Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Naibu waziri wa mawasiliano na teknolojia ya habari Mhandisi Maryprisca Mahundi amepiga goti mbele ya wajumbe wa mkuato mkuu wa umoja wa wanawake Tanzania UWT mkoa wa Mbeya akiwashukuru kwa kumuamini na kumchagua kwenye uchaguzi wa mwaka 2020, huku akiomba ridhaa kwa wajumbe hao kumuamini na kumpa kura kwa mara nyingine kua mbunge wa viti maalum mkoa wa Mbeya.
Mahundi amesema katika kipindi cha miaka mitano amejitaidi kadri ya uwezo wake kuwakwamua kina mama kiuchumi ili kuepukana na mikopo umiza, huku akiwaomba ridhaa hiyo kwa mara nyingine uli kuendelea kuwafikia wanawake wengi zaidi ambao bado wanateseka kupitia mikopo umiza. Wajumbe zaidi ya 1500 wamekutana leo kwaajili ya kupiga kura ya kumchagua mbunge wa viti maalum atakayewakilisha wanawake Bungeni, ambapo hadi sasa uchaguzi bado unaendelea kwa watiania nane kupigiwa kura hizo.