Askari ameambiwa hana mamlaka, akajibu kwa kufyatua risasi hewani! Kisha akaanza kumsukuma Adam provocatively, ili Adam naye ajibu uchokozi huo kwa kurusha ngumi. Na kumbe Adam ana hekima, kwamba kama jibu la "huna mamlaka" ni kufatuliwa risasi hewani, basi akirusha ngumi atafyatuliwa ya kichwani! Huyu siyo polisi, ni bangi tupu!
Lakini hawa walionywa, kwamba haya mnayoshabikia au kunyamazia wanapofanyiwa wengine, kuna siku yatawarudia na hakuna atakayewatetea. Sijui kama wenzao waliomo mjengoni wanajifunza kitu hapa!