Che mittoga
JF-Expert Member
- Mar 28, 2017
- 12,658
- 16,205
Mkuu kwanini huchukui uamuzi wa kusoma Biblia ili nawe ujifunze kwenye maandiko ?Mkuu unaitaja tu biblia,unaonaje sasa ukatoa vifungu kutoka kwenye biblia vinavyoeleza haya uliyoyaeleza hapa kuhusu majini?
Hebu tumia biblia kutupa somo la hawa viumbe.
Unataka mi ndio nikusomee halafu nikuelezee. Biblia zipo chukua hatua ya kuisoma kama unataka maarifa zaidi.
Kwani unaogopa kusoma Biblia ?
Mimi nitakupa andiko moja tu na kama utahitaji maarifa zaidi soma Biblia utayapata.
Mungu alipo mwuumba Adam alimweka katika bustani ya Edeni na akamwambia,
Ale matunda yote ya bustanini hapo lakiki matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya asile, kama akila
"hakika atakufa"
Mwanzo 2 : 16 - 17.
Shetani alivyoona Adam na mkewe Wanafaidi matunda waliyopewa na Mungu akajisikia vibaya, aliona wivu husuda na chuki.
Shetani akajigeuza Nyoka akavizia Adamu hayupo pamoja na mkewe Hawa akamwendea Hawa na akamwambia,
Kama mkila hayo matunda mliyoyakatazwa
"hakika hamtakufa"
Mwanzo 3 : 1 - 6.
Sasa hapa kunamambo mengi sana ya kujifunza kuhusu tabia ya Shetani.
Kwanza anamwonea wivu Mwanadamu kwakuwa Mungu amempenda sana kuliko yeye na kumpa mamlaka ya kuitawala nchi na kula mema ya nchi.
Pili ni mwongo sikuzote yaani siyo mkweli.
Mungu anasema Hakika mtakufa, Shetani anasema hakika hamtakufa, mkila hayo matunda.
Adamu na Hawa walipokula Wakafa baadae.
Kumbuka Mungu alitaka Adamu na Hawa waishi milele, kwani aliwaambia mkila hilo tunda ndio mtakufa msipokula hamtakufa.
Unaona jinsi shetani asivyo wa kuaminika, alivyo na hila, asivyompenda mwanadamu, asivyo na msaada wa wema kwa Binadamu.
Adamu alipo kumbuka sasa atakufa kwakuwa kala hilo tunda, Shetani hakuonekana, hakuja kumsaidia Adamu akiepuke kifo.
Hapo ndipo ujue Shetani hana msaada wowote mzuri kwa Binadamu.
Hivyo Shetani alisababisha Adam na Hawa.
Wasiwe na uwezo wa kuishi milele, mwisho wasiku wafe, adhabu ambayo ni kubwa sana, na mbaya sana tunayoipata hivi leo.
Wafukuzwe bustani ya Edeni ambamo walikuwa wanaishi maisha mazuri sana.
Hawa azae kwa uchungu.
Adamu na Hawa waishi kwa jasho lao.
Wanyama wakali wawe maadui wa binadamu kama Nyoka anavyotuuma na tunakufa tusipotibiwa.
Kwa ujumla maisha haya magumu tunayoishi sasa yamesababishwa na Shetani
Soma Kitabu cha
Mwanzo, sura ya kwanza hadi ya tatu utathibitisha habari ninayokueleza.
Ukitaka kujifunza zaidi soma Biblia yote utapata maarifa makubwa sana kuhusu Wema wa Mungu na Ubaya wa Shetani, pamoja na jamii zake za Majini, Mapepo,
Mizimu, nk.
Zaidi Soma Biblia.