Maruhani au majini wanatoaje kw mwili mwa mtu?

Kwanza mkuu ukiachana na video za Youtube,ushawahi kushuhudia tukio la mtu aliyepandwa na jini?
Ndio,
kwenye Ngoma za Maruhani.
Wagangawachawi wanayapigia ngoma za maruhani.
Hivyo Binadamu wanaokaliwa na majini wanapoteza fahamu na kuanza kucheza na kuimba na kuzungumza bila wao kujitambua. Nimeona Live kabisa bila chenga, ngoma hizi zipo mikoa ya Pwani, Tanga Tabora, Sumbawanga nk.

Tena basi.
Nilishwawahi kushuhudia Katika Maombi ya Mchungaji Wachungaji.
Mojawapo ni kwa Mchungaji
Mwakasege huko Arusha na Daresalaam.
Baada ya kufanya maombi mazito kwa kumwomba Mungu. Watu waliokaliwa na Majini walipagawa na mapepo hayo na kuanza kupiga kelele za maumivu makali.
Tofauti na kule kwenye ngoma za Majini ambapo Maruhani yalikuwa yanacheza ngoma kwa fulaha sana, na kuimba na kuzungumza kwa mbwembwe nyingi.
Kwenye mikutano ya Mchungaji Mwakasega Majini yalikuwa yanahangaika kwa mateso na sauti za kulia,kulaumu na kuhuzunika.
Hadi Mchungaji aliposema kwa Sauti kubwa

" Enyi Pepo Wachafu Nawaamuru Katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti Ondokeni kwa hao Watu mliowakalia "

Hapo nikaona wote walio pandisha mapepo wanaanguka chini na kurudiwa na ufahamu wao.
Kila aliyeanguka akaanza kuhojiwa na kusema kilicho mtokea.
Zaidi kama upo Daresalaam, naomba Uhudhurie mkutano wa Mchungaji Mwakasege utakaofanyika Daresalaam katika viwanja vya Yanganyika (Pekas) kuanzia jumapili ya tarehe 08 / 10 /2017 hadi tarehe 15. Utaona jinsi mtu anavyopandisha Jini anavyokuwa. Anabadilika kabisa.
We Jaribu tu kwenda kwaajiri ya kufanya Utafiti,
usiwe na nia ya kusali, wala usiwaze unachowaza sasa, upe ubongo kazi ya kutafakari bila kuegemea kwenye Imani yoyote ile.
we nenda kachunguze tu ikiwezeka nenda na mwenzako ambaye hajawahi kuona mtu aliyepandisha Maruhani.

Halafu Lete Mrejesho.
 
kila mbinu utakayoijaribu haitofanikiwa, hata kama itakua na mafanikio hayatakua ya kudumu, na kwa bahati nzuri kama wenzangu walivyosema kua ukombozi upo kwa Yesu kristu peke yake, hence there is no any other way out
 


Mkuu umesema hayaonekani hayo MAJINI.

Lakini historia inaonyesha kuna wakati Majini haya yalishea maisha na wanadamu na vile vile yalifungwa gerezani na hao.

JE BINADAMU aliwezaje kumkamata jini na kumfunga gerezani?
 
Jina la yesu Kristo tu linatosha kufukuza majini.
Yesu mwenyewe alisema Mtu yeyote akiwa na imani kidogo hata kama punje ya haradali anaweza kuamulu mlima ung'oke ukajitupe baharini.
Sasa tafasiri ya mlima si mlima kama meru ama kitonga mlima unaodhungumzwa ni matatizo.
 
Mkuu umesema hayaonekani hayo MAJINI.

Lakini historia inaonyesha kuna wakati Majini haya yalishea maisha na wanadamu na vile vile yalifungwa gerezani na hao.

JE BINADAMU aliwezaje kumkamata jini na kumfunga gerezani?
Ujue watu wanachanganya.
Kuna Historia na Hadithi

Hadithi ni Stori za kutunga kama zile za Adili na Nduguze, Bulicheka nk.

Historia ni Habari za kweli zilizotokea zamani. Mfano, Uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961.

Nadhani hii unayosema wewe ya Binadamu kuishi na kushirikiana na Majini na kuonana kwa macho ya mtu ya nyama, ni Hadithi tu za kutunga.

Nina uhakika wewe na mimi hatujawahi kumwona Jini uso kwa uso. Hata umbile la Jini au Ruhani hatulijui.
Aliyeliona Jini basi aje atueleze lipoje.

Hakuna Historia, wala Habari ya kweli inayosema Binadamu alishirikiana na Jini na kuonana ana kwa ana, uso kwa uso, na kufanya kazi zinazoonekana kama, Kulima, Kuvua, Kujenga nk.
Kama Historia hiyo ipo mahali basi anayeijua atuoneshe ni kitabu gani cha Kitaaluma au Kihistoria kimeandika habari hiyo.
Jini lipo katika hali ya Roho, tena ni Roho Mbaya, Chafu, yenye Uovu wote.
Unaosikia wanashirikiana na Majini ni hao Wagangawachawi, na wanashirikiana kiroho tu.
Yaani wanamwomba Shetani ili waingiwe na Majini kwenye mwili wao, Majini hayo yanawawezesha kufanya mambo mabaya kama, Kuroga, watu, Kuagua, Kutapeli watu, Kuiba, Kuua nk.

Ndio hivyo Mkuu.
 
Niende nikachunguze nini mkuu? kutolewa kwa majini kwenye miili ya watu?
 
Mkuu wewe habari za majini umezipata wapi? maana isije ikawa wewe ndio unaeleza vitu ambavyo sio vya kweli.
 
Mkuu wewe habari za majini umezipata wapi? maana isije ikawa wewe ndio vitu ambavyo sio vya kweli.
Nenda ktk Youtube, tafuta Video clips za Alhaji Yahaya Hessein, yenye kichwa cha habari.

Je majini yanatolewaje ndani ya mtu ?

Isikilize kwa umakini mkubwa
Utapata majibu yanayofanana na uliyojibiwa.
Kwenye video nyingine za huyo Mtaalamu wa Elimu ya Majini, utapata majibu ya maswali yako mengine uliyonayo.
 
Mkuu unataka kusema kwamba hizi habari za majini unazoeleza hapa umezitoa kwa Sheikh Yahya?
 
Mafuta au mti siyo kitu kwa roho. Ni sawa na ule usemi eti majini hawapendi nguruwe! Si kweli ni magirini tu. Anawezaje kutopenda nguruwe halafu akae chooni? Imani thabiti na uelewa wa mtu juu ya elimu ya kumjua Mungu wa Kweli ndiyo kinga pekee ya kudhibiti roho haribifu
 
Kama upo dar mcheki huyu mganga,, anaitwa mungu wa kabili 0744 000 473. Number hiyo apo
Huyu mganga nii hatari kwa maisha ya binadamu mbele za mola wetu mlezii,..

Kwa visaa nilivyovisikia kutoka kwakee kifo chake ni halali yetu anawapotosha watu kwenye njiaa iliyoonyooka ya mungu muumba wa kila kituu..

Ushauri tumwamini mola wetuu, tumuabudu na tumuombe hifadh ivii viumbe vingine vinatutengenezea mazingira mabaya sikuu tutaonana mungu muumba wa ulimwengu.
 
Duh ameshakufa unamaanisha? Alikufaje
 
Hapo umemjibu vyema kabisa! Labda kama atataka mabishano lakini akitaka kuelewa na kujifunza, maelezo yamejitosheleza sana. Ubarikiwe mtumishi.
 
umeongea vizuri, ila kuna mambo sikubaliani na wewe.

majini-ruhani wanatofautiana uwezo kama sisi binadamu hivyo kuna waganga (wa kweli) wasio na ushirika na wachawi wanaweza yaondoa majini.
Hakuna mganga wa kienyeji anayeweza kutoa roho chafu, sababu hana mamlaka hayo kwa maana mganga wa kienyeji hutumia miti shamba na wakati mwingine vitabu vya kichawi kwa mwongozo wa mizimu, majini, mashetani ambao kwa kifupi ni haohao tu tofauti majina. Awe jini, ruhani, pepo, mzimu, shetani, mzuka vibwengo nk, wote ni kitu kimoja tu. Hakunaga jini mzuri roho chafu ni chafu tu nia ni kuharibu.
 
Naam, ndivyo ilivyo
 
Ok mkuu kabla hata ya kwenda kuangali hiyo video nimeona bora niishie tu hapa huu mjadala maana maelezo yako yamechanganya mambo mengi,umechanganya matatizo ya uchawi na matatizo ya kuingiwa na jini tu.

Uelewa wetu kuhusu majini unatofautiana sana.
Kutofautiana kwa uelewa kati ya mtu na mtu hutokana na mafundisho au mtazamo juu ya elimu kuhusu mambo haya. Wapo waliofundishwa kuwa kuna majini wazuri na wabaya. Lakini ukiangalia chanzo cha hao majini mpaka kuitwa majini ilitokana na uasi wao huko mbinguni, kabla hawajawa majini walikuwa ni malaika tena watakatifu.
 
Unatoa majibu mazuri sana, asiyeelewa ufahamu wake utakuwa umetiwa giza, na anayebisha kuna interest zake binafsi
 
kwa imani yako uko sahihi, ila kwa ukweli halisi hauko sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…