teamasala
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 615
- 633
Mi pia kipindi nmejifungua mama mkwe wangu alikuja na mjukuu wake wa 5yrs jamani ni mjeuri' na kulilia kila kitu anachokiona kitamj kwenye fridge[emoji23]' alimkuta dada wangu wa kazi yule mtoto wa 5yrs alikua anamwonea jamani esp. Kipindi nipo hospitali adi dada wangu akakosa amani' yani ni anaweza pita jikoni akamkuta dada akampiga kibao na kumsemea uongo au akimkuta dada anakunywa juice anaimwaga' nakumbuka kuna siku niliwapa korosho wale pamoja akazitemea mate ili dada asile uuhw bibi anamtetea mjukuu wake yanni nilichoka nikatamani siku ziende mbele.
Ahuahuahuahua! Umenikumbusha jambo Sir, nilienda mahala kwa Shangazi yangu ambaye kidogo umri umemuenda anaishi mjukuu wake mmoja aliyepatikana baada ya toto lake kukandwa huko na halijaolewa.
Jinsi anavyomlea unaweza kuanza kulia, ni mgomvi plus msumbufu anapomuona babu na bibi yake wapo around anaweza kumwaga maji makusudi chini, akabeba chakula cha wageni chote, akachana biblia, akalilia simu na hapa ndo komesha analia kama kaumwa dondola.
Anafanya vimbwanga vyote hivi akiambiwa acha na bibi au babu yake basi anazidi kumbe ndivyo wanavyomlea na akipiga watoto wenzake anarudishiwa makonde na ngumi heavy asipokuwepo bibi au babu yake halii ila wakiwepo hicho kilio ni cha siku nzima.
Hivyo mkuu hasira ulizokuwa ukizipata mimi nilizipata mara dufu na unakuwa huna la kufanya maana anadekezwa na kila mtu hata yai lina nafuu unajaa hasira ila huwezi kufanya kitu.