Mkuu asante sana kwa kunifunza
Kuna kitabu niseme kama sijakosea nisahihishe .
Kinaitwa TOBITI katika biblia kinamuhusu Tobia je hicho kitabu ni HADITHI ZA KUTUNGA,HISTORIA AU UKWELI HALISI?
Kitabu cha TOBITI ni cha hadithi za Wayahudi, na hakipo kwenye vitabu vya Historia za Wayahudi.
Kitabu hicho pamoja na YUDITHI ni hadithi za kutunga tu za Wayahudi.
Vitabu hivyo vimeongezwa tu kwenye Biblia wanazotumia Wayahudi.
Havipo kwenye Biblia wanazotumia Wakristo.
Vitabu vya Tobiti, Yudithi, Wamakabayo wa 1, na Wamakabayo wa 2, Hekima ya Sulemani, Hekima ya Yoshua Bin Sira, vinaitwa vitabu vya DEUTEROKANONI,
vipo kwenye biblia ya Kiyahudi kama nyongeza ya Hadithi na Simulizi zao.
Biblia ya Wakristo haina hivyo vitabu, Ina vitabu 66.
Biblia ya Kiyahudi ina vitabu 72 pamoja na hivyo nilivyokutajia.
Unajua Historia inaendana na ukweli.
Kwa mfano,
Kwenye Biblia, vitabu vya Injiri vinasema Yesu Kristo azaliwa huko Israeli na alikuwa Masihi wa Mungu.
Vitabu vya Historia ya Israeli navyo pia, vinasema Yesu Kristo alizaliwa na kuishi Israeli, alikuwa Nabii na mafundisho yake yapo.
Leo ukienda kutalii Israeli utaambiwa kuhusu maisha halisi ya Yesu Kristo huko Israeli, na utaoneshwa alipozaliwa, alipohubiri, alipoteswa, alipokufa, alipozikwa, alipofufuka na alipopaa Mbinguni.
Hivyo unaona Historia na Ukweli vinaenda pamoja.
Lakini maelezo ya vitabu vya TOBITI na YUDITHI hayaonekani kwenye Historia wala kwenye Utalii wa Israeli.
Hapo ndipo utakapo hakikisha kuwa hizo zilikuwa Hadithi tu za kutunga za Waisraeli.
Kwenye Biblia hivyo vitabu havipo.
Vitabi vya DEUTEROKANUNI.