Maruhani au majini wanatoaje kw mwili mwa mtu?

Kuna watu wanazaliwa na matatizo na kuishi nayo maisha yao yoote! Kila wanapotafuta ufumbuzi wa tatizo wanatatuliwa kwa muda tu ila huendelea na matatizo yao mpaka wanayaacha haya makazi ya mwili wa damu na nyama. Ila suluhisho kamili lipo kwa Yeye ambaye ni Njia Kweli na Uzima.
 
Acha kudanganya watu jina la yesu limtoe shetani mwilini mwa Binadamu utakuwa unafikia kwa kutumia tumbo na si kichwa
 
Mi navyojua huyo malaika aliitwa shetani baada ya uasi na si jini,labda nikuulize kwanini aliitwa hivyo?
 
Kwa nyongeza tu ni hivi, hakuna lisilowezekana katika roho. Hata mchawi anao uwezo wa kujionesha kwa mtu wa kawaida akiwa katika hali yake ya kiroho giza na akamtisha sana mtu. Halikadhalika kwa majini, wanao uwezo wa kujionesha mbele ya mtu physically! Ila wanajionesha zaidi au maranyingi sana katika ulimwengu wa kiroho kuliko damu na nyama. Kama majini hapo kabla walikuwa watakatifu (malaika) kisha wakaasi na kuwa mashetani basi wanao uwezo wa kujionesha kwa wanadamu waziwazi. Ukisoma kitabu cha Mwanzo katika kisa cha Lutu (Sodoma na Gomora) au kitabu cha waamuzi wazazi wa Samsoni walimwona malaika physically, pia kitabu cha Joshua alipokutana na malaika wa jeshi la mbinguni uso kwa uso, mzee Yakobo (Israel) alipambana naye mapaka alfajiri na pia Petro akiwa gerezani alidhani anaona maono kumbe ilikuwa ni physically mpaka akakiri kuwa hayakuowa maono bali ni wazi wazi.
Nyongeza:-
Mungu ni tajiri saana! Karama zake hazina majuto, alipomfukuza shetani na wafuasi wake hakuwanyang'anya uwezo waliokuwa nao, ila, aliliondoa Jina Lake ambalo ni Nuru. Ndiyo maana shetani amefungwa katika kifungo cha giza (hajui kutenda lililo jema tangu hapo) mpaka siku ya mwisho iliyowekewa mhuri, anayeijua ni Mungu pekee.
 
Bado upo kiimani zaidi ila kiuhalisia haupo sahihi.

Na tatizo lenu ni moja pale mnaposema kwamba kuna nguvu aina mbili yani ya Mungu na ya shetani,haoa huwa mnakosea shetani nguvu kazitolea wapi?
 
Anaishi mkoa gani? Majini yanaondolewa kupitia Jina la Yesu tu, mbali na hapo ni kuyatuliza.
 
Shetani tafsiri yake ni muasi. Wewe unaelewaje?
Upo sawa,kwa hivyo utaona kuwa neno shetani ni kiumbe aliyeasi kwa maana hata binaadamu huweza kuwa shetani endapo atamuasi Mungu.

Ila tunapozungumzia jini huyu ni kiumbe mwengine hana sifa za malaika.
 
Anaishi mkoa gani? Majini yanaondolewa kupitia Jina la Yesu tu, mbali na hapo ni kuyatuliza.
Kwanini iwezekane kuyatuliza na ishindikane kuyaondoa? hivi kwa mfano yale maombezi ya makanisani kwa wenye majini,huwa tunaona watu wakianguka na baadaye kurudia katika hali zao za kawaida je,pale ndiyo huwa majini yameshatoka kwa jina la Yesu?
 
Dah mi nina ndugu yangu nimehangaika mwaka wa 4 nisijue la kufanya yani. Si hospitali, si kanisani si kwa sharif majini ila bado ndugu yangu anateseka.
Hali ilianza kipindi amejipanga kuoa tu, alikuwa na wasichana wawili anawatazamia achukue mmojawapo kilichokuja tokea katikati ya mchakato barua ya posa ikakataliwa, akaanza badilika mara anakuwa kama ana loose memory, baadae akaanza kuongea mwenyewe, ukiskiliza kinachoongelewa ni kama mtu anamlazimisha kuoa mwanamke mmoja kati ya wale wawili. Alikua na biashara anafanya vizuri sana ikavurugika akaibiwa vitu baadae akarudi nyumbani kabisa.

This is the 4th year analazimishwa kuoa tu na kitu ambacho nadhani ni hilo pepo. Zamani alikuwa halali anaongea usiku kucha sahizi walau kimetulia kidogo tulimpa ma anti-depressant mwaka mzima tukijua labda alipata depression baada ya kukataliwa barua ya posa. Well sasa ni dhahiri haikuwa depression bali ni jini. Nilimtafuta hadi yule mtu mzito ila haikufaa nilipoteza pesa tu, nmeenda vatcan sinza kwa yule mchungaji holaaa... nimeenda kwa sharif majini mabibo chenga yani anaeweza kunipa reference ya kutatua hili tatizo anisaidie.
 
Acha kudanganya watu jina la yesu limtoe shetani mwilini mwa Binadamu utakuwa unafikia kwa kutumia tumbo na si kichwa
Jamii Forum ni jukwaa la kuelimishana na kubadilishana mawazo.
Kama limetolewa wazo na halifanani na mawazo yako unaweza kileta mawazo yako ili na sisi tuelimike.
Kitendo cha kumdhihaki mtu au kumtukana kwakuwa tu hajasema kama unavyofikiri si kitemdo cha kistaarabu hata kidogo.
Na haiwezekani jukwaa hili likawa na watu wanaozungumza wazo moja tu ambalo linapendwa na msomaji.
Kama una elimu mbadala tueleze na sisi tujifunze toka kwako na sio una nukuu watu na unaishia kuwadhihaki bila sababu.
Heshima ni kitu cha bule ndugu, na kama hupendi wazo fulani na huna cha kusema sio vibaya ukakaa kimya.

Huna tabia nzuri na inakulazimu ujirekebishe.
 


Mkuu asante sana kwa kunifunza

Kuna kitabu niseme kama sijakosea nisahihishe .

Kinaitwa TOBITI katika biblia kinamuhusu Tobia je hicho kitabu ni HADITHI ZA KUTUNGA,HISTORIA AU UKWELI HALISI?
 
Mkuu unataka kusema kwamba hizi habari za majini unazoeleza hapa umezitoa kwa Sheikh Yahya?
Sio,
Mimi nasoma sana Kitabu Kitakatifu cha Biblia ambacho ndicho kinachonipa ufahamu wa Elimu ya Kiroho.
Ukisoma Biblia, Kwa umakini, polepole, na kwakurudirudia wakati umeituliza akili yako, utapata maarifa mengi yanayo husu Ufalme wa Mbingu na ule wa Kuzimu.
Kwa hapa duniani mafundisho ya Scoan ambayo nimekueleza kuangalia video zake yamenipa ufahamu zaidi wa Elimu ya Kiroho.
Sheikh Yahaya Husseini nilikuwa namsikiliza tu alipokuwa anatoa Elimu ya Majini.
Kwakuwa alikuwa hajasoma Biblia nakuielewa, yeye alijihusisha zaidi katika upande wa mahusiano ya Majini na Binadamu, kwa mtazamo wa wale wanaoona kuwa ati,
"kuna Majini Mazuri yanayoweza kushirikiana na Binadamu katika kazi za maendeleo"

Mimi nakanusha hiyo hoja. Nasema,
"Majini yote ni maovu kwa Binadamu"

Mimi uelewa wangu umetokana na kusoma Biblia kwa bidii.

Nawewe hebu nieleze unachojua kuhusu elimu ya Majini.
Je yako mazuri ?
Je yanashirikianaje na binadamu ?
Je yakimwingia mtu yanatolewaje ?
Unayapenda Majini ?

Lete habari mkuu unavyoelewa wewe.
 
Mkuu asante sana kwa kunifunza

Kuna kitabu niseme kama sijakosea nisahihishe .

Kinaitwa TOBITI katika biblia kinamuhusu Tobia je hicho kitabu ni HADITHI ZA KUTUNGA,HISTORIA AU UKWELI HALISI?
Kitabu cha TOBITI ni cha hadithi za Wayahudi, na hakipo kwenye vitabu vya Historia za Wayahudi.
Kitabu hicho pamoja na YUDITHI ni hadithi za kutunga tu za Wayahudi.
Vitabu hivyo vimeongezwa tu kwenye Biblia wanazotumia Wayahudi.
Havipo kwenye Biblia wanazotumia Wakristo.
Vitabu vya Tobiti, Yudithi, Wamakabayo wa 1, na Wamakabayo wa 2, Hekima ya Sulemani, Hekima ya Yoshua Bin Sira, vinaitwa vitabu vya DEUTEROKANONI,
vipo kwenye biblia ya Kiyahudi kama nyongeza ya Hadithi na Simulizi zao.
Biblia ya Wakristo haina hivyo vitabu, Ina vitabu 66.
Biblia ya Kiyahudi ina vitabu 72 pamoja na hivyo nilivyokutajia.

Unajua Historia inaendana na ukweli.
Kwa mfano,
Kwenye Biblia, vitabu vya Injiri vinasema Yesu Kristo azaliwa huko Israeli na alikuwa Masihi wa Mungu.
Vitabu vya Historia ya Israeli navyo pia, vinasema Yesu Kristo alizaliwa na kuishi Israeli, alikuwa Nabii na mafundisho yake yapo.
Leo ukienda kutalii Israeli utaambiwa kuhusu maisha halisi ya Yesu Kristo huko Israeli, na utaoneshwa alipozaliwa, alipohubiri, alipoteswa, alipokufa, alipozikwa, alipofufuka na alipopaa Mbinguni.
Hivyo unaona Historia na Ukweli vinaenda pamoja.
Lakini maelezo ya vitabu vya TOBITI na YUDITHI hayaonekani kwenye Historia wala kwenye Utalii wa Israeli.
Hapo ndipo utakapo hakikisha kuwa hizo zilikuwa Hadithi tu za kutunga za Waisraeli.
Kwenye Biblia hivyo vitabu havipo.
Vitabi vya DEUTEROKANUNI.
 
Kuna ushahidi gani wa mtu kutolewa majini kwa jina la Yesu? hebu nipe huo ushahidi.
Hata huko makanisani hayaondoki, ukitaka kudhibitisha hilo, nenda kwenye makanisa haya yanayoitwa ya kiroho, utaona watu wanaondolewa mapepo, kama wanavyoyaita ni walewale wa wiki iliyopita.
 
Mkuu unaitaja tu biblia,unaonaje sasa ukatoa vifungu kutoka kwenye biblia vinavyoeleza haya uliyoyaeleza hapa kuhusu majini?

Hebu tumia biblia kutupa somo la hawa viumbe.
 
 
Asante mkuu.

Je ni vitabu gani vingine ambavyo ni hadithi za kutunga vipo katika biblia ya wakristo?
Je biblia ya wautumiayo wakatoliki si ya wakristo na wao si wakristo na kwanini unazani waliweka vitabu vya Tobiti na Yudithi ile hali havina ukweli?

Je kuna uwezekano kuwa kuna stori za kutunga hasa ukisoma Luka moja na kuendelea?

Maana inaonesha watu walijitungia injiri wakawepo watu maalumu wa kuipitisha iwe kwa matakwa yao ama lah.

Kwanini tuamin Yohana,Warumi na tusiamin Tobia na Yuditdhi?

Kwanini nisiseme tunaamin kile tulichokalilishwa na wale wenye nguvu na kipaji cha kuaminisha?

Kwanini isiwe vitabu vyote ni utunzi wa watu maalumu kwa malengo maalumu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…