Masahihisho: Kinachosherehekewa ni Uhuru wa Tanganyika siyo Tanzania Bara. Hatutavumilia upotoshaji

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426


Hii ni kwa sababu Mwl Nyerere na viongozi wa TANU walikuwa Watanganyika na waliikomboa Tanganyika na wala si nchi nyingine yoyote ile.

Watanganyika hampaswi kuvumilia uongo wowote ule hata kama anayeuongea ni kiongozi mzito, kataeni hadharani ili mheshimike.

 
Tanganyika gained independence on Dec. 9, 1961, and became a republic one year later. On April 26, 1964, it joined with Zanzibar to form the United Republic of Tanganyika and Zanzibar.28 Nov 2023
 
Ilitakiwa mumsapoti sana hayati Mchungaji Mtikila anapopambania upatikanaji wa Tanganyika. Badala yake mkampora UKAWA na kabla ya hapo mlimfukuza uanachama mwaka 1997 alipogombea ubunge Ludewa/Makete.

Alipokua anasema saa ya ukombozi ni sasa, mnasema tulishakombolewa zamani. Alikuwa anapambania uwepo wa Tanganyika kwa faida ya watanganyika na sio kwa faida yake au ya chama. Hakua muumini wa vyama vya siasa.

Majuto ni mjukuu.
 
Hivi haya maneno/majina ya 'Tanzania Bara' na 'Tanzania Visiwani' yalianzia wapi??
Yaliingizwaje kwenye Katiba ya nchi hii??
 
Kwani "wapotoshaji" wao wanasemaje na kwa msingi upi na kwa manufaa ya nani?
 
Ni sawa kabisa, lakini wakati huo hakuna aliyejuwa kuwa hali itakuja iwe mbovu kama ilivyo fikia sasa.
Kweli majuto ni mjukuu!
Pengine yeye alikuwa na maono ambayo wengi hawakuyaelewa.
 
Mbona umeweka picha ya Nyerere agenda kuzuga kupiga kura?

Hiyo Tanganyika ipo?
 
Jamani Tanzania si imezaliwa baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar? Sasa inakuaje kusema unasheherekea uhuru wa Tanzania bara wakati kipindi hicho hata tanganyika haijaungana na Zanzibar?
Kama waliifuta Tanganyika sababu ya Tanzania waifute na Zanzibar sababu ndio zilizozaa neno Tanzania.
 
Haja hii nimeiendeshea darasa humu, Darsa: Maadhimisho ya Leo, ni ya Uhuru wa Tanzania, yaani, Tanzania National Day, ila Kumbukumbu Ndio ya Uhuru wa Tanganyika!
Kwa vile hakuna tena Tanganyika, is dead and buried long ago, kilichopo sasa ni Tanzania, then maadhimisho ni uhuru wa Tanzania ila kumbukumbu ndio ya uhuru wa Tanganyika.
Kuna vitu viwili, maadhimisho na kumbukumbu!.
P
 
Nyie CCM ndiyo mkaamua kumtoa roho kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…