Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Huyo polisi anastahili kusimamishwa kazi.

Ndo mambo gani sasa hayo ya kufyatua risasi hewani kama siyo kutishia watu?

Ingekuwa ni juu yangu ningemfukuzia mbali kabisa maana hafai huyo....he is too trigger happy!

Tena hafai hata kidogo, ,,hana kabisa sifa ya kuwa askari,,,,,ni wakufukuziliwa mbali
 
Ishu ni hv, huyu ndugu malima jr alienda IOM akamuacha dereva wake kwenye gari, dereva akaegesha gari upande ambao kuna maduka na migahawa na ni upande ambao huwa hawakamati labda wakubabatishe mjinga mjinga, sasa mabwana wakubwa (Majembe) wakaja akawa anataka kukamata gari, dereva anamuuliza kitambulisho jamaa akagoma, sasa dereva akaanza kumfokea ndo wananchi wakajaa kwenye tukio, walipomuomba tena atoe kitambulisho akagoma ndo wakataka kumpiga, bahati walikuja na polisi ambao walikuwa kwenye gari, baada ya kelele polisi wakatoka kutuliza presha za wananchi. Mwenye gari (Malima) alipokuja akauliza kwa nn wanataka kukamata gari na kwa nn hawataki kutoa vitambulisho majibu hayakupatikana, Polisi wakapanda kwenye gari wakawa wanaondoka, sasa cha ajabu baanda ya mwendo waa sekunde 30 wakapaki gari pembeni wakaanza kujibizana upya ndo hapo dereva akapaniki na askari akapaniki jamaa akaamua kufyatua risasi juu watu hawakukimbia. Ikabidi Polisi wamchukue Malima Jr waende nae Kituoni.
Utasikia shitaka lake sasa
 
Kwa kweli sijaona ulazima wa huyo askari kutumia bunduki katika hilo tukio, ni ushamba na ubabe ulipitiliza, IGP amuwajibishe mara moja, kama wanaweza kudhalilisha watu waliowahi kuwa viongozi katika hii nchi itakuaje kwa sisi raia wa kawaida!
 
We bwana mdogo hivi unajua kuwa askari akishika siraha ya moto haruhusiwi kubishana na raia au kuonesha jazba za waziwazi namna ile
Hii ni kwa mujibu wa kitabu gani cha sheria mkuu? Kwa hiyo ukiwa na silaha inatakiwa uwe kama bubu.
 
Yani sijui hata Kama alipitia mafunzo huyu polisi, enzi zileeee kulikuwa na somo pale polisi la jinsi ya kuzuia hasira, na huyu zingekuwa zama zile tayari kazi alikuwa Hana kwa makosa kadhaa niliyoyabaini hapo.....
Inasikitisha sana
 
Wanabodi.
Askari yule katika tukio la Adam Malima afutwe kazi kwa utovu wa nidham alioufanya, ametia dosari jeshi letu pendwa hivyo aubebe mzigo wake.
 
Haku park sehemu isiyoruhusiwa, gari lilikuwa limeegeshwa na dereva akiwemo ndani, na liliegeshwa upande wenye maduka ambao unaruhusiwa, ila mara nyingi huwa wanapenda kusumbua na hata kusababisha wenye maduka kukosa wateja kwa kuogopa kukamatwa na hao majembe
Samahani ndugu hivi majembe ndio nini mnaniacha njia panda
 
Mh.Malima akibishana na Polisi kisa inadaiwa eti "Wrong Parking" kama kweli wrong parking na silaha juu ???
01d91af724ec739f3d22b991b3707293.jpg
1d165c2427f2db569a32c1193ab1756a.jpg
9b8edb5c0971ce15c9d9dbfd05202588.jpg
a1b2c900f80c4a93b3dd38c56570f39c.jpg
683fcea14b27eeb0849a5390138b1d54.jpg
 
Hivyo ndivyo polisi wetu wapopandwa na hasira na kuua raia wasio na hatia; baadae kuweza kupoteza ushaidi unasikia, polisi imefanikiwa kuuwa jambazi moja na mengine kutoweka na kutokomea kusikojulika baada ya jambazi kuanza kurushia polisi risasi. Polisi hao waliweka mtego na kuwanasa kabla ya kufanikiwa kuiba. Kumbe maskini ya mungu tukio halikuwa hivyo. Dhuu Tanzania bado tuna safari ndefu sana kupata haki ya kila mwenye haki.
Nimependa hiyo
 


Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.

Yalikuwa ni majibizano kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.

Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.

Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.

Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.

Umeeleza kishabiki, dhidi ya polisi. Jaribu kuwa mkweli.Polisi waliwatisha wananchi waliozunguka gari au walimtisha Malima ?
 
Watumishi wazamani msome alama za nyakati , kwenye serikali hiii watu wajifunze interest zake
 
Back
Top Bottom