Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Masaki, Dar: Adam Malima atishiwa kwa Bunduki, Risasi zarindima kama Njugu

Kwahiyo kama malima kadharau, ndiyo askari atumie silaha ya moto kutisha na baadae kufyatua risasi. Hatahivyo askari alazimisha watu watii serikali. Askari hakufanya reasonable action
 
Kafanya vizuri kuuliza kiongozi wa msafara,hata popote pale kwenye wengi lazima kuuliza nani msemaji yupo vizuri sana mh
 
Hawa viongozi wetu kauli zao mbovu sana na bahati yake ingekuwa mm hizo risasi ningepiga hata mguu mmoja ili iwe kesi kabisa, bunduki sio fimbo
Viongozi wetu wajiheshimu cheo cha baba sio cha familia.
 
Ajabu mlisema gari ilikuwa na dereva ndani kwanini huyo kijana wa majembe asimwambie tia gari lakini kwa akili ya kupata hela za bila jasho itakuwa alivamia dereca na kutaka kuchukua funguo kwa nguvu. Hawa majembe ni wahuni na utakuwa umebarikiwa manispaa huu uhuni
 
ulimsikia askari aliyefyatua risasi akiongea kwa uchungu "kwanini hamuheshimu serikali??"
Tanzania viongozi wanajiweka matiti mbele na usiye kiongozi unanyanyaswa.
Wote tuwe watii wa sheria......tusiwaangalie polisi kwa makengeza kwakuwa kila mara wako wrong
Mambo hayaamuliwi kwa hisia mdogo wangu. Polisi kuwa na uchungu ni dalili ya yeye kukosa control. Inanishangaza mnapowashangaa wananchi kutowapenda polisi huku matendo kandamizi hamyasemi.

Hakuna mtu anawapenda hao wanaokamata kamata magari ya watu huko peninsular. Watu hawa wa hovyo wasiolipa hata senti moja kodi ndio vinara wa kunyanyasa walipa kodi na sasa wanaongozana na polisi kufanya unyanyasaji. Nani anawapenda?
 
Hebu tafuta hiyo video uangalie basi
Nimeangalia vizuri, polisi amefyatua risasi
Ukweli usipingika ni kwamba huyo jamaa amewajibu nyodo kwa kua baba yake alikua mtu mkubwa kwenye system, kumbuka inauma sana mtu kukufanyia dharau uwapo katika eneo lako la kazi, mambo haya haya ndiyo yalipelekea Ditopile akampiga mtu risasi kisa anajua yeye ni mtu kutoka kwenye system na wengine anawaona kama vikaragosi, na watu wengi tumekua tukiwadharau polisi kwa kua vipato vyetu vinatupa kiburi.

Tusiegemee upande mmoja wa polisi, tujiulize chanzo cha polisi kukasirika ni nini? Kama yale majibizano yao tungeyasikia yote basi tungejua yule jamaa kamjibu nini polisi mpaka polisi kuchukia kiasi kile.

Hata wewe ungekua KK security ukijibiwa nyodo hata geti utagoma kufungua
 
Dharau hizi hizi dhidi ya polisi ndizo zimemfikisha Manji katika usumbufu ule unaomuandama sasa hivi, let say Bashite alikosea kumuita kupitia media, Manji kwakua alijua yeye ni maarufu akaita media kuongea na kutoa kejeli, kafika police wapambe wake wanasafisha gari kama ishara ya dharau.

Jamani hakuna anayependa kudharauliwa wala kupandishiwa sauti awapo eneo lake la kazi, hata uende getini umkute KK security ukionesha dharau/kejeli ya kazi yake lazima atalazimika kukuzuia usiingie na pengine utazuka ugomvi.

Watanzania mara zote tunasema polisi ndio watu wabaya lakini mabaya yetu hatuyasemi, hata wewe unayedhani polisi wanakosea kila siku ukipata nafasi ya kuwa polisi hutakubali kudharauliwa mtambueni polisi kama kiongozi wa ulinzi na usalama sasa mnapoonesha dharau lazima atakwazika(human nature)
Raia wanapoomba kumiliki silaha moja ya mambo wanayochunguzwa ni pamoja na ustahimilivu!Polisi hapaswi kuwa provoked kiasi cha kufyatua risasi hewani!Anapaswa apimwe akili
 
Ukisikia mwalimu anamfokea kwa nguvu mwanafunzi ati KWANINI HUNIHESHIMU,.....jua Mkuu wa shule aidha analewa gongo au ni swahiba wa mwanafunzi!!

"Kwanini hamuiheshimu seriikali??!!!.."...Hili ni swali la mtu aliyekata tamaa!!!

Mithali 27: 12 Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo,
lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito
zaidi kuliko hivyo vyote viwili.
Mithali 27:12....jiwe ni zito na mchanga ni mzito... Lakini kukasirishwa kwa mpumbavu kuzito kuliko hivyo vyote viwili (uzito na mizigo) [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji87] [emoji779] [emoji779] [emoji779] [emoji115] [emoji115] [emoji115]
 




Mchana huu pamesikika milio ya risasi maeneo ya Masaki karibu na Double tree Hotel.

Yalikuwa ni majibizano kati ya Majembe Auction Mart waliokuwa wameambatana na Polisi walipojaribu kukamata gari lilokuwa limeegeshwa pembeni ya barabara hali ya kuwa Dereva yupo ndani.

Inasemekana gari lilikuwa la Mwanae Kighoma Malima aliyeenda IOM kufatilia ishu zake.

Mtu wa Majembe akavamia gari hilo na alipodaiwa kuonyesha vitambulisho aligoma kutoa ndio wananchi walipolizingira gari wakitaka kumpiga wakijua ni jambazi.

Polisi aliingilia kati na katika majibizano akafyatua risasi juu kumtishia ndugu Malima aliyekuwa hana hata silaha wala hakukuwa na mwananchi aliyekuwa na silaha.

Adam Kighoma Malima alikuwa mbunge wa jimbo la Mkuranga na Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, enzi za Kikwete. Anatokea katika chama cha CCM.

Kwanza mhusika mwenyewe nasikia alimuua baba yake halafu anadharau police hii haikubaliki jpm nyonga watu
 
Kwahiyo mtu akikuuliza mkuu wa masafara yuko wapi ni dharau? Hivi nyie ni nani aliewashikia akili zenu? Au ndio jinsi mlivyozaliwa?
Polisi anapiga risasi hewani halafu unasema eti alidharauliwa.
Kwa hakika kuna watu mkuu, sijui inakuwaje. Mpaka unawakatia tamaa. Hata jambo la kipuuzi linatetewa.
 
Back
Top Bottom