Masaa 10 ya Jehanamu nyumbani kwa Sister

Masaa 10 ya Jehanamu nyumbani kwa Sister

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Last Jumamosi nilipata mualiko kumtembelea Sister Home kwake Mikocheni. Nilienda na Mke Wangu na Mtoto wetu mmoja wa miaka 4.5

Saa nne tulikuwa tumefika home maana tuliambiwa siku hiyo hata kinywa tukafungulie pale na jioni tukifungie pale pale. Waswahili wanasema mtu hakatai wito.

Sister ana watoto wawili, mmoja miaka 6 na mwingine 4. Tulianza kupata changamoto mapema sana baada ya kutia tu mguu pale home. Watoto wake wanalilia simu. Nikawa nawaza hii iPhone yangu nimpe mtoto achezee kweli?

Basi yule wa miaka minne akawa analia balaa anajirusha huko na kule akitaka apewe simu acheze game. Sister anacheka tu na kusema "We Junior usimsumbue Uncle bwana, basi chukua hii yangu huku ana mpeti peti" wallah nilikuwa napatwa na hasira sana.

Akaendelea kusema simu zao mle ndani zote zimeshapasuliwa vioo mara kadhaa sababu ya watoto kugombania. Wakati huo tena yule mtoto anamvuta mke wangu nywele nyuma ya kiti.

Sister anasema tu "We xxx mwache Aunt nitakuwa sikupi game ucheze" Yule Mtoto kuambiwa vile aliangua kilio kikubwa sana. Nikahisi wife uzalendo ulimshinda akamwasha kibao. Kumbe sivyo. Alikasirika sababu ya kuambiwa atanyimwa game.

Sister akawa anambembeleza wakati huo yule mwingine ametokea chumbani kwa Wazazi wake kavaa chupi ya sister kichwani. Mbaya zaidi kaja kwangu nimwone eti kavaa mask nimeshika hivi ni chupi astaghafilulah nikaachia kama mtu aliyeshika moto. Ndio Baba yake akaja iokota na kuipeleka tena room akisema wewe xxx acha michezo hiyo kwa uncle.

Tumeenda kula mezani yule mdogo kaanza tu kulia. Analia wanamuuliza nini anasema hataki maziwa anataka chocolate nikajiuliza hili si lilikuwa suala la kusema tu why alie?

Huyu mkubwa amesusa kula akaanza bembelezwa, akabembelezwa sana mwishowe akaitwa Dada amlishe mtoto wa miaka 6 analishwa? Tumerudi kukaa sitting room taabu zinaendelea wanakuja kunidandia mwilini wakitaka niwabebe, wakitaka tukacheze mpira, wakitaka tuimbe.

Muda huo wote sijaweza hata kukaa vizuri kuongea na wenyeji wangu. Wao wanacheka tu na kufurahi kiukweli Mtoto wangu akawa kama amepigwa na butwaa hivi anashangaa sana.

Wakaambiwa wakacheze kwenye bembea. Dada akaitwa akawasukume, wangu alienda ndani ya dk 10 akarudi hataki kwenda tena. Nadhani walimghasi na vile hajazoea shida na ugomvi.

Akina uncles wakarudi wanalia mmoja anadai kaangushwa na mwenzie na mwenzie anadai amegongwa, wakiwa wanabishana mmoja alimrushia remote control mwenzie ikamkosa. Sister akawa mkali akisema "wewe junior kesho hupandi gari yangu, utapanda ya baba" hii ndo adhabu yake eti.

Mpaka mchana nilikuwa nmeshachoka sana kukaa pale. Tunakula mezani yule jr akaanza kulia, wanamuuliza jun unalia nini anasema usingizi unamuuma, nilishangaa sana kumbe hata usingizi una maumivu, ikabidi achukuliwe akalazwe na mwenzie naye akawa ameinama kwenye meza kalala anaulizwa naye anasema usingizi akabebwa akalazwe, huo ni mchana.

Mpaka jioni nilishachoka kabisa na sikuwa na hamu, mke wangu alikuwa ametulia kimya na mtoto wangu amejituliza pembeni yangu, kiunyonge akitaka tuondoke.

Jumapili tumekaa sebuleni mara Mtoto wangu wa miaka 4.5 akaanza kulia nikamuuliza kulikoni tena? Akanijibu usingizi.😡😡😡😡😡kama Mama yake asingeniwahi nadhani tungekuwa tumempeleka hospital amelazwa mashavu yamepasuka. Nlianza ona emeingiwa na pepo.

Nlikuja muuliza toka lini usingizi umekuwa ugonjwa kwake au maumivu? Nilimuuliza siku zote hufanyaje akajibu huenda chumbani akapanda kitandani akalala. Then swali langu likawa leo amepatwa na nini? Akaomba msamaha. Sorry Daddy!

Nikashusha pumzi. Nika rewind matukio yooooote ya Jumamosi kwa sister it was like a little hell. Na mtoto wangu alitaka eti aige that life. Nikashangaa wenzangu wanaleaje Watoto, nami nakosea wapi?

Well, watoto wangu tunacheza, tunataniana, tunaimba n.k but kwa wakati. Na hawashiki simu yangu kuchezea nakaa mpaka mwezi sisikii wanalia. Mfano huyu wa miaka 6 anaanzaje kulia? Huyu wa miaka 4 anaweza ongea why alie?

Siwezi enda kwa sister tena na hata home simwaliki kuja na watoto wake. Acha tuwe tunaonana juu kwa juu. Sitaki tuje kutafutiana lawama baadaye. Sitaki undugu lawama. Kama ameamua kufuga tushetani akae nato peke yake. Sitaki kabisa.
 
Ukianza kusikia watoto wanaitwa akina Juniya.. kaa mbali...

Hongera kwa uvumilivu.. mie bwana one hour in tayari wangekwisha feel presence of The Bigger [emoji48].. Sipendi purukushani.. na familia nzima ingejua kuwa nipo.

Nikishindwa I will make a lame excuse na nitabeba viambata vyangu vyote na kuondoka... An excuse so lame nikaondoka lazima ujievaluate.
 
Ahuahuahuahua! Umenikumbusha jambo Sir, nilienda mahala kwa Shangazi yangu ambaye kidogo umri umemuenda anaishi mjukuu wake mmoja aliyepatikana baada ya toto lake kukandwa huko na halijaolewa.

Jinsi anavyomlea unaweza kuanza kulia, ni mgomvi plus msumbufu anapomuona babu na bibi yake wapo around anaweza kumwaga maji makusudi chini, akabeba chakula cha wageni chote, akachana biblia, akalilia simu na hapa ndio komesha analia kama kaumwa dondola.

Anafanya vimbwanga vyote hivi akiambiwa acha na bibi au babu yake basi anazidi kumbe ndivyo wanavyomlea na akipiga watoto wenzake anarudishiwa makonde na ngumi heavy asipokuwepo bibi au babu yake halii ila wakiwepo hicho kilio ni cha siku nzima.

Hivyo mkuu hasira ulizokuwa ukizipata, mimi nilizipata mara dufu na unakuwa huna la kufanya maana anadekezwa na kila mtu hata yai lina nafuu unajaa hasira ila huwezi kufanya kitu.
 
Ukianza kusikia watoto wanaitwa akina Juniya.. kaa mbali...
Ahahahaha! Sir i understand you
Hongera kwa uvumilivu.. mie bwana one hour in tayari wangekwisha feel presence of The Bigger [emoji48].. Sipendi purukushani.. na familia nzima ingejua kuwa nipo..

Nikishindwa I will make a lame excuse na nitabeba viambata vyangu vyote na kuondoka... An excuse so lame nikaondoka lazima ujievaluate.

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Ahuahuahuahua! Umenikumbusha jambo Sir, nilienda mahala kwa Shangazi yangu ambaye kidogo umri umemuenda anaishi mjukuu wake mmoja aliyepatikana baada ya toto lake kukandwa huko na halijaolewa..
Nyie mnauvumilivu sana.. mie nitasema maneno machache wazee wataficha uso.. au nikiwatembelea watamfungia ndani.. iswear
 
Mimi huwa navifinya kama ni wajirani ,mtoto wa sister namtia mimbata tu akiendelea fimbo zinamhusu
Kwanza nawaza yaani sister yupi huyo anaweza kuwa na vijana ..akakaa akawatazama wanaleta shida kwa ankali...hyiiiiii bhagosha! Mh!

Kwanza watoto watatupisha.. nimchane yeye na mumewe halafu ndio niondoke.
 
Kwanza nawaza yaani sister yupi huyo anaweza kuwa na vijana ..akakaa akawatazama wanaleta shida kwa ankali...hyiiiiii bhagosha! Mh!

Kwanza watoto watatupisha.. nimchane yeye na mumewe halafu ndioniondoke

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Mimi hao uncle zangu heshima mbele, wakizingua wanajua nawanyoosha muda huohuo, nikisema acha mara moja ya pili siulizi.
 
Mimi hao uncle zangu heshima mbele ,wakizingua wanajua nawanyoosha mda huohuo, nikisema acha mara moja ya pili siulizi.
Unajua hakuna kitu kinatisha kwa mtoto kama kujua wazazi wake kuna mtu wanamuheshimu.

Ukiingia kwao... Unasikia wamewekwa kitimoto.. Ankali wenu hapendi ujinga.. kuruka ruka hapana... Mnakaa mnatulia.. msije mkatutia aibu... Watoto watakuwa wanakuangalia from vicinity 🙂
 
Nilikuwa safari nikapita kwa kaka mdogo kumsabahi, nilimkuta na familia yake yote yaan yeye, mkewe na mwanae.

Huyo mtoto ni anafujo utasema mji mzima umehamia humo ndani, kulia lia usipime!!

Akajipendekeza anga zangu, anataka maji huko akaja kulilia kwangu, nikamnyazisha kwa ukali! Nikamuuliza maji yako wapi? Huwezi kuyafikia? Kuna ulazima gani kulia?

Nikatoka nje, nikarudi na bakora! Alichezea viboko mbele ya baba na mama yake! Baada ya hapo nyumba ikawa kimyaaa!

Na hata nilipoondoka naambiwa kabadilika sana kulia hovyo hovyo ameacha na ana akili za kujiongeza sasa.
 
Nilikuwa safari nikapita kwa kaka mdogo kumsabahi, nilimkuta na familia yake yote yaan yeye, mkewe na mwanae.

Huyo mtoto ni anafujo utasema mji mzima umehamia humo ndani, kulia lia usipime!!

Akajipendekeza anga zangu, anataka maji huko akaja kulilia kwangu, nikamnyazisha kwa ukali! Nikamuuliza maji yako wapi? Huwezi kuyafikia? Kuna ulazima gani kulia?

Nikatoka nje, nikarudi na bakora! Alichezea viboko mbele ya baba na mama yake! Baada ya hapo nyumba ikawa kimyaaa!

Na hata nilipoondoka naambiwa kabadilika sana kulia hovyo hovyo ameacha na ana akili za kujiongeza sasa.
Custodian of the Clan!

Mie nimejituniku cheo hicho... 🙂

Safi sana.. CC hahaha
 
Nyie mnauvumilivu sana.. mie nitasema maneno machache wazee wataficha uso.. au nikiwatembelea watamfungia ndani.. iswear

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Ni ugenini mkuu unapaswa kuficha uhalisia wako.
Imagine linakuja unazungumza linakupiga kofi la mdomo kwa kukushitukiza na linaambiwa " We Ivan jamani mbona hivyo" linaanza kulia kisa limeambiwa hivyo 😟
 
Back
Top Bottom