Tetesi: Marufuku ya kuzidisha abiria ili kupambana na Corona, Daladala zimeanza kugoma Dar es Salaam

Tetesi: Marufuku ya kuzidisha abiria ili kupambana na Corona, Daladala zimeanza kugoma Dar es Salaam

Poleni sana...

Serikali kupunguza bei za mafuta ni kitu ambacho siyo rahisi, sababu bei elekezi zote hutegemea soko la dunia...

Kwenye hiki kipindi cha hili janga serikali yenyewe ipo kwenye maumivu makubwa ya kiuchumi, kwa hiyo lazima ichukue maamuzi magumu...

Kheri hata movement zinaruhusiwa na hicho kidogo kinapatikana huku afya za watu zingizingatiwa...

Hasara roho pesa makaratasi...

Cc: mahondaw
 
Wakuu,

Serikali imepiga marufuku daladala kusimamisha na kujaza abiria, taratibu ambao haukuzoeleka sana haswa kwa jiji la Dar.

Mimi nikiwa mmoja wa wamiliki wa daladala hizi naishauri Serikali mambo machache haswa katika kipindi hiki cha mpito kwakuwa Serikali imesema daladala itakayosimamisha abiria itapigwa faini laki Tisa au gerezani miaka miwili ifanye hivi ili kubalance situation.

Mfano daladala ikitoka mbezi hadi Temeke umbali wa kilomita 37 Kila abiria analipa 600 na daladala moja inasiti za abiria 26 hadi 22 akifika temeke anakuwa anapata 15600tsh hadi 13200tsh ambapo kwa umbali huo gari inaweza kutumia lita 5 ambapo ambapo ni sawa na tsh 11000.

Sasa Kama gari hadi inafika Temeke imekusanya 15600 za nauli ukitoa mafuta 11000tsh inamaana daladala hi itabakiwa na 4600.

Sasa kwa namna hii je huyo dereva atapataje hesabu na posho yake ya kila siku, bado kuna zile pesa za kupigia kiwi za jamaa zetu wale aliosema mkuu ambapo kwa siku nzima huenda zikafika 10000 tena hizi huwa hazinaga ubishi lazima utatoa tu.

Ushauri wangu, Serikali ipunguze bei za mafuta kwa daladala zote ikiwezekana iwe na vituo vyake vya mafuta na maduka yake maalumu ya vipuri pia Serikali itafute muda ikae na wadau husika lakini sio kufanya maamuzi bila kushirikiana na wadau watakaoteseka ni wananchi wakawaida wanategemea magari haya.
Mbona hujawahesabu abiria wanaopanda na kushuka njiani? Ambao kimsingi ni wengi zaidi kuliko wanaoanza safari hadi mwisho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kibiashara hailipi, lakini kiafya pia haifai, tunafanyaje hapa mkuu?
Labda serikali iongeze mabasi, kusolve hilo tatzo maana yaliyopo hayatoshi.. Wanaotumia usafiri wa umma ni wengi sana. Mfano mzuri tu angalia mabasi ya g/mboto na mbagala mida ya jion yanavyojaza af uwaambie watu wakae level seat si wengine watajikuta wapo kituoni had usiku wa manane.
 
Nadhani solution ni kupandisha bei ya usafiri kwa muda ili watu waanze kukaa ndani kama hawana shughuli za msingi.. mtu mwenye kitu cha maana ndio asafiri kwa daladala.

Ndio maana Mu7 alisema "huna gari private unaenda mjini kufanya nini? Baki ndani usije kufa bure.."
 
Tujikumbushe kitu..

Tukirudi nyuma kuanzia mwaka wa 2005 serikali ilikuwa ikipiga marufuku daladala kujaza,nakumbuka wakat huo traffic akiwakamata wamejaza faini inawahusu..

Sasa turudi

Kwani sheria ilibadirika lini?
Tuelewe ya kwamba wafanyabiashara huwa wana tabia zao kubwa..
Nazo ni hizi

Kupandisha bei wakat demand ikiwa juu..
Na pia huilazimisha serikali kufata matakwa yao kwa kutumia njia ya kutotoa huduma..

Tufaham ya kwamba,kinachotafutwa ni faida kubwa wala asije mtu akasema hawapat faida..
Siku zote mfanyabiashara anataka faida kubwa,hatak faida ndogo na huduma bora..
 
Serikali iuze ndege tatu inunue mabasi ya kutoa huduma ya level seat....... Serikali hii ya kilaghai
 
Muda umefika sasa kwa Dar kuondoa Coaster kama ilivyokuwa kwa Hiace miaka ya nyuma. Coaster ziishie Mbagala, Mbezi, Pugu, Tegeta n.k
Wamiliki waamrishwe kununua gari kubwa zenye siti ambazo zitabeba abiria wa kutosha. Foleni nyingine tunazitaka wenyewe, mrundikano mwingine tunausababisha sisi, na hata kusambaa kwa baadhi ya magonjwa tunakusababisha.
TUBADILIKE.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuwa hali hii ni janga la dunia nzima ni wakati sasa wa kubadilisha na kupanga mikakati yanayosaidia pande zote
Msaada wa serikali kwa sasa ni muhimu sana
Magari yote ya usafiri yaondolewe VAT kwa mafuta na ushuru mwingine kwa muda wa mpito mpaka june hivi
Watu kujazana ni hatari sana kwa maambukizo lazima lizingatiwe
Mishemishe ipungue sana na hata traffic wanaosimisha kwa kubrashi waache kwa muda wa mwezi tu au mnaonaje
Afya zetu ni bora kuliko hizo hela

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
KUPANDA KWA LEVEL SEAT SAWA,ILA NAULI ZA DALADALA ZIWE SHS 700 KITUO HADI KITUO.HALAFU POLICE WAKAMATE GARI HATA KAMA AMESIMAMISHWA MTU MMOJA."NAULI IKIWA JUU,WATU WATAPUNGUZA SAFARI ZISIZOKUWA ZA LAZIMA".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu,

Serikali imepiga marufuku daladala kusimamisha na kujaza abiria, taratibu ambao haukuzoeleka sana haswa kwa jiji la Dar.

Mimi nikiwa mmoja wa wamiliki wa daladala hizi naishauri Serikali mambo machache haswa katika kipindi hiki cha mpito kwakuwa Serikali imesema daladala itakayosimamisha abiria itapigwa faini laki Tisa au gerezani miaka miwili ifanye hivi ili kubalance situation.

Mfano daladala ikitoka mbezi hadi Temeke umbali wa kilomita 37 Kila abiria analipa 600 na daladala moja inasiti za abiria 26 hadi 22 akifika temeke anakuwa anapata 15600tsh hadi 13200tsh ambapo kwa umbali huo gari inaweza kutumia lita 5 ambapo ambapo ni sawa na tsh 11000.

Sasa Kama gari hadi inafika Temeke imekusanya 15600 za nauli ukitoa mafuta 11000tsh inamaana daladala hi itabakiwa na 4600.

Sasa kwa namna hii je huyo dereva atapataje hesabu na posho yake ya kila siku, bado kuna zile pesa za kupigia kiwi za jamaa zetu wale aliosema mkuu ambapo kwa siku nzima huenda zikafika 10000 tena hizi huwa hazinaga ubishi lazima utatoa tu.

Ushauri wangu, Serikali ipunguze bei za mafuta kwa daladala zote ikiwezekana iwe na vituo vyake vya mafuta na maduka yake maalumu ya vipuri pia Serikali itafute muda ikae na wadau husika lakini sio kufanya maamuzi bila kushirikiana na wadau watakaoteseka ni wananchi wakawaida wanategemea magari haya.

Kwa huu mchanganuo wako sidhani kama biashara ya daladala inalipa, Ila kwa uhalisia kiti kimoja cha daladala huwa kinakaliwa na mtu zaidi ya mmoja!!
 
Kweli kabisa.Nauli iongezwe kidogo kutoka 400 Hadi 600.Gari itakayosimamisha abiria,Hata akipigwa adhabu 30,000 TU,Hawatathubutu kusimamisha mtu.PIA ABIRIA AKIKAMATWA KASIMAMA NDANI YA DALA, ADHABU 10,000,Na Police wawe very strict kwa watakaokamatwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom