Marvel Cinematic Universe special thread

Marvel Cinematic Universe special thread

Mkuu naomba twende wote[emoji120]

NB. Umeitazama Episode ya mwisho ya The Boys?
Nimeiona jana episode ya mwisho, kwa kweli season 4 itakua ya moto sana, naona kabisa Ryan atawasumbua nimeona lile tabasamu lake pale mwishoni baada ya baba yake kumuua yule jamaa na wajinga kushangilia lile tabasamu limeongea vitu vingi sana kwa ajili ya next season,

Mission bado inaendelea next season itakua ya Victoria, The Boys watajipanga jinsi ya kumuondoa,

Nimependa MM ameungana tena na Mtoto wake maana kila siku nilikua namfikiria kama Mtoto wake atampenda tena,

Queen Maeve kua hai na Ashley kufuta zile footages nimependa sana, ila kipondo alichompa Homelander sio mchezo [emoji119] sikujua kama ana nguvu kiasi kile,

Sasa Soldier Boy wamemuhifadhi tena ikitokea kafunguliwa sijui itakuaje hizo hasira zake,

A-Train kanipa huzuni kaka ake alivyomkataa,

Hivi huyu Deep hua ana matatizo gani?? Kwanini asiishi tu baharini na Samaki wenzie naona kama Nchi kavu hapamfai kila siku anatia yeye huruma tu,

Black Noir kanihuzunisha sana, Homelander kweli hana rafiki, nilicheka alipowaambia kwenye kile kikao chao cha dharura "you guys are not my family, i don't need your help"

Haya tusubiri season 4 sijui wataileta lini tena.
 
Yes, maeve pale kamkalisha Homelander sema alikuwa ana practice kweli kweli kipindi kile na ikalipa

besides maeve nimependa writers walivyomuandaa mpaka kujitoa muanga kuwasaidia wenzake

Unakumbuka kule alipowageuka wasimuue soldier boy...mpaka starlight akamwambia “I thought you were a hero” Maeve akamjibu kwa kusema “there is no such thing” lakini ironically baadae Maeve ndio akawa “hero” kajitoa sadaka ili awaokoe wenzie nilipenda sana, kudos kwa writers room

Kingine soldier-boy backstory ya baba ake kutomkubali kumwambia kuwa kachukua shortcut whatsoever... imetufanya tumuone na yeye ni human after all japo ni piece of shit, kwahiyo alivyokuwa anamkataa Homelander na mjukuu wake huku akimuita Homelander p*ssy attention seeker sijui [emoji23](nilicheka balaa)

Alikuwa ana maana labda plan yake ilikuwa akiwa na mtoto wake amfanye awe better man alafu akamkuta mwanae homelander ndio vile dumpster fire...

na kuna vitu niliviona vilifanana na ile riot ya capital kipindi cha trump kama niko sahihi

Hii episode nikisema niichambue ntaandika gazet... mambo hayo ya jamaa etu sio mm[emoji28]

Mwishon I felt sorry for deep...japo kuwa ana matatizo yake ila yule dem kazingua sana yaani kamuandika jamaa kitabu kabisa na kapata airtime kwenye talk-show utakuta anamponda mwana[emoji23]

Ningekuwa mm ngemfanya mengi yule demu
Episode tamu sana, imetuacha na vibe la kujua what next huku kila mtu kawa na happy ending kasoro A-Train na Deep
 
Episode tamu sana, imetuacha na vibe la kujua what next huku kila mtu kawa na happy ending kasoro A-Train na Deep
Hao ndio kila siku inakuaga ivo…just kupotray the mental health of superheroes…apart from that hamna kitu…hawajahusika kabisa katika mapigano
 
The boys imeweza Mix hadi animation humo humo vipande vya Noir na musical 🎶 numbers kama broadway...ile episode Kimiko anacheza Hospitali, nikawaheshimu

PS: aliengalia MoM kwa mara ya kwanza ile Music notes fight scene aliionaje😅?
 


Dr strange suit up scene
 
Inabidi na mimi niiangalie hiyo the boys sasa.
groot umenifurahisha kitu unajua nn, keeping up with the internet, movies and memes inakuwa ngumu kweli siku hiz, na ukiachwa unajihis kama unazeeka flan

Kuna siku nlikutana na wadau zangu tukawa mahali wanaongelea stranger things wakati sijaona hata episode moja siku ile nlijiuliza nmefuata nini hapa [emoji23][emoji3064]
 
groot umenifurahisha kitu unajua nn, keeping up with the internet, movies and memes inakuwa ngumu kweli siku hiz, na ukiachwa unajihis kama unazeeka flan

Kuna siku nlikutana na wadau zangu tukawa mahali wanaongelea stranger things wakati sijaona hata episode moja siku ile nlijiuliza nmefuata nini hapa [emoji23][emoji3064]
Kweli aisee😂😂. Maana nimejikuta kila siku naachwa njia panda😅
 
MCU wana akili sana ya kupiga pesa, kila series yao, iwe animated au live action, wanaunganisha na muvi inayosubiriwa. kudos kwa the fegie bros na team yao nzima.
 
Ms. MARVEL Imevunja rekodi ya highest score kwa tv series zote za marvel 😂😂
20220715_030216.jpg
 
Back
Top Bottom