Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Kwahiyo kama malima kadharau, ndiyo askari atumie silaha ya moto kutisha na baadae kufyatua risasi. Hatahivyo askari alazimisha watu watii serikali. Askari hakufanya reasonable action
 
Kafanya vizuri kuuliza kiongozi wa msafara,hata popote pale kwenye wengi lazima kuuliza nani msemaji yupo vizuri sana mh
 
Hawa viongozi wetu kauli zao mbovu sana na bahati yake ingekuwa mm hizo risasi ningepiga hata mguu mmoja ili iwe kesi kabisa, bunduki sio fimbo
Viongozi wetu wajiheshimu cheo cha baba sio cha familia.
 
Ajabu mlisema gari ilikuwa na dereva ndani kwanini huyo kijana wa majembe asimwambie tia gari lakini kwa akili ya kupata hela za bila jasho itakuwa alivamia dereca na kutaka kuchukua funguo kwa nguvu. Hawa majembe ni wahuni na utakuwa umebarikiwa manispaa huu uhuni
 
Mambo hayaamuliwi kwa hisia mdogo wangu. Polisi kuwa na uchungu ni dalili ya yeye kukosa control. Inanishangaza mnapowashangaa wananchi kutowapenda polisi huku matendo kandamizi hamyasemi.

Hakuna mtu anawapenda hao wanaokamata kamata magari ya watu huko peninsular. Watu hawa wa hovyo wasiolipa hata senti moja kodi ndio vinara wa kunyanyasa walipa kodi na sasa wanaongozana na polisi kufanya unyanyasaji. Nani anawapenda?
 
Hebu tafuta hiyo video uangalie basi
Nimeangalia vizuri, polisi amefyatua risasi
Ukweli usipingika ni kwamba huyo jamaa amewajibu nyodo kwa kua baba yake alikua mtu mkubwa kwenye system, kumbuka inauma sana mtu kukufanyia dharau uwapo katika eneo lako la kazi, mambo haya haya ndiyo yalipelekea Ditopile akampiga mtu risasi kisa anajua yeye ni mtu kutoka kwenye system na wengine anawaona kama vikaragosi, na watu wengi tumekua tukiwadharau polisi kwa kua vipato vyetu vinatupa kiburi.

Tusiegemee upande mmoja wa polisi, tujiulize chanzo cha polisi kukasirika ni nini? Kama yale majibizano yao tungeyasikia yote basi tungejua yule jamaa kamjibu nini polisi mpaka polisi kuchukia kiasi kile.

Hata wewe ungekua KK security ukijibiwa nyodo hata geti utagoma kufungua
 
Raia wanapoomba kumiliki silaha moja ya mambo wanayochunguzwa ni pamoja na ustahimilivu!Polisi hapaswi kuwa provoked kiasi cha kufyatua risasi hewani!Anapaswa apimwe akili
 
Mithali 27:12....jiwe ni zito na mchanga ni mzito... Lakini kukasirishwa kwa mpumbavu kuzito kuliko hivyo vyote viwili (uzito na mizigo) [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji779] [emoji779] [emoji779] [emoji115] [emoji115] [emoji115]
 
Kwanza mhusika mwenyewe nasikia alimuua baba yake halafu anadharau police hii haikubaliki jpm nyonga watu
 
Kwahiyo mtu akikuuliza mkuu wa masafara yuko wapi ni dharau? Hivi nyie ni nani aliewashikia akili zenu? Au ndio jinsi mlivyozaliwa?
Polisi anapiga risasi hewani halafu unasema eti alidharauliwa.
Kwa hakika kuna watu mkuu, sijui inakuwaje. Mpaka unawakatia tamaa. Hata jambo la kipuuzi linatetewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…