Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

kama waliovamia clouds walichekewa, waliomtishia nape walichekewa , huyu askari sio wa kumlaumu sana. ameshajua status quo inataka nini.
 
Inashangaza sana askari junior kama huyu kufanya mambo ya ajabu yale...kwanza anasema ameapa hivi yeye na Malima nani hasa kala kiapo??? Na viapo vingapi hasa??? Kingine kuna haja gani kutumia risasi kama huna tishio la maisha?? Huku ukisisitiza serikali haiheshimiwi??? Hivi kweli yule askari ana mafunzo sahihi??? Naamini kuna haja ya kuweka sheria na mafunzo mapya na kuondoa kabisa mlolongo wa kikoloni ndani ya majeshi...hakuna alie salama huo ni ukweli.
Kula kiapo ndio kula nini? Hebu dadavua hicho alichokula malima na cha huyo askari tulinganishe.
 
Hii si ishara nzuri kwa nchi hata kidogo tunafika mahali tunakuwa sugu!nimesikia raia wanasema huna mamlaka!Askari anapiga risasi juu wanamuangalia utadhani ni manati au toy...hapa sasa siyo pazuri.
 


Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.

Yalikuwa ni majibizano kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.

Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.

Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.

Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.

Duuu!! Ndo matatizo ya undugunazation ktk serikal etu
 
Watu hamjifunzi, huyo dogo ana lalamika kwa sauti mbona hamheshimu serikali, akijua kabisa Magu akisikia hii issue atamtafuta. Hadi askari wanajua kuwa ukiitetea serikali hata kwa kuipaka matope unaonekana shujaa.

ofcoz dogo ameonyesha upumbavu wa hali ya juu na usio vumilika. mwenzake alikua smart sana.

Tusubiri Magu kuongelea hili jambo, najua akiona hii video atatoa machozi, tuombe asiseme ningekuepo ningempiga kamoja ...
 
Mmh aisee, malima kwa nini hafuati maagizo ya polisi, ingekuwa wa upinzani tungesikia mengine
 
Sasa hii ni full video au umeunganisha unganisha clips?
 
Kwa maelezo haya, polisi hajafanya kosa kabisa kufyatua risasi hewani.

Kwa sababu, naona maelezo hapo yanasema wananchi walikuwa Karibu kujichukulia sheria mikononi.

Hivyo, polisi kuokoa maisha ya aliyedhaniwa ni jambazi ili asitolewe roho.

Au mi nimeelewa tofauti!?

Katika uelewa wako na macho yako yameonaje hiyo video hapo, pale nani alisogea au uliona nani anataka kupiga Nani, ili useme alikuwa anatawanya watu waliotaka kujichukulia hatuwa mkononi?
 
Back
Top Bottom