Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Pamoja na yote yanayoendelea kuhusu Mdude, ambayo nisingependa kuyarudia hapa, kinachopaswa kufahamika ni kwamba Mdude Nyagali alitolewa gerezani baada ya kuishinda serikali ya Tanzania Mahakamani.
Hakutolewa kwa Msamaha wa Rais wala hakutolewa kwa Huruma ya Mtu yeyote yule, alishinda Kesi ya kubambikwa, ya uongo iliyotungwa ili kumkomoa, shukrani kwa Chama chake na Jopo la Mawakili wake wakiongozwa na Mangula.
Wale wanaotaka anyamaze kama zuzu, yaani akae tu kimya kama ndondocha wa kiarabu pamoja na unyama wote aliotendewa kuanzia kule walikoshindwa kumuua baada ya Mungu na Wazungu kuingilia kati, hadi hizi njama za madawa ya kulevya, hatukuwasikia wakikemea unyama aliotendewa, na itambulike wazi kwamba waliomtesa na ambao walitaka kumuua Mdude bado wapo na wapo madarakani, kuanzia viongozi wa juu, watekaji, polisi na wengine wengi, aliyepungua ni mmoja tu, kwahiyo tunapomkosoa Mdude kwa kauli zake tufikirie pia aliyotendewa na watu hawahawa tunaowatetea.