Masahihisho: Kinachosherehekewa ni Uhuru wa Tanganyika siyo Tanzania Bara. Hatutavumilia upotoshaji

Masahihisho: Kinachosherehekewa ni Uhuru wa Tanganyika siyo Tanzania Bara. Hatutavumilia upotoshaji

Habari P,
Tenga kati ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwako na adhimisho la kuzaliwa kwako.
Sherehe ya kuzaliwa ni ile siku mtoto amezaliwa, hivyo siku ya uhuru wa Tanganyika ni ile siku ya kupata uhuru.

Tanganyika ilidumu toka Desemba 9, 1961-April 26, 1964, takriban miaka miwili na miezi 4, na kugeuka Tanzania, hivyo maadhimisho yote ya uhuru toka hiyo 1964 ni maadhimisho ya uhuru wa Tanzania na sio Tanganyika. Uhuru ni wa Tanganyika na maadhimisho ni ya kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika, ila yanaadhimishwa na Tanzania, hivyo it's Tanzanian national day!.
P
 
Haja hii nimeiendeshea darasa humu, Darsa: Maadhimisho ya Leo, ni ya Uhuru wa Tanzania, yaani, Tanzania National Day, ila Kumbukumbu Ndio ya Uhuru wa Tanganyika!
Kwa vile hakuna tena Tanganyika, is dead and buried long ago, kilichopo sasa ni Tanzania, then maadhimisho ni uhuru wa Tanzania ila kumbukumbu ndio ya uhuru wa Tanganyika.
Kuna vitu viwili, maadhimisho na kumbukumbu!.
P
Tanzania bara imetokea wapi?
Nani aliunda hilo jina Tanzania bara?
Kwanini wanaogopa kutamka neno Tanganyika?
 
Sherehe ya kuzaliwa ni ile siku mtoto amezaliwa, hivyo siku ya uhuru wa Tanganyika ni ile siku ya kupata uhuru.

Tanganyika ilidumu toka Desemba 9, 1961-April 26, 1964, takriban miaka miwili na miezi 4, na kugeuka Tanzania, hivyo maadhimisho yote ya uhuru toka hiyo 1964 ni maadhimisho ya uhuru wa Tanzania na sio Tanganyika. Uhuru ni wa Tanganyika na maadhimisho ni ya kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika, ila yanaadhimishwa na Tanzania, hivyo it's Tanzanian national day!.
P
Mkuu huu uongo wako unaouandika humu ni kwa manufaa ya nani ?
 
Mkuu Paskali angalia kwenye mashindano ya CECAFA under 18 Tanzania imecheza na Zanzibari. Sasa huku tunakoelekea sio kuzuri sababu upande mmoja haukaripiwi umeachwa ufanye mambo yake wakati upande mwingine huu wa bara umejaa wanafiki na wachumia tumbo
 
Zanzibar ni Nchi
 
Uko sahihi. Kabla ya 1964 hakukuwa na nchi inayoitwa Tanzania.

Nadhani neno Uhuru wa Tanzania Bara linakuja kutokana na kutokuwepo kwa hiyo Tanganyika kwa Sasa.
Tanganyika ilikufa kibudu 1964 baada ya kuungana na Zanzibar.
Yaani nchi mbili huru zinaungana, moja inakufa moja inaendelea kuexist, haya nayo ni maajabu.
Tanganyika iko hai
 
Ilitakiwa mumsapoti sana hayati Mchungaji Mtikila anapopambania upatikanaji wa Tanganyika. Badala yake mkampora UKAWA na kabla ya hapo mlimfukuza uanachama mwaka 1997 alipogombea ubunge Ludewa/Makete.

Alipokua anasema saa ya ukombozi ni sasa, mnasema tulishakombolewa zamani. Alikuwa anapambania uwepo wa Tanganyika kwa faida ya watanganyika na sio kwa faida yake au ya chama. Hakua muumini wa vyama vya siasa.

Majuto ni mjukuu.
Mtikila aliangushwa na watanzania wote. Tusinyoosheane vidole.
 
Naipenda nchi yangu Jamhuri ya Tanganyika. Waseme siku ile iliposhushwa Union Jack ni bendera ipi ilipandishwa kama siyo hii hapa????
FB_IMG_1702085740919.jpg
FB_IMG_1702085740919.jpg
FB_IMG_1702085740919.jpg
FB_IMG_1702085740919.jpg
FB_IMG_1702085740919.jpg
FB_IMG_1702085740919.jpg
 
Mtikila aliangushwa na watanzania wote. Tusinyoosheane vidole.
Ukiona watu wanasema mtu hawezi kuwa mkubwa kuliko chama cha siasa basi ujue hapo upo mahali pasipo sahihi.

Yaani watu hawaamini mawazo ya mtu mmoja kuwa yanaweza kuwa sahihi kuliko ya taasisi (chama). Na kwenye kauli hizi za mtu kutokua mkubwa kuliko chama, hapa vyama vya upinzani huungana mkono na CCM, wote huwa na msimamo huo.

Mtu akitoa mawazo tofauti na ya taasisi, piga chini. Hawezi kupata umaarufu kuliko chama
 
Hii ni kwa sababu Mwl Nyerere na viongozi wa TANU walikuwa Watanganyika na waliikomboa Tanganyika na wala si nchi nyingine yoyote ile.
Duh!!

Kuna watu wamejichomeka kwenye hii sherehe!!! Bado na hapa wanataka gawio la sherehe!!! Hii ni too much
 
1702107053580.png

Ni nani leo hii atakubali kujipanga hivyo kwenye foleni bila bunduki pembeni
 
Hii ni kwa sababu Mwl Nyerere na viongozi wa TANU walikuwa Watanganyika na waliikomboa Tanganyika na wala si nchi nyingine yoyote ile.

Watanganyika hampaswi kuvumilia uongo wowote ule hata kama anayeuongea ni kiongozi mzito, kataeni hadharani ili mheshimike.

View attachment 2837078
Tanganyika a.k.a Tanzania Bara. The United Kingdom a.k.a Britain. Wapi tatizo?
 
Back
Top Bottom