Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Ndio,Kwanza mkuu ukiachana na video za Youtube,ushawahi kushuhudia tukio la mtu aliyepandwa na jini?
kwenye Ngoma za Maruhani.
Wagangawachawi wanayapigia ngoma za maruhani.
Hivyo Binadamu wanaokaliwa na majini wanapoteza fahamu na kuanza kucheza na kuimba na kuzungumza bila wao kujitambua. Nimeona Live kabisa bila chenga, ngoma hizi zipo mikoa ya Pwani, Tanga Tabora, Sumbawanga nk.
Tena basi.
Nilishwawahi kushuhudia Katika Maombi ya Mchungaji Wachungaji.
Mojawapo ni kwa Mchungaji
Mwakasege huko Arusha na Daresalaam.
Baada ya kufanya maombi mazito kwa kumwomba Mungu. Watu waliokaliwa na Majini walipagawa na mapepo hayo na kuanza kupiga kelele za maumivu makali.
Tofauti na kule kwenye ngoma za Majini ambapo Maruhani yalikuwa yanacheza ngoma kwa fulaha sana, na kuimba na kuzungumza kwa mbwembwe nyingi.
Kwenye mikutano ya Mchungaji Mwakasega Majini yalikuwa yanahangaika kwa mateso na sauti za kulia,kulaumu na kuhuzunika.
Hadi Mchungaji aliposema kwa Sauti kubwa
" Enyi Pepo Wachafu Nawaamuru Katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti Ondokeni kwa hao Watu mliowakalia "
Hapo nikaona wote walio pandisha mapepo wanaanguka chini na kurudiwa na ufahamu wao.
Kila aliyeanguka akaanza kuhojiwa na kusema kilicho mtokea.
Zaidi kama upo Daresalaam, naomba Uhudhurie mkutano wa Mchungaji Mwakasege utakaofanyika Daresalaam katika viwanja vya Yanganyika (Pekas) kuanzia jumapili ya tarehe 08 / 10 /2017 hadi tarehe 15. Utaona jinsi mtu anavyopandisha Jini anavyokuwa. Anabadilika kabisa.
We Jaribu tu kwenda kwaajiri ya kufanya Utafiti,
usiwe na nia ya kusali, wala usiwaze unachowaza sasa, upe ubongo kazi ya kutafakari bila kuegemea kwenye Imani yoyote ile.
we nenda kachunguze tu ikiwezeka nenda na mwenzako ambaye hajawahi kuona mtu aliyepandisha Maruhani.
Halafu Lete Mrejesho.