapo umepiga hesabu ya mafuta mara mbili, kwa maana mafuta ya siku na mafuta ya kesho.... hili likoje..?

Na ni kweli kila siku tunaona daladala zikiingia ‘sheli’ kujaza mafuta kila wakati, sasa lile full tank walilolaza jana linaishia wapi.? kama umenielewa nipe shule hapo.
 
Wakuu,

Serikali imepiga marufuku daladala kusimamisha na kujaza abiria, taratibu ambao haukuzoeleka sana haswa kwa jiji la Dar.

Mimi nikiwa mmoja wa wamiliki wa daladala hizi naishauri Serikali mambo machache haswa katika kipindi hiki cha mpito kwakuwa Serikali imesema daladala itakayosimamisha abiria itapigwa faini laki Tisa au gerezani miaka miwili ifanye hivi ili kubalance situation.

Mfano daladala ikitoka mbezi hadi Temeke umbali wa kilomita 37 Kila abiria analipa 600 na daladala moja inasiti za abiria 26 hadi 22 akifika temeke anakuwa anapata 15600tsh hadi 13200tsh ambapo kwa umbali huo gari inaweza kutumia lita 5 ambapo ambapo ni sawa na tsh 11000.

Sasa Kama gari hadi inafika Temeke imekusanya 15600 za nauli ukitoa mafuta 11000tsh inamaana daladala hi itabakiwa na 4600.

Sasa kwa namna hii je huyo dereva atapataje hesabu na posho yake ya kila siku, bado kuna zile pesa za kupigia kiwi za jamaa zetu wale aliosema mkuu ambapo kwa siku nzima huenda zikafika 10000 tena hizi huwa hazinaga ubishi lazima utatoa tu.

Ushauri wangu, Serikali ipunguze bei za mafuta kwa daladala zote ikiwezekana iwe na vituo vyake vya mafuta na maduka yake maalumu ya vipuri pia Serikali itafute muda ikae na wadau husika lakini sio kufanya maamuzi bila kushirikiana na wadau watakaoteseka ni wananchi wakawaida wanategemea magari haya.
Kwa namna Gonjwa lilivyozito na linavyotisha potelea pwete, Dar es salaam ni eneo dogo sana. Bora wagome tu nayo itakuwa njia ya kupambana na Corona. Kwa Mtazamo wangu huyo Mwanaharakati wa Madereva ataanza kutekeleza sheria mara tu baada ya Mwenyewe au Mke wake au Mtoto wake kupata Corona-Covid 19
 
Bajaji zitapiga hela sana,kama route ya kwetu Kimara/Mbezi kwenda Mwenge ni mwendo wa Bajaji tu ,hakuna kubanana kwenye mwendokasi au madaladala.

Route za Bagamoyo ni Seat Level tu week iliyoisha nilienda shamba Kiwangwa hakuna kusimamisha abiria.
 
Mzee umechambua vema sana hizo gharama za uendeshaji daladala ‘Mwanza’ kwa siku, ila sielewi kitu kimoja hebu nifumbue macho:

Ninavyojua mimi [ninavyosikia], dereva anakabidhiwa gari ikiwa na mafuta ‘full tank’ anaanza kazi.... anachotakiwa ni kuhakikisha akirudi kupark gari iwe full mafuta kama alivyokabidhiwa.

Sasa hapo umepiga hesabu ya mafuta mara mbili, kwa maana mafuta ya siku na mafuta ya kesho.... hili likoje..?

Na ni kweli kila siku tunaona daladala zikiingia ‘sheli’ kujaza mafuta kila wakati, sasa lile full tank walilolaza jana linaishia wapi.? kama umenielewa nipe shule hapo.
Wengine hupewa gari ina lita10 tu ndio kianzio, ndio maana unakuta gari inaingia sheli inajaza ya 5000 au 10000 ili ikipaki ibaki na mafuta kidogo ya kuanzia,
Pamoja na kupigia mafuta mara 2 hata ukitoa hiyo moja bado ni hasara tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa hapa ni wenye magari kupunguza hesabu yao tu hakuna namna nyingine, gari inapiga ruti saa 11 asubuhi adi saa 5 usiku na bado hesabu na posho ni changamoto sembuse wapakie level siti?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali kazeni hapo hapo hakuna viumbe wanajiona wameyapatia maisha Kama madereva na makondakta wa daladala...

Naomba wabinywe haswaaaaa Kama hawataki wapaki gari zao tutapanda bajaji au Uber za pikipiki....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dawa yenu nyie wabishi ni museveni. Daladala zote zifungiwe na hiyo tsh 4600 mkose. Mkale polisi.

Kwani kwa siku gari inapiga trip ngap?

Yani mnashindwa ku adjust kidogo katika kipindi hiki kigumu kwa mda mfupi ili huu ugonjwa uwe controlled, kazi ziendelee kama kawaida. Kwa hiyo unathamini pesa kuliko uhai wa mtu. Haya jaza hao watu kama nyanya waambukizane corona wakufe wote tuone hiyo 4600 utaitoa wapi mbuzi wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Serikali imepiga marufuku daladala kusimamisha na kujaza abiria, taratibu ambao haukuzoeleka sana haswa kwa jiji la Dar.

Mimi nikiwa mmoja wa wamiliki wa daladala hizi naishauri Serikali mambo machache haswa katika kipindi hiki cha mpito kwakuwa Serikali imesema daladala itakayosimamisha abiria itapigwa faini laki Tisa au gerezani miaka miwili ifanye hivi ili kubalance situation.

Mfano daladala ikitoka mbezi hadi Temeke umbali wa kilomita 37 Kila abiria analipa 600 na daladala moja inasiti za abiria 26 hadi 22 akifika temeke anakuwa anapata 15600tsh hadi 13200tsh ambapo kwa umbali huo gari inaweza kutumia lita 5 ambapo ambapo ni sawa na tsh 11000.

Sasa Kama gari hadi inafika Temeke imekusanya 15600 za nauli ukitoa mafuta 11000tsh inamaana daladala hi itabakiwa na 4600.

Sasa kwa namna hii je huyo dereva atapataje hesabu na posho yake ya kila siku, bado kuna zile pesa za kupigia kiwi za jamaa zetu wale aliosema mkuu ambapo kwa siku nzima huenda zikafika 10000 tena hizi huwa hazinaga ubishi lazima utatoa tu.

Ushauri wangu, Serikali ipunguze bei za mafuta kwa daladala zote ikiwezekana iwe na vituo vyake vya mafuta na maduka yake maalumu ya vipuri pia Serikali itafute muda ikae na wadau husika lakini sio kufanya maamuzi bila kushirikiana na wadau watakaoteseka ni wananchi wakawaida wanategemea magari haya.
Ushauri wangu, paki daladala lako, jikinge na Corona na uepuke kusambaza kwa wengine. Ukiamua kuingia barabarani, fuata maelekezo ya Serikali dhidi ya uambukizaji wa Corona! Ukakaidi, ushughulikiwe!
 
Watu msiopanda daladala hamfikirii vizuei kwa kifupi level seat haiwezekani daladala zipo chache watu wanaopandia vituo vya katikati watatembea kwa miguu..
Na hata waliopo wanapoanzia gari wanaeza kwenda kwa mguu vile vile mana sie wapanda daladala tuna tabia ya kugeuza na gari vituo kadhaa kabla yani itakua tafrani..

Hakuna mtu anaependa kusimama sema ukileta ubishoo wa kusubiri siti kazini utafika saa 5

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengine hupewa gari ina lita10 tu ndio kianzio, ndio maana unakuta gari inaingia sheli inajaza ya 5000 au 10000 ili ikipaki ibaki na mafuta kidogo ya kuanzia,
Pamoja na kupigia mafuta mara 2 hata ukitoa hiyo moja bado ni hasara tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama akipewa gari ina lita 10, si naye atapaswa kuilaza na lita 10..?

Hawa daladala sio wajinga, wanapiga hela sema wanapenda kulialia.... wakidakwa na wale jamaa mbona huwa zinawatoka tu bila shuruti.!!
 
Sasa wewe mkuu bila hao abiria kuwa na afya utapataje ata hicho kidogo jalin afya kwanza maslah badae kwa uchum wote WA dunia umeyumba
 
Shukuruni kuruhusiwa kupakia hiyo level seat, huko Uganda wamesimamisha kabisa public transport.
 
Back
Top Bottom