Achana na maelezi, je kwa ulichokiona unadhani kulikua na ulazima gani wa kupiga risasi?
Kwa ulichokiona, kulikuwa na ulazima gani kwa hao jamaa kupaki gari mahala siyo ruhusa kupaki!?
Kwa ulichokiona, kwa nini waongee hivyo kuwadharau polisi!?
Kwa ulichokiona, kwa nini wasitii Sheri na kuwa waadilifu!?
Polisi alifanya hivyo kukomesha midomo na wanaopenda kufata gari lao kwenda kituo cha polisi.
Ila polisi wetu wasilaumiwe
kwa sababu, nchi zingine huwa watu wanatii sheria bila shuruti mfano, kama ni no parking ( No ) wenzetu hawapaki kabisaa sasa sisi huko Tanzania inakuwaje!?
Tuache kutetea wavunja sheria kwa sababu ya vyeo, fedha au sababu zingine zingine tunazozijua.
Mfano, Barabara nyingi hapo Dar zimewekewa uzio wa kukataza kukatisha zile bustani sasa angalia barabara ya Mandela, Nyerere, kijitonyama kwenda city centre kila bustani hizo waenda kwa miguu wanakatiza na wenye magari wanazigonga.
Swali, mbona pale Mwenge mkono wa kushoto pana hizo bustani lakini watu hawakatishi na Magari hayagongi zile bustani!?
Jibu lake pale bustani ya Mwenge pana kakibao kadogo sana kameandikwa ONYO kukatisha bustani (JWTZ) na hakuna kweli anayegusa wala gari halijawahi kugusa wala kugonga ile bustani.
Sasa kwa nini, hao wasitii Sheria!?
Hili jambo, ukiliangalia kwa chuki zako kwa polisi utaona kuwa polisi kakosea ila hekima ya Malina ilipungua pale yeye Kama kiongozi tena mkubwa alipaswa kuonesha weredi na uwezo wa kuchambua mambo na hekima.
Acha , nisiseme sana ila haya mambo yanahitaji hekima na kutii sheria au amri bila shuruti.