Mkuu sio lazima iwe mbezi--- temeke,
mimi naenda g.lamboto---ubungo,
Kituo cha kwanza kuanza kushusha ni buguruni. Ukitoka hapo ni stand ya mkoa!
Natumia mafuta ya tsh. 13,000. ( Kwenda tu)
Level seat ni abiria 42 nauli ni 500. Napata 21,000 tu.
Labda kwa bahati baada ya kushuka watu, wapande wengine 10(ni wengi sana!)
Nitakuwa na jumla ya tsh. 26,000×10 (trip ninazoenda kwa siku. Nikikomaa sana naenda 12. Ambazo ni =312,000.
Pia kuna mida ya mchana abiria sio wengi.
Matumizi kwa wafanyakazi 3 kwa siku tsh. 20,000.
Kubrash viatu 10,000.
Mafuta 130,000.
Hesabu ya gari 140,000.
Kulaza gari na kuliosha 7,000.
Jumla ni 307,000.
312,000 kutoa 307,000!?
Kama serekali inawajali wanyonge wanaotumia usafiri wa uma, ingeangalia namna nzuri ya kufidia hasara inayotokea ili wanyonge waendelee kupata huduma ya usafiri.
Vinginevyo daladala zitashindwa kujiendesha na zote zitapaki"
Sent using Redmi Y2