Marufuku ya Makonda kwenda US, UK, Australia & Canada

Marufuku ya Makonda kwenda US, UK, Australia & Canada

Ndugu yangu, hapo unawadanganye watu. Siyo automatic. Ban yake itaendelra kubakia na inaweza kuongezewa nguvu kama akiteuliwa kuwa waziri.
Kuna vitu mtu ukiwa hujui, ukisikia usichojua, unadhani ni uongo!.
Nakuhakikishia licha ya US travel ban, Konda Boy anaweza kutimba US kuhudhuria UNGA!.
P
 
Nani mwenye uwezo wa kuihoji Marekani?

Marekani wanamlia timing Rais wa Venezuela Maduro wamkamate wakamfunge Marekani.

Venezuela imezingirwa na majeshi ya Marekani.

Hivi mnaandikaga kujifurahisha au mnaelewa uhalisia wa mambo?

Aliyejitowa WHO ni nani? Mahakama ya The Hague?
Pamoja na nchi yake kuwekewa vikwazo na yeye kupigwa Marufuku ya kuingia Marekani lakini uliwahi kushuhudia the late Mugabe aliwahi kushindwa au kuzuiliwa kuingia New York kuhudhuria Mikutano ya Umoja wa Mataifa?
The way ulivyoandika kishabiki it seems like huna uelewa na International Laws na umeegemea zaidi katika story za vijiweni zile za kuamini Rambo anaweza akapiga mtaa mzima na kuamini Arnold ni Commando wa Jeshi la Marekani.
Kujitoa WHO na hizo Mahakama za Kimataifa kama ICC na ICJ hata Tanzania ama Taifa lolote linaweza likafanya hivyo pia. Kwahiyo sio jambo la ajabu kuamua kutokuwa mwanachama huko.
Huenda sio mfuatiliaji mzuri wa siasa za kimataifa, hebu kumbuka hata nchi za Africa ziliwahi kutishia kufanya hivyo baada ya kuona zimekuwa zikitumika kama tools za kukandamiza maslahi ya Africa (Rejea bugdha walizokutana nazo viongozi wa Kenya juu ya machafuko ya vurugu za kisiasa za mwaka 2007).
Hakuna nchi ambayo inakuwa obliged to be a member of certain IGOs, nchi hujiunga na kujitoa voluntarily (rejea URT kujitoa COMMESA)
Na nchi ambayo si mwanachama hawezi kuwa binded ama kuwajibishwa kwa kutofuata rules na regulations za certain IOs/IGOs.
 
Not true. Visa yeyote ile inatolewa kwa utashi wa mamlaka ya nchi husika. Wanaweza kukunyima kabisaa mazima bila hata ya kukupa sababu. Pia wanaweza kukunyima leo lakini kesho wakakupa. Na wanaweza wakakupa lakini ukiingia tu ndani ya nchi yao bado wakakukataa na kukurudisha ukiwa hapohapo airport kwasababu zozote wanazozijua wao. Ndo hivyo yaani.
Mkuu jiongezee uelewa kidogo juu ya International Laws na global politics, itakusaidia kujua kila general rule huwa ina exceptions zake.
Hata hiyo US kuna maeneo yapo ndani ya US lakini hayapo under the control of 100% of the US government.
Ukijua hilo wala hutaweza kubishana juu uwezo wa kuingia US kwa mtu ambaye ana zuio la kuingia katika nchi hiyo.
 
Ndugu yangu, hapo unawadanganye watu. Siyo automatic. Ban yake itaendelra kubakia na inaweza kuongezewa nguvu kama akiteuliwa kuwa waziri.
Makosa anayotuhumiwa ni ya jinai(kudhulumu maisha)
Au Jinai marekani ina duration?
USA wafanye tu mpango file la makonda waliachie mtandaoni tuone kama anayem protect atawazuia wazee wa fitna 🤣🤣
 
Mkuu jiongezee uelewa kidogo juu ya International Laws na global politics, itakusaidia kujua kila general rule huwa ina exceptions zake.
Hata hiyo US kuna maeneo yapo ndani ya US lakini hayapo under the control of 100% of the US government.
Ukijua hilo wala hutaweza kubishana juu uwezo wa kuingia US kwa mtu ambaye ana zuio la kuingia katika nchi hiyo.
You are misinformed Mkuu. Unajua lakini kwamba rais wa Palestina na wana diplomasia wake wametangazwa kunyimwa visa ya kuingia US kuhudhuria mkutano wa UN siku chache zilizopita tu? Pitia hii link:https://www.reuters.com/world/middl...er-abbas-un-allies-back-statehood-2025-08-29/
 
Tusiongee Sana,! Tusubiri uwajibikaji ndio utatoa majibu ya safari au kilimanjaro!
 
Kama anaenda kuwakilisha nchi Umoja wa.Mataifa kwenye kikao Cha mwaka anaruhusiwa kuingia Marekani kwa viza ya shughuli za Umoja wa Mataifa. Hii ni kwa nchi yeyote mwanachama wa UN. Akishaingia huko anaruhusiwa kukaa hotelini kwake na kwenye eneo la mkutano tu. Akimaliza shughuli, straight to Airport. Kote anakotembea lazima awe kwenye gari la kibalozi.
Mahmood Abbas kanyimwa visa maana Palestina sio nchi huru mwanachama wa Umoja wa Mataifa.
 
Kwa ile ban ya kutoingia US ni wazi sasa Mheshimiwa Mbunge na Waziri (Mtarajiwa) analazimika kuishia Zanzibar na Juba kutekeleza majukumu yake ya WIZARA YA MAMBO YA NJE.
Lakini kumbuka kwamba sisi Africa tunaweza kuishi bila kwenda au kuchukua kitu chochote cha Amerika tukaishi. Lakini Wao Amerika hawawezi kuishi bila kuja Africa au kujisogeza karibu na madini yetu wakaishi kwa furaha. They need us more than we need them. Angalia mfano wa Rais wa Burkinafaso Ibrahim Traole yeye hana time kwenda Amerika anapiga tu kazi ndani kwake na anapendwa na wananchi wake.
 
Unaijua status ya Palestine kwenye UN? Does a Palestine a State? A Palestine is a member State of the United Nations?
Hizo ndo sababu wamenyimwa visa? Unajua maana ya visa? Be serious Mkuu. The questions you are posing are irrelevant. Hakuna sheria yeyote au mkataba wowote wa kimataifa unao dictate nchi yeyote kulazimika kukupa kibali cha kuingia kwenye nchi husika bila ridhaa na utashi wa nchi husika. Iran is a member state of the UN. Je unajua kwamba viongozi wake pia waliwahi kukataliwa kuingia US kuhudhuria mkutano wa UN? Pitia hii link: https://www.reuters.com/article/wor...-visa-to-attend-un-us-official-idUSKBN1Z605T/
 
Kwani hatukukubaliana kwamba Tanzania inaizidi USA na EU kwa "kila kitu"?Sasa kwa nini tulilie kwenda huko?
 
Back
Top Bottom