Marvel Cinematic Universe special thread

Hivi kwann mnasema Black Adam ni mbaya??
Aisee movie nimeirudia ile na sijaichoka hadi sasa
 
Hii kweli Ntatafuta wakat, Labda weekend maana najua si Kuvuka na Sea Taxi tu.

Najua kuna mtu humu anatamani angeambiwa yeye
Eeh Sea Tax inakufikisha fasta kikubwa uwe na kadi tu,

Hahaha nishamjua huyo, utakuja nae bhana
 
Huyo jamaa unamsema (anaitwa atom), powers zake hazina utofauti na anti man( au na anti man naye humkubali?)
Yes yes, ila sasa hatukumuona akijidogosha, yeye alikua anajikuza tu, labda 2 tutaona makeke yake zaidi
 
Hivi kwann mnasema Black Adam ni mbaya??
Aisee movie nimeirudia ile na sijaichoka hadi sasa
Tunatofautiana tu. Mi Black Adam haijanikosha, nimeangalia mara moja tu nikaifuta[emoji38][emoji38] Kama tu wewe jinsi ile series ya All of us are dead ulivyoona haijakubamba, lakini Mimi nimeikubali sana. Kama kuna vitu naona ni vigumu, basi ni kuirudia Black Adam, kiukweli siwezi
 
Yes yes, ila sasa hatukumuona akijidogosha, yeye alikua anajikuza tu, labda 2 tutaona makeke yake zaidi
Yap, uwezo huo anao.

Kwa maoni yangu, alikuwa anafanya vile kutokana na black adam, kadiri anavyokuwa mkubwa na nguvu zinaongezeka, alihitaji hizo nguvu kupambana.

Hope tutaonana nae huko black adam 2.

Anyway, WB wameboa raia sana kumuachia Henry Cavill.
 
Huyo jamaa unamsema (anaitwa atom), powers zake hazina utofauti na anti man( au na anti man naye humkubali?)
Mi bado mgeni sana kwenye muvi za aina hii, huenda hayo mambo nisiyoyapenda nitakuja kuyaelewa mbeleni huko. Sasahivi itabidi nianze kufuatilia kila muvi ya Marvel na DC ndio nitakuja kuyaelewa hayo madude.
Sasahivi najitahidi niwe kotekote nilikuwa sipendi Korean movies sasahivi naangalia, nilikuwa sipendi drama sasahivi napenda, nilikuwa siangalii animations sasahivi naangalia, series nilikuwa naona uvivu kufuatilia sasahivi nafuatilia vizuri tu, sasa nimeamua kuja huku pia siku za mbele hizo power za kuwa giant na kujidogosha pengine nitaziona za kawaida[emoji38][emoji38]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Unakumbuka kumbe kuhusu all of us are dead, hapana bhana mule utoto mwingi sana,
Kama sasa hivi naangalia series ya Willow, najikaza tu ila utoto mwingi hadi nakasirika ila story yake ni nzuri.
 
Karibu kwenye ulimwengu wa Animation,
Ndio mitaa yangu hiyo.
 
Kwa wote ambao hawakuipenda Black Adam basi 2 wakae mkao wa kuenjoy, nimepata maono itabamba sanaaa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Unakumbuka kumbe kuhusu all of us are dead, hapana bhana mule utoto mwingi sana,
Kama sasa hivi naangalia series ya Willow, najikaza tu ila utoto mwingi hadi nakasirika ila story yake ni nzuri.
Hiyo Willow ni Marvel au
 
Karibu kwenye ulimwengu wa Animation,
Ndio mitaa yangu hiyo.
Leo usiku najituliza na Puss in Boots: The Last Wish halafu The Amazing Maurice Hadi Leo sijaangalia ila nayo soon nitaangalia. Paws of Fury na Minions mwaka Jana ziliumwagilia moyo wangu ipasavyo[emoji28][emoji28]
 
Kwa hiyo mwaka huu 2023 kwenye movies and TV shows za Marvel tunasubiria
1. Ant-Man and the Wasp: Quantumania (Feb 17)
2. Guardians of the Galaxy Vol 3 (May 5)
3. What If?.....(Spring 2023)
4. Secret Invasion (Spring 2023)
5. Spider-Man: Across the Spider Verse (June 2)
6. The Marvels ( July 28)
7. Loki (Summer 2023)
8. Echo (Summer)
9. Kraven the Hunter
10. Iron Heart (Autumn 2023)
11. Agatha: Coven of chaos
 
Leo usiku najituliza na Puss in Boots: The Last Wish halafu The Amazing Maurice Hadi Leo sijaangalia ila nayo soon nitaangalia. Paws of Fury na Minions mwaka Jana ziliumwagilia moyo wangu ipasavyo[emoji28][emoji28]
Iangalie kwanza Puss in Boots halafu tutakuja kuichambua.... the Amazing Maurice niliiangalia ilivyoisha nikairudia tena hapo hapo same na Minions,
Can you imagine[emoji38]
 
Iangalie kwanza Puss in Boots halafu tutakuja kuichambua.... the Amazing Maurice niliiangalia ilivyoisha nikairudia tena hapo hapo same na Minions,
Can you imagine[emoji38]
Hiyo Despicable Me 4 itoke tu tuiangalie, 2024 mbali lakini[emoji848][emoji848] hii ndio next movie ya Minions
Ukiangalia animation kali tuambieni tusije tukachoma bando. Diary of a Wimpy kid najifikiria mara mbilimbili niishushe au la[emoji2][emoji2]
 
M all ears

Kwenye Cinematic Event Kubwa Tupange tukutane tukaangalie, kama tatizo ni ID zikibaki anonymous sawa ila kwa [mention]Dream Queen [/mention] yeye kubaki anonymous sijajua hapo [emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…