Lipo tatizo kubwa,Watanzania hatupaswi kuishi kama wakimbizi {kiroho,kimwili,kisaikolojia}katika nchi yetu wenyewe.Mungu awajalie viongozi wetu hekima zaidi/Busara zaidi,Kuna vitendo vyapaswa kudhibitiwa mapema..Taswira ya taifa inabadirika taratibu kutoka kuwa taifa la amani kwenda kuwa taifa la wasiwasi na hofu..
Binadamu wote ni sawa ila Raia waandamizi katika vyama vya siasa na serikali {Viongozi wastaafu,Mawaziri wakuu wastaafu,Waliowahi kuwa mawaziri} wanapaswa kuthaminiwa na kuenziwa kwa namna moja hadi nyingine.Heshima kwao ni moja ya shukrani juu ya utumishi wao kwa taifa.
Wananchi hawapaswi kuzoeshwa matumizi yasio fuata taratibu ya siraha,mamlaka na nguvu.Tulizoea kusikia haya yakifanyika katika nchi zenye machafuko ama uasi usiokoma.Tusipoziba ukuta tutajenga ukuta.Tusiwakumbatie wachache wenye kuvunja sheria,mila na desturi za taifa kwa kuwapongeza,kuwapandisha vyeo ama kuwaficha.
''Mwenyezi Mungu nijalie uzima wa milele mara baada ya maisha ya hapa duniani ili nisiwe na hofu na wanaoweza kuua mwili huu wa damu na nyama bali nikuhofu wewe uwezae kuua hata roho/nafsi..''