DOKEZO Masaki: Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Anayedaiwa kuwa Afisa Usalama (TISS) afanya vurugu, amjeruhi mwananchi.

Tukio la kutisha lilitokea jana usiku (26.10.2024) katika klabu maarufu inayojulikana kama 1245 Lounge, Bar and Restaurant iliyopo Masaki, ambapo Afisa Usalama wa Taifa anayefahamika kwa jina la Derick Junior Lima (maarufu kama Chief Abayomi) alianzisha fujo na kujaribu kumpiga risasi Julian Bujulu baada ya kutokea sintofahamu kati ya Derick na Julian iliyosababishwa na Derick kujaribu kulazimisha kuondoka na mwanamke aliekuwa ameenda kustarehe katika Club hiyo akiambatana na Julian.

Taarifa zinaeleza zaidi kwamba Derick ni mtu mwenye mke na watoto na kwamba mwanamke anayehusishwa na ugomvi huo ni Dada yake Julian ambapo walikuwa wametoka pamoja kwenda kwenye starehe.

Kwa mujibu wa mashuhuda, ghasia zilianza baada ya Derick kutaka kuondoka na mwanamke huyo kwa nguvu bila kujali yupo na kina nani, jambo lililopelekea Kaka mtu kuingilia kati akizuia Dada yake kuondoka na Derick. Mzozo huo ulipopamba moto, Derick alitoa bastola akiwa na lengo la kumpiga risasi Julian lakini kwa bahati nzuri, bastola ya Derick iligoma kutoa risasi. Baada ya kushindwa kupiga risasi, kwa hasira Derick aliamua kumpiga Julian kichwani kwa kutumia kitako cha bunduki hiyo na kumsababishia majeraha makubwa.

Kamera za CCTV katika klabu hiyo zimenasa tukio zima jinsi Derick alivyotenda na kusababisha majeruhi makubwa kichwani yaliyopelekea kuwahishwa hospitali na baadae kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili ambapo amelazwa kwa matibabu zaidi.

Mpaka wakati huu, Derick Lima anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay huku uchunguzi ukiendelea. Kuna wasiwasi mkubwa kwamba haki haitatendeka kutokana na uhusiano wake wa karibu na wakubwa. Mpaka sasa kuna baadhi ya β€œMatajiri” wa mjini ambao wamekuwa wakimtumia Derick katika kukwepa kodi na kutekeleza mambo yao haramu wamekuwa wanaendelea na jitihada kuhakikisha anatoka mikononi mwa polisi bila kuwa na kesi.

Polisi wamechukua mashine za CCTV katika Club hiyo na katika kuhakikisha mmiliki wa Club hiyo anaminywa na asitoe ushirikiano, wameachia makusudi video inayomuonyesha mmiliki huyo akifanya mapenzi na mmoja wa aliekuwa mfanyakazi wake katika moja ya ofisi za Club hiyo.

Your browser is not able to display this video.

UPDATE: Polisi wamemkamata Polisi wamtia mbaroni anayedaiwa kuwa "Afisa Usalama" aliyemjeruhi raia kwa 'kitako cha bunduki'
 
Duh,
Nchi inazidi kupoteza mwelekeo kwa kasi sana.

Waziri Rajabu..
 
Aisee! Kuna aina ya watu hutakiwi hata uji associate nao na kuna club siendi, call me old school but wacha tu baadhi ya vitu vinipite.

Alafu wakinadada sisi nao kuna saa tuko cheap πŸ™„ Yani nkiangalia hapo hao wanaofanya wakaka watoane damu na huyo aliyeinamishwa hapo on the other video nikiwacombine wote sijui kama hata 5M kwnye account wanazo lakini ndio wamejiassociate na watu wa ovyo hivyo πŸ˜”

Mungu atusaidie tu kwakweli
 
Mdada ukienda club na mambo ya hovyo lazima yakupate tu, hata uwe pisi mbovu namna gani ila club utaonekana pisi kali.

Bora usiwe mtu wa mienendo hiyo.
 
Taasisi ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi iko wapi?? Askari anaskika akisema kabisaa hiii siiachi yaani Video ya ngono na hakuishia hapo akairusha mtandaoni. Aibu sana kwa jeshi letu. Aibu sana hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…