Nilikuwa safari nikapita kwa kaka mdogo kumsabahi, nilimkuta na familia yake yote yaan yeye, mkewe na mwanae.
Huyo mtoto ni anafujo utasema mji mzima umehamia humo ndani, kulia lia usipime!!
Akajipendekeza anga zangu, anataka maji huko akaja kulilia kwangu, nikamnyazisha kwa ukali! Nikamuuliza maji yako wapi? Huwezi kuyafikia? Kuna ulazima gani kulia?
Nikatoka nje, nikarudi na bakora! Alichezea viboko mbele ya baba na mama yake! Baada ya hapo nyumba ikawa kimyaaa!
Na hata nilipoondoka naambiwa kabadilika sana kulia hovyo hovyo ameacha na ana akili za kujiongeza sasa.