Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Askari yupo sahihi kufyatua risasi hewani ila hayo maneno yaliyokuwa yanamtoka mdomoni ndo yameondoa dhana yote ya kufyatua hewani....

Utafyatuaje risasi hewani kwa mazingira haya yaliyojitokeza?? kwani walikuwa watu wangapi hapo waliokusanyika na kusababisha amani ya aina yoyote ile kuvunjika??? Hii nchi tuna watu wa ajabu kweli kweli... Kuna hatua za kufuata hata kama raia anakuwa mbishi... Hizi kazi za kutumikia nchi inataka uvumilivu wa hali ya juu... nani anawalazimisha kuvichagua kama hamwezi??
 
Huyo askari (ukiacha aliyefyatua risasi) ana wasiwasi kweli. Anahofia mwenzake ataharibu. Amewahi kuondoa ushahidi (amechukua ganda la risasi iliyofyatuliwa). Duh...yaani huyo askari bangi angeweza kuleta madhara makubwa sana hapo.
 
Nadhani Kigoma ana matatizo. Na ndiyo maana aliibiwa hela Moro na changu.
 
mtu anasale za jeshi la polisi na bunduki tena mchana bado unatafuta kitambulisho.
Alafu kuwa na sale sio sababu then aliye ulizwa kitambulisho sio askari na majembe agent Baba VIP..!
 
Inawezekana hujui kama tunaandaa model ya kukagua matumizi sahihi sahihi ya lugha yetu adhimu, nyie msiojua lugha hii itabidi mtuonyeshe makaburi ya babu wa babu wa babu zenu. Huenda mkawa na lugha nyingine ya asili.
Hakuna mtu anayejua kiswahili 100% kwa sababu hata kiswahili siyo lugha yetu kwa 100% maneno mengine tumetoa lugha za wenzetu (tumetohoa, tumerudufisha n.k)
 
Huyo askari (ukiacha aliyefyatua risasi) ana wasiwasi kweli. Anahofia mwenzake ataharibu. Amewahi kuondoa ushahidi (amechukua ganda la risasi iliyofyatuliwa). Duh...yaani huyo askari bangi angeweza kuleta madhara makubwa sana hapo.
Ni kweli pamoja na kuchimba mkwara lakini. Huyu Askari alikuwa na tahadhali mno. Mara apande gari mara ashuke
 
Sikuizi ni mwendo wa kuwalaumu polisi tu.Yan mtu akisoma post inaneno polisi anaanza kuwatukana bila hata kufatilia undani wa habari.
 
Tunalo tatizo kubwa, pengine imekuwa sifa mojawapo ya kupandishwa cheo, Ni sababu IPI ilimfanya afyatue risasi hovyo? Hawana discpline ya silaha hata kidogo ni ujinga mtupu
 
Wanabodi.
Askari yule katika tukio la Adam Malima afutwe kazi kwa utovu wa nidham alioufanya, ametia dosari jeshi letu pendwa hivyo aubebe mzigo wake.
Umeandika kama vile kila mtu ameshuhudia hilo tukio mubashara!!
 
Sijui kama tunapowakabidhi silaha police wetu huwa pia tumeshawapima reasoning capacity ya muhusika. Naona hatari kubwa huko mbeleni. ...may be woga wangu tuuu.....may be...
 


Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.

Yalikuwa ni majibizano kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.

Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.

Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.

Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.
 
Huyo askari (ukiacha aliyefyatua risasi) ana wasiwasi kweli. Anahofia mwenzake ataharibu. Amewahi kuondoa ushahidi (amechukua ganda la risasi iliyofyatuliwa). Duh...yaani huyo askari bangi angeweza kuleta madhara makubwa sana hapo.
Hujui lolote katika ulinzi, ganda la risasi ni muhimu kuokotwa likitumika vibaya litaleta madhara pengine mtu kupoteza kazi.
 
Mdomo wako sio utendaji, mimi ni mwanaume najua sina ushabiki na mambo ya kijinga.
Watanzania mnjifanya kujua kila kitu, kutukana askari wakati mnalindwa na hao askari nyie ni pimbi sana.

Unajiita mwelevu ilihali ukiona mjusi unaogopa.
Mbona povu linakutoka kwani ulilazimishwa kuwa polisi
 
Kuna nchi fulani askari au mtu yoyote kuonyesha au kuweka bunduki , pastola adharani ni kosa la jinai, hii haijalishi kama ni askari au raia, na sio kwamba hasipo, sema hiki kitu hakitakiwi kuonekana haradhani kabisa kabisa…hapa kwetu aijui vipi …!
 
Back
Top Bottom