Maruhani au majini wanatoaje kw mwili mwa mtu?

Kwanza mkuu ukiachana na video za Youtube,ushawahi kushuhudia tukio la mtu aliyepandwa na jini?
Ndio,
kwenye Ngoma za Maruhani.
Wagangawachawi wanayapigia ngoma za maruhani.
Hivyo Binadamu wanaokaliwa na majini wanapoteza fahamu na kuanza kucheza na kuimba na kuzungumza bila wao kujitambua. Nimeona Live kabisa bila chenga, ngoma hizi zipo mikoa ya Pwani, Tanga Tabora, Sumbawanga nk.

Tena basi.
Nilishwawahi kushuhudia Katika Maombi ya Mchungaji Wachungaji.
Mojawapo ni kwa Mchungaji
Mwakasege huko Arusha na Daresalaam.
Baada ya kufanya maombi mazito kwa kumwomba Mungu. Watu waliokaliwa na Majini walipagawa na mapepo hayo na kuanza kupiga kelele za maumivu makali.
Tofauti na kule kwenye ngoma za Majini ambapo Maruhani yalikuwa yanacheza ngoma kwa fulaha sana, na kuimba na kuzungumza kwa mbwembwe nyingi.
Kwenye mikutano ya Mchungaji Mwakasega Majini yalikuwa yanahangaika kwa mateso na sauti za kulia,kulaumu na kuhuzunika.
Hadi Mchungaji aliposema kwa Sauti kubwa

" Enyi Pepo Wachafu Nawaamuru Katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti Ondokeni kwa hao Watu mliowakalia "

Hapo nikaona wote walio pandisha mapepo wanaanguka chini na kurudiwa na ufahamu wao.
Kila aliyeanguka akaanza kuhojiwa na kusema kilicho mtokea.
Zaidi kama upo Daresalaam, naomba Uhudhurie mkutano wa Mchungaji Mwakasege utakaofanyika Daresalaam katika viwanja vya Yanganyika (Pekas) kuanzia jumapili ya tarehe 08 / 10 /2017 hadi tarehe 15. Utaona jinsi mtu anavyopandisha Jini anavyokuwa. Anabadilika kabisa.
We Jaribu tu kwenda kwaajiri ya kufanya Utafiti,
usiwe na nia ya kusali, wala usiwaze unachowaza sasa, upe ubongo kazi ya kutafakari bila kuegemea kwenye Imani yoyote ile.
we nenda kachunguze tu ikiwezeka nenda na mwenzako ambaye hajawahi kuona mtu aliyepandisha Maruhani.

Halafu Lete Mrejesho.
 
kila mbinu utakayoijaribu haitofanikiwa, hata kama itakua na mafanikio hayatakua ya kudumu, na kwa bahati nzuri kama wenzangu walivyosema kua ukombozi upo kwa Yesu kristu peke yake, hence there is no any other way out
 
Asante, sasa nakujibu.

Kwanza ujue Jini au Ruhani hayaonekani kwa macho, kwakuwa ni roho.
Pia ujue hakuna Jini au Ruhani ambalo likimwingia mtu litamnufaisha, yote yana nia mbaya ya kumharibu Binadamu.
Namaanisha hakuna Jini jema kwenye uhusiano na Mwanadamu.
Mtu mwenye Majini utamtambua kwa mabadiliko katika hali yake tu, na kama Jini likimtoka basi binadamu huyo hurudi ktk hali yake ya kawaida.
Hali gani hizo ?

1. Tabia- Jini lina mfanya mtu awe na tabia zisizorekebishika kama, wizi, kujichua, utapeli, uzinzi, ulevi, ugomvi, nk. Vilivyopitiliza.

2. Magonjwa- Jini linasababisha magonjwa ambayo hayaonekani kwemye vipimo vya kisayansi. Unakuta mtu anadhohofika tu hata akila chakula bora na Dactari haoni ugonjwa wowote.
Vichaa wengi wanakaliwa na Majini. Ugonjwa wa kifafa mara nyingi unasababishwa na Majini.

3.Vifo- Jini linasababisha vifo kwa aliyenalo. Vifo vya ajali, kuanguka ghafla, kufa usingizini, unaweza kukuta familia moja inafiwa na watu kumi ndani ya mwaka mmoja au miwili, Vifo vya korogwa kama kwa Tego, au Kisomo, au Ndumba. Kumbuka mtu akikuroga kwa mgangamchawi analituma Jini lije kukutoa roho yako.

Hizi dalili tatu mojawapo zinazomtokea Binadamu mwenye Jini.

Hakuna namna ya kulitoa Jini zaidi ya kwenda kwa watumishi wa Mungu ambao ni waadilifu ili wakombee kwa Mungu ili Jini limtoke Binadamu.
Nimesema Watumishi wa Mungu waadilifu.

Mchawi au Mganga wa kienyeji katu hawezi kulitoa Jini.
Sababu moja ni kuwa kwanza hawezi kuliona, likitulia kimywa atakuambia limetoka, na linaweza kutulia hata miaka miwili au mitano.
Uli kujua kuwa Jini limemtoka mtu basi utaona zile dalili za mtu mwenye Jini zinaondoka kabisa kwa Binadamu huyo na kupotea.
Kama alikuwa mlevi kupindukia anarudi kuwa sio mlevi tena. nk.
Wazazi wengi hawaelewi kuhusu tabia za ajabu za vijana wao na kuanza kuwaadhibu hadi kukata tamaa, kumbe sababu ni kuwa vijana wao wameingiliwa na Majini ambayo yanamfanya Kijana ashindwe kuacha tabia zake mbaya.
Kwaleo naona niishie hapa kama unaswali lingine niulize tu, ila iwe kwa kutaka kuelewa na sio kubishana.

Zaidi ukitaka kuthibitisha hayo niliyokuambia, weka bando la kutosha katika simu yako, ukishapata mtandao wa 4G bofya ktk internet, tafuta sehemu ya Youtube video halafu andika neno

" Scoan Spirit Deriverence"

Utaona video za baadhi ya mambo niliyokueleza.
Asante sana,
kwa kunivumilia.

Mkuu umesema hayaonekani hayo MAJINI.

Lakini historia inaonyesha kuna wakati Majini haya yalishea maisha na wanadamu na vile vile yalifungwa gerezani na hao.

JE BINADAMU aliwezaje kumkamata jini na kumfunga gerezani?
 
Jina la yesu Kristo tu linatosha kufukuza majini.
Yesu mwenyewe alisema Mtu yeyote akiwa na imani kidogo hata kama punje ya haradali anaweza kuamulu mlima ung'oke ukajitupe baharini.
Sasa tafasiri ya mlima si mlima kama meru ama kitonga mlima unaodhungumzwa ni matatizo.
 
Mkuu umesema hayaonekani hayo MAJINI.

Lakini historia inaonyesha kuna wakati Majini haya yalishea maisha na wanadamu na vile vile yalifungwa gerezani na hao.

JE BINADAMU aliwezaje kumkamata jini na kumfunga gerezani?
Ujue watu wanachanganya.
Kuna Historia na Hadithi

Hadithi ni Stori za kutunga kama zile za Adili na Nduguze, Bulicheka nk.

Historia ni Habari za kweli zilizotokea zamani. Mfano, Uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961.

Nadhani hii unayosema wewe ya Binadamu kuishi na kushirikiana na Majini na kuonana kwa macho ya mtu ya nyama, ni Hadithi tu za kutunga.

Nina uhakika wewe na mimi hatujawahi kumwona Jini uso kwa uso. Hata umbile la Jini au Ruhani hatulijui.
Aliyeliona Jini basi aje atueleze lipoje.

Hakuna Historia, wala Habari ya kweli inayosema Binadamu alishirikiana na Jini na kuonana ana kwa ana, uso kwa uso, na kufanya kazi zinazoonekana kama, Kulima, Kuvua, Kujenga nk.
Kama Historia hiyo ipo mahali basi anayeijua atuoneshe ni kitabu gani cha Kitaaluma au Kihistoria kimeandika habari hiyo.
Jini lipo katika hali ya Roho, tena ni Roho Mbaya, Chafu, yenye Uovu wote.
Unaosikia wanashirikiana na Majini ni hao Wagangawachawi, na wanashirikiana kiroho tu.
Yaani wanamwomba Shetani ili waingiwe na Majini kwenye mwili wao, Majini hayo yanawawezesha kufanya mambo mabaya kama, Kuroga, watu, Kuagua, Kutapeli watu, Kuiba, Kuua nk.

Ndio hivyo Mkuu.
 
Ndio,
kwenye Ngoma za Maruhani.
Wagangawachawi wanayapigia ngoma za maruhani.
Hivyo Binadamu wanaokaliwa na majini wanapoteza fahamu na kuanza kucheza na kuimba na kuzungumza bila wao kujitambua. Nimeona Live kabisa bila chenga, ngoma hizi zipo mikoa ya Pwani, Tanga Tabora, Sumbawanga nk.

Tena basi.
Nilishwawahi kushuhudia Katika Maombi ya Mchungaji Wachungaji.
Mojawapo ni kwa Mchungaji
Mwakasege huko Arusha na Daresalaam.
Baada ya kufanya maombi mazito kwa kumwomba Mungu. Watu waliokaliwa na Majini walipagawa na mapepo hayo na kuanza kupiga kelele za maumivu makali.
Tofauti na kule kwenye ngoma za Majini ambapo Maruhani yalikuwa yanacheza ngoma kwa fulaha sana, na kuimba na kuzungumza kwa mbwembwe nyingi.
Kwenye mikutano ya Mchungaji Mwakasega Majini yalikuwa yanahangaika kwa mateso na sauti za kulia,kulaumu na kuhuzunika.
Hadi Mchungaji aliposema kwa Sauti kubwa

" Enyi Pepo Wachafu Nawaamuru Katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti Ondokeni kwa hao Watu mliowakalia "

Hapo nikaona wote walio pandisha mapepo wanaanguka chini na kurudiwa na ufahamu wao.
Kila aliyeanguka akaanza kuhojiwa na kusema kilicho mtokea.
Zaidi kama upo Daresalaam, naomba Uhudhurie mkutano wa Mchungaji Mwakasege utakaofanyika Daresalaam katika viwanja vya Yanganyika (Pekas) kuanzia jumapili ya tarehe 08 / 10 /2017 hadi tarehe 15. Utaona jinsi mtu anavyopandisha Jini anavyokuwa. Anabadilika kabisa.
We Jaribu tu kwenda kwaajiri ya kufanya Utafiti,
usiwe na nia ya kusali, wala usiwaze unachowaza sasa, upe ubongo kazi ya kutafakari bila kuegemea kwenye Imani yoyote ile.
we nenda kachunguze tu ikiwezeka nenda na mwenzako ambaye hajawahi kuona mtu aliyepandisha Maruhani.

Halafu Lete Mrejesho.
Niende nikachunguze nini mkuu? kutolewa kwa majini kwenye miili ya watu?
 
Ujue watu wanachanganya.
Kuna Historia na Hadithi

Hadithi ni Stori za kutunga kama zile za Adili na Nduguze, Bulicheka nk.

Historia ni Habari za kweli zilizotokea zamani. Mfano, Uhuru wa Tanganyika wa mwaka 1961.

Nadhani hii unayosema wewe ya Binadamu kuishi na kushirikiana na Majini na kuonana kwa macho ya mtu ya nyama, ni Hadithi tu za kutunga.

Nina uhakika wewe na mimi hatujawahi kumwona Jini uso kwa uso. Hata umbile la Jini au Ruhani hatulijui.
Aliyeliona Jini basi aje atueleze lipoje.

Hakuna Historia, wala Habari ya kweli inayosema Binadamu alishirikiana na Jini na kuonana ana kwa ana, uso kwa uso, na kufanya kazi zinazoonekana kama, Kulima, Kuvua, Kujenga nk.
Kama Historia hiyo ipo mahali basi anayeijua atuoneshe ni kitabu gani cha Kitaaluma au Kihistoria kimeandika habari hiyo.
Jini lipo katika hali ya Roho, tena ni Roho Mbaya, Chafu, yenye Uovu wote.
Unaosikia wanashirikiana na Majini ni hao Wagangawachawi, na wanashirikiana kiroho tu.
Yaani wanamwomba Shetani ili waingiwe na Majini kwenye mwili wao, Majini hayo yanawawezesha kufanya mambo mabaya kama, Kuroga, watu, Kuagua, Kutapeli watu, Kuiba, Kuua nk.

Ndio hivyo Mkuu.
Mkuu wewe habari za majini umezipata wapi? maana isije ikawa wewe ndio unaeleza vitu ambavyo sio vya kweli.
 
Mkuu wewe habari za majini umezipata wapi? maana isije ikawa wewe ndio vitu ambavyo sio vya kweli.
Nenda ktk Youtube, tafuta Video clips za Alhaji Yahaya Hessein, yenye kichwa cha habari.

Je majini yanatolewaje ndani ya mtu ?

Isikilize kwa umakini mkubwa
Utapata majibu yanayofanana na uliyojibiwa.
Kwenye video nyingine za huyo Mtaalamu wa Elimu ya Majini, utapata majibu ya maswali yako mengine uliyonayo.
 
Mkuu unataka kusema kwamba hizi habari za majini unazoeleza hapa umezitoa kwa Sheikh Yahya?
 
Huyo ilibidi asomewe ruqya,

Apende sana kudumu na udhuu maana mtume amesema ni ngao Moja wapo dhidi ya hao viumbe

Asisikilize wala kutazama vitu vilivyokatazwa aidha mzikii auu madude mengine ambayo siyoo mazurii..

Apende kusoma quranii, yaani akijikita kusoma qurani yaani anawajengea mazingira mabaya hao madudu

Kama kunauwezekano apate mafuta halisi ya mzaituni awe anapakaaa maaana ataaa shetanii aweee amejisahau vipiii hawezi kupumzika kwenye mtii huoo.
Mafuta au mti siyo kitu kwa roho. Ni sawa na ule usemi eti majini hawapendi nguruwe! Si kweli ni magirini tu. Anawezaje kutopenda nguruwe halafu akae chooni? Imani thabiti na uelewa wa mtu juu ya elimu ya kumjua Mungu wa Kweli ndiyo kinga pekee ya kudhibiti roho haribifu
 
Kama upo dar mcheki huyu mganga,, anaitwa mungu wa kabili 0744 000 473. Number hiyo apo
Huyu mganga nii hatari kwa maisha ya binadamu mbele za mola wetu mlezii,..

Kwa visaa nilivyovisikia kutoka kwakee kifo chake ni halali yetu anawapotosha watu kwenye njiaa iliyoonyooka ya mungu muumba wa kila kituu..

Ushauri tumwamini mola wetuu, tumuabudu na tumuombe hifadh ivii viumbe vingine vinatutengenezea mazingira mabaya sikuu tutaonana mungu muumba wa ulimwengu.
 
Duh ameshakufa unamaanisha? Alikufaje
 
Asante, sasa nakujibu.

Kwanza ujue Jini au Ruhani hayaonekani kwa macho, kwakuwa ni roho.
Pia ujue hakuna Jini au Ruhani ambalo likimwingia mtu litamnufaisha, yote yana nia mbaya ya kumharibu Binadamu.
Namaanisha hakuna Jini jema kwenye uhusiano na Mwanadamu.
Mtu mwenye Majini utamtambua kwa mabadiliko katika hali yake tu, na kama Jini likimtoka basi binadamu huyo hurudi ktk hali yake ya kawaida.
Hali gani hizo ?

1. Tabia- Jini lina mfanya mtu awe na tabia zisizorekebishika kama, wizi, kujichua, utapeli, uzinzi, ulevi, ugomvi, nk. Vilivyopitiliza.

2. Magonjwa- Jini linasababisha magonjwa ambayo hayaonekani kwemye vipimo vya kisayansi. Unakuta mtu anadhohofika tu hata akila chakula bora na Dactari haoni ugonjwa wowote.
Vichaa wengi wanakaliwa na Majini. Ugonjwa wa kifafa mara nyingi unasababishwa na Majini.

3.Vifo- Jini linasababisha vifo kwa aliyenalo. Vifo vya ajali, kuanguka ghafla, kufa usingizini, unaweza kukuta familia moja inafiwa na watu kumi ndani ya mwaka mmoja au miwili, Vifo vya korogwa kama kwa Tego, au Kisomo, au Ndumba. Kumbuka mtu akikuroga kwa mgangamchawi analituma Jini lije kukutoa roho yako.

Hizi dalili tatu mojawapo zinazomtokea Binadamu mwenye Jini.

Hakuna namna ya kulitoa Jini zaidi ya kwenda kwa watumishi wa Mungu ambao ni waadilifu ili wakombee kwa Mungu ili Jini limtoke Binadamu.
Nimesema Watumishi wa Mungu waadilifu.

Mchawi au Mganga wa kienyeji katu hawezi kulitoa Jini.
Sababu moja ni kuwa kwanza hawezi kuliona, likitulia kimywa atakuambia limetoka, na linaweza kutulia hata miaka miwili au mitano.
Uli kujua kuwa Jini limemtoka mtu basi utaona zile dalili za mtu mwenye Jini zinaondoka kabisa kwa Binadamu huyo na kupotea.
Kama alikuwa mlevi kupindukia anarudi kuwa sio mlevi tena. nk.
Wazazi wengi hawaelewi kuhusu tabia za ajabu za vijana wao na kuanza kuwaadhibu hadi kukata tamaa, kumbe sababu ni kuwa vijana wao wameingiliwa na Majini ambayo yanamfanya Kijana ashindwe kuacha tabia zake mbaya.
Kwaleo naona niishie hapa kama unaswali lingine niulize tu, ila iwe kwa kutaka kuelewa na sio kubishana.

Zaidi ukitaka kuthibitisha hayo niliyokuambia, weka bando la kutosha katika simu yako, ukishapata mtandao wa 4G bofya ktk internet, tafuta sehemu ya Youtube video halafu andika neno

" Scoan Spirit Deriverence"

Utaona video za baadhi ya mambo niliyokueleza.
Asante sana,
kwa kunivumilia.
Hapo umemjibu vyema kabisa! Labda kama atataka mabishano lakini akitaka kuelewa na kujifunza, maelezo yamejitosheleza sana. Ubarikiwe mtumishi.
 
umeongea vizuri, ila kuna mambo sikubaliani na wewe.

majini-ruhani wanatofautiana uwezo kama sisi binadamu hivyo kuna waganga (wa kweli) wasio na ushirika na wachawi wanaweza yaondoa majini.
Hakuna mganga wa kienyeji anayeweza kutoa roho chafu, sababu hana mamlaka hayo kwa maana mganga wa kienyeji hutumia miti shamba na wakati mwingine vitabu vya kichawi kwa mwongozo wa mizimu, majini, mashetani ambao kwa kifupi ni haohao tu tofauti majina. Awe jini, ruhani, pepo, mzimu, shetani, mzuka vibwengo nk, wote ni kitu kimoja tu. Hakunaga jini mzuri roho chafu ni chafu tu nia ni kuharibu.
 
Hao wote ni Pepo wachafu ambao wapo katika milki ya Shetani Lusifer.
Ila wanatofautiana kwa kuwa katika jamii mbalimbali.
Kuna Majini, Mizimu, Maruhani, Vibwengo, Vinyamkera, Vindondocha, Misukule, nk.
Hiyo midudu yote inatumikishwa na Shetani kwenye kazi zake za kumharibu mwanadamu na Kumkufuru Mungu.
Naam, ndivyo ilivyo
 
Ok mkuu kabla hata ya kwenda kuangali hiyo video nimeona bora niishie tu hapa huu mjadala maana maelezo yako yamechanganya mambo mengi,umechanganya matatizo ya uchawi na matatizo ya kuingiwa na jini tu.

Uelewa wetu kuhusu majini unatofautiana sana.
Kutofautiana kwa uelewa kati ya mtu na mtu hutokana na mafundisho au mtazamo juu ya elimu kuhusu mambo haya. Wapo waliofundishwa kuwa kuna majini wazuri na wabaya. Lakini ukiangalia chanzo cha hao majini mpaka kuitwa majini ilitokana na uasi wao huko mbinguni, kabla hawajawa majini walikuwa ni malaika tena watakatifu.
 
Nakanusha.
Kwanza lazima ujue, Majini, Maruhani yapo katika Ulimwengu wa Roho.
Ulimwengu wa Roho umegawanyika katika Falme mbili.
Ufalme wa Mbingu kwenye NURU ukiongozwa na Mungu, na Ufalme wa KUZIMU kwenye GIZA ukiongizwa na Shetani.
Falme hizi ndizo zinazoweza kushindana, kupigana vita na Falme moja kuishinda Falme nyingine.
Toka mwanzo Ufalme wa Mbingu una nguvu kuliko ufalme wa Kuzimu.

Ufalme wa Dunia hauna nguvu kwanye hizo falme mbili.

Ndio maana binadamu alipoumbwa, Mungu alimwamuru, atawale vilivyomo ndani ya nchi anavyoviona tu.

" Na tumfanye mtu kwa mfano wetu,...wakatawale...nchi yote pia" Mwanzo 1: 26-28.

Sasa mamlaka ya kutawala Ulimwengu wa Roho Binadamu alipewa na nani hadi aweze kulilazimisha Jini limtoke mtu ?

Ili aweze kutawala Ulimwengu wa Roho, ni lazima Binadamu aombe nguvu toka ama Ufalme wa Mungu au Ufalme wa Shetani.

Na Binadamu akiomba nguvu toka ufalme wa Shetani ili auharibu ufalme wa Shetani katu hawezi kupewa.
Mara nyingi Binadamu anaomba nguvu ufalme wa Shetani ili amharibu Binadamu kwani ndiye dhaifu kwake, ndo maana Binadamu anarogeka.

Ili kuuharibu Ufalme wa Shetani ni lazima Binadamu aombe nguvu toka Ufalme wa Mbingu kwani una nguvu kuliko Kuzimu.

Msidanganyike wandugu Mganga wa kienyeji huyo Binadamu kama wewe KATU hawezi kutoa Jini.
Jini linatolewa na Mungu pekee.
Na ametupa jina la Yesu Kristo wa Nazareti ili litumike kuondoa nuksi zote pamoja na Mapepo wachafu.

Nawasilisha.

Ili kuliondoa Pepo na liweze kukutiii ninlazima uombe nguvu toka katika ufalme wa Mbingu.

We jiulize tu Jini linaweza kukaa mdani ya Binanamu na kumtawala.

Ivi kwa nini Binadamu anashindwa kukaa ndani ya Jini na kulitawala ?
Wewe unaweza kukaa ndani ya Jini ?
Kama Binadamu anashindwa kukaa ndani ya Jini, atawezaje kwa kutumia nguvu zake binafsi kuliamrisha Jini litoke ndani ya Binadamu ?
Hao waganga wa kienyeji wanao sema wanauwezo wa kuliondoa Jina nao pia wanakaliwa na Majini, ndio maana unawaona mganga anajifanya anaondoa majini lakini hali yake ni maskini wa
kutupwa.
Eti utaskia Mganga anatumia Mizimu kuondoa majini. Yaani Dada amfukuze Shemeji.
Jini katu haliwezi kuliondoa Jini Mwenzake maana wapo Ufalme mmoja wa uhalibifu hawawezi kugombana, wala kuangushana.
Pale mgonjwa unazugwa tu ili utoe pesa yako na zaidi unaongezewa Majini mengine ili yapate pakukaa.
Kumbuka Baharini kuna baridi sana, Majini yanapenda sana kukaa ndani ya mtu ndio makazi Bora Zaidi kwao, na hayaondoki kirahisi hadi watolewe kwa nguvubna nguvu ya Mungu pekee.
Kamwe Jini halitoki kwa Muarubaini.
Unatoa majibu mazuri sana, asiyeelewa ufahamu wake utakuwa umetiwa giza, na anayebisha kuna interest zake binafsi
 
Hakuna mganga wa kienyeji anayeweza kutoa roho chafu, sababu hana mamlaka hayo kwa maana mganga wa kienyeji hutumia miti shamba na wakati mwingine vitabu vya kichawi kwa mwongozo wa mizimu, majini, mashetani ambao kwa kifupi ni haohao tu tofauti majina. Awe jini, ruhani, pepo, mzimu, shetani, mzuka vibwengo nk, wote ni kitu kimoja tu. Hakunaga jini mzuri roho chafu ni chafu tu nia ni kuharibu.
kwa imani yako uko sahihi, ila kwa ukweli halisi hauko sahihi
 
Back
Top Bottom